Hakuna mgao kwisha mpaka tupate watu serious wa kuamua na kutekeleza. Nina maana mpaka watanzania tutakapoamua kufanya mahadiliko ya kweli.
Stori kila siku ni zilezile Mara maji yamekwisha mtera, Mara magugu bwawani, Mara miundombinu chakavu, ttansfoma kubwa imeungua n.k n.k. Ni maajabu kumaliza wiki 1 bila umeme kukatika! Na unaweza katika ns kurudi hata Mara 3 kwa siku!. Ajabu ya Musa na Tanzania. Hivi hatuwezi Fanya vizuri zaidi ya hapo au ndo akili yetu imegotea hapo? Mimi nawalaumu watawala wetu wa sasa kwa kuwa ndio watekelezaji wa sera walizojipangia/ walizopangiwa. Hawawazi kingine Bali ufisadi Tu na ndio maana tupo hapa tulipo. Miradi ya uneme ni ya pesa nyingi. Ukifiatilia kwa makini unagundua kuwa kila mradi Jamaa wameweka ndoano zao kila upande- UFISADI TUPU...