Mgao wa umeme wa masaa 24 waja

Mgao wa umeme wa masaa 24 waja

tamaudj

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2013
Posts
270
Reaction score
108
Kuna kila dalili kwamba kuna mgao mkali sana unakuja kwani dalili hizi zipo wazi kutokana na halia halisi ya kinachotokea sasa.Kila siku sasa kwa takribani mwezi umeme unakatika hovyo si mchana si usiku,kuna nini TANESCO?
 
Mkuu nilidhani umekwisha lithibitisha hili, kumbe ni swali unauliza...
 
Mkuu nilidhani umekwisha lithibitisha hili, kumbe ni swali unauliza...

Nakerwa na tabia hii ya katikakatika mkuu,yaani nakerwa mnoooo,ndo maana nimeiweka kwenye tetesi.
 
kuna kila dalili kwamba kuna mgao mkali sana unakuja kwani dalili hizi zipo wazi kutokana na halia halisi ya kinachotokea sasa.kila siku sasa kwa takribani mwezi umeme unakatika hovyo si mchana si usiku,kuna nini tanesco?

usiseme unakuja mgao umeshaanza muda sana watu tunalala giza kilasiku
 
Na uje tu hata leo tumeshajizoelea shida.
 
Nakerwa na tabia hii ya katikakatika mkuu,yaani nakerwa mnoooo,ndo maana nimeiweka kwenye tetesi.
...ni kweli ndugu inakera mno....miaka 53 baada ya uhuru mambo "shaghalabaghala".....halafu pesa nyingi inaelekezwa kwenye posho za wateule wachache na safari nyingi za hovyo hovyo...hata hivyo "mgao" mmbaya zaidi ni kuishabikia "serikali hii dhalimu"....
 
Bei imepanda na hapo hutawaona viongozi wakitoa majibu ya kueleweka zaidi ya kusikia sababu za kisiasa. Maana kama ni bei wametupandishia lakini matatizo yako palepale. Tunawaomba viongozi mtupatie mikataba ya umeme inasemaje maana hapa naona tunapuuzwa sasa.
 
mawaziri mzigo wapo wengi, wa kwanza kabisa ni professor muhongo, maneno anayosema na hali halisi ya umeme ni vitu viwili tofauti na sijui kwa nini hatuandamani nchi nzima kwa matatizo kama hayo, bei juu, halafu unaishi gizani, halafu nyanya zetu kwenye mafriji zinaoza
 
Kama ccm ina bado moyo wa huruma kwa Tz, tunawaomba jamani pamoja na unyonyaji huu tuleteeni basi vyombo vya sola. Wengine tujifariji kidogo kwa sola hatutaumizwa kiasi hiki mnacho tuumiza.
Kweli ccm msijinyonge wazi wazi hivi. Kama ni kuwanyonya wananchi hapa mmezidiiiiii Pole zenu. 2015 mtawaeleza nini wananchi??? Umeme ni kitu cha luxury?? Diesel ni luxury, kuwa na gari ni luxury, hospitali kununua dawa ni luxury, ni nini cha muhimu kwa wananchi kwenu?? This is a shame.
55 yrs ya uhuru na bado mnaona umeme ni luxury? JK unaidhinisha matrilion kwa wabunge ili kuwanyamazisha wasipate la kuwaambia wananchi?? Pole zako na lichama lako. I LAY ALL THE BLAMES ON YU AND YOUR CCM
 
Duuuh Tanzania yangu jamani kila cku majanga hayapungui sijui tutafika tukiwa na hali gani kwa kweli
 
nakuunga mkono hapa nilipo sasa umeme kushney na haieleweki utarudi muda gani! Shughuli zinakwama
 
mawaziri mzigo wapo wengi, wa kwanza kabisa ni professor muhongo, maneno anayosema na hali halisi ya umeme ni vitu viwili tofauti na sijui kwa nini hatuandamani nchi nzima kwa matatizo kama hayo, bei juu, halafu unaishi gizani, halafu nyanya zetu kwenye mafriji zinaoza

bwana MENGI alishasema prof.muhongo ni muongo.
 
wapi huko? me kwangu kila siku umeme upo
 
Jana jioni nyumbani hapakuwa na umeme, naingia ofisini leo asubuhi umeme hamna...mwisho wa mwezi kulipa bili kama kawa...shame!..
 
Tuvute subira! Uchumi wa gesi utamaliza tatizo hili na litabaki kuwa historia.
 
Tuvute subira! Uchumi wa gesi utamaliza tatizo hili na litabaki kuwa historia.

Hata siku ileee Kikwete alisema kampuni ya umeme toka USA inakuja na suala la umeme wa mgao itakua historia,CCM Washenzi sana na ahadi za kijambazi!! Hapa Tanga tayari wameshaukata!!!
 
karibu siku ya 3 leo, usiku wa manane lazma wakate kidogo mpaka alfajiri.
 
Back
Top Bottom