Mgeja: Kilango sio saizi yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeja: Kilango sio saizi yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 29, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Khamis Mgeja, amesema hana nia ya kufanya malumbano na Anne Killango Malecela kwa kuwa halingani naye na anamheshimu sana .

  “Sitaki kufanya malumbano ya kisiasa na Anne kwa kuwa siyo ‘size’ yangu…namshangaa kunijia juu na kunitolea maneno ya kashfa kwa mambo yasiyomhusu,” alisema na kuongeza kwamba hata imani yake ya dini inamzuia kufanya malumbano na mwanamke.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam , Mgeja alisema alieleza nia yake ya kutaka mmoja wa wanachama ambaye ni kiongozi aache kutoa maneno yasiyo na heshima dhidi ya vikao halali vya maamuzi vya CCM.

  Hivi karibuni, Mgeja alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza nia ya kuwasilisha hoja dhidi ya Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwenye kikao cha NEC akimtuhumu kuendeleza mgawanyiko ndani ya Chama. Mgeja alisema anawasilisha hoja hiyo ili Chama kiiweke kama agenda kusudi Sitta aweze kuthibitisha madai yake kuwa alienguliwa kuwania uspika kwa hila na Kamati Kuu ya CCM.

  Baada ya taarifa hiyo, Anne alikaririwa akimjibu Mgeja kuwa aachane na Sitta na kuwa anapaswa kueleza kuhusu sababu gani zilizomfanya akiwa kiongozi akapoteza majimbo manne mkoani Shinyanga.

  Mgeja alisema Anne ameshindwa kuelewa kuwa Tanzania imo kwenye ushindani wa vyama vingi ambako kuna kushinda na kushindwa na huko ndiko kukomaa kwa demokrasia, hivyo asianze kutafuta mchawi na kumuomba ajifunze kutoka nchi zilizopoteza dola kama Kenya , Zambia na Uingereza ambako vyama tawala viliondolewa.

  Kuhusu tuhuma kuwa ametumwa na baadhi ya watu, Mgeja alisema: “Napenda kumuondoa mashaka kuwa mimi hakuna mtu yeyote au genge lolote la kunituma kwani ninao uwezo binafsi wa kujitegemea kifikra na kimtazamo na najitosheleza, hivyo anachokifanya ni sawa na mchezo wa watoto kumuangusha mtu mkubwa ambaye hawezi kutishiwa nyau.”

  Aliongeza kuwa anashangaa kuona kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Anne na Sitta kiasi cha mbunge huyo wa Same Mashariki kuamua kumjibia Sitta wakati hawatoki mkoa mmoja, sio msemaji wake na wala sio wakili wake na kuwa alichopaswa kumsaidia hapo ni kujibu hoja ya msingi ya kuondolewa kwa hila.

  “Nikitaka kujibu ya Anne Killango ninaweza kuanzia Zanzibar hadi Bara na namshangaa kuulizia kupoteza majimbo Shinyanga, mbona haulizi Pemba tulikopoteza viti vyote, Kigoma, Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Iringa, Mara na Kilimanjaro anakotoka na ambako Mgeja hakuwepo?” alihoji Mwenyekiti huyo wa Shinyanga.
  source mwananchi
   
 2. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata huyo Six sio saiz yako!, Saiz yako ni wajumbe wa mitaa, na wenyeviti wenzio wa mikoa. Huyo Six waachie akina Lowassa, Chenge na JK. Hata Lisupu La Ajabu La Kamba sio saiz yake, sembuse weye??!!

  Haya, na kwani imani ya dini yako inaruhusu malumbano aina gani??? Kwenye vikao vya chama ajenda, hoja binafsi ni bungeni pekee, uko bungeni weye???
   
Loading...