Mgao wa umeme mikoa mbalimbali

Mgao wa umeme mikoa mbalimbali

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Maelezo kuhusu Hali ya Umeme kwa baafhi ya Maeneo Mkoa wa Arusha.

Shirika la Umeme linapenda kueleza kile kinachoendelea mkoani Arusha kama ifutavyo; Eneo la Olasiva, Kwa kuanzia tunamalizia, mradi wa Olasiti Meckson school wiki hii. Hivyo wateja wa eneo Hilo watapata umeme mzuri. Pia miradi wa Sanawari Kati na shangalai uko Kwenye hatua za mwisho kufikia tarehe 15.12.2015 itakuwa imekamilika. Mradi wa kuboresha, huduma Olasiva uko 40% hivyo mwisho wa mwezi huu, tunaimani kuukamilisha.

Kumalizika kwa miradi hapo juu ambayo tayari imeanza, ulitatupa nafasi kuanza miradi ya Olasiti Kati, Ngaramtoni, na Engosheratoni. Ni matumaini ya mkoa tatizo la umeme mdogo litakuwa historia ndani ya miezi mitatu ijayo. Asante.
Hapana mmetutesa vya kutosha tangu june alafu unakuja na maelezo yenu hapa mpaka watu tunaisi tunasomeshwa namba kisa tu arusha ni mkoa wa upinzani.Kama mnakata mchana mzima kwanini msiwashe kuanzania saa 1 usiku mpka saa moja asubui siku inayafuata,Umeme auwaki mchana auwaki usiku alafalu unakuja na maelezo hapa yako ebu jiulize wanaouza samaki na bidhaa za kukaa kwenye majokofu wafanyeje,kweli na elimu yenu akumfundishwa plan b when plan a fail,kweli kweli unaweza kuja na majibu rahisi hivyo au mnafikiri kila mtu anauwezo wa kumili generator na kulihudumia sasa si bora mseme kuna mgao then tuamie kwenye solar energy tuache kuwategemea kabisa au mnataka watalii wanaokuja wakirudi makwao waseme huku kuna shida ya umeme kitu ambacho kinaleta impact kwenye uchumi.Mimi binafsi naumia sana na huu mgao sana sana sana.
 
Yaani mgao mikoani ni balaa shinyanga,tabora kila siku wanalala bila umeme,wanadanganya eti wanabadilisha nguzo.Nguzo hata usiku?
 
Kwa staili hii ya migao ya umeme Tanzania ya Viwanda ni ndoto za mchana, Mgao una Mwaka sasa tangu uanze na hakuna dalili za mgao kuisha na hari inazidi kuwa mbaya sana,
 
Nilisha amua ku invest kwenye solar toka ule mgao wa mara ya kwanza.
Kuna product kibao za kichina zinazoweza ku replace karibia kila kitu cha ndani kinachotumia umeme.
Pia kuna makampuni ya solar kibao Arusha.
Ni bora kujipinda na solar maana huu umeme wa tanesco sidhani kama utakaa utuliage.
 
Aya sasa ni saa nne na nusu na hamna umeme apo walikata saa 11 asubuh Arusha jiji
 
Yaani mgao mikoani ni balaa shinyanga,tabora kila siku wanalala bila umeme,wanadanganya eti wanabadilisha nguzo.Nguzo hata usiku?

Mbeya ndo usiseme. sio Mbarali wala tunduma kote ni sheedah
 
Habarini humu ndani,kwakweli tanesco mkoani morogoro mjini mnakera sana wananchi ,mnakata umeme asubuhi mnarudisha saa 6 usiku alaf ikifika saa 12 asbh mnakata tena . mnarudisha tukiwa tumelala unatusaidia nini sasa,leo jmoc weekend mmeukata mapema sa 12 asubuh na wakati jana sa 6 usiku ndio mlirudisha mna maana gani.
Ni nini tatizo si mngetangaza kwenye vyombo vya habari basi tujue
Wananchi tunashindwa kuangalia hata taarifa ya habari kila siku ,umeme tunalipia lakini hakuna faida yeyote mpo kimya hamsemi tatizo kazi kukata umeme tu,mnakera sana tanesco
 
Habarini humu ndani,kwakweli tanesco mkoani morogoro mjini mnakera sana wananchi ,mnakata umeme asubuhi mnarudisha saa 6 usiku alaf ikifika saa 12 asbh mnakata tena . mnarudisha tukiwa tumelala unatusaidia nini sasa,leo jmoc weekend mmeukata mapema sa 12 asubuh na wakati jana sa 6 usiku ndio mlirudisha mna maana gani.
Ni nini tatizo si mngetangaza kwenye vyombo vya habari basi tujue
Wananchi tunashindwa kuangalia hata taarifa ya habari kila siku umeme tunalipia lakini hakuna faida yeyote mpo kimya hamsemi tatizo kazi kukata umeme tu,mnakera sana tanesco
Ni kero hadi kichefuchefu. Wanaendesha shirika kama familia yao. Hawaogopi madhara wanayosababishia jamii kwa kukatakata umeme.nilidhani watabadirika awamu ya tano kumbe mambo ni yaleyale
 
Nasikitika kukatika katika kwa Umeme ovyo katika Mikoa ya Morogoro, Tabora ,Pwani na kwengineko,tuliambiwa ifikapo Mwezi September 2015 tatizo la umeme litak uwa historia kutoka na kupatikana wa gesi katika mitambo kadhaa lakini hali imekuwa ileile,Umeme unakatika saa kumi na moja Asubuhi unarudi saa saba usiku,si jumamosi wala Jumapili !Ubabaishaji huu utaisha lini?
 
umeme umekatika saa moja asubuhi ukarudishwa saa nane usiku sasa wamekata tena saa moja asubuhi hawa jamaa inabidi tumbuatumbua majipu iwakute na wenyewe kwa style hii
 
umeme umekatika saa moja asubuhi ukarudishwa saa nane usiku sasa wamekata tena saa moja asubuhi hawa jamaa inabidi tumbuatumbua majipu iwakute na wenyewe kwa style hii

Wapi huko mkuu........?.....
nilipo mimi full manishati.........
 
Tanesco Mbeya mtupe majibu. Haiwekani mwezi Wa nne sasa tunatumia generator ofisini.
 
Back
Top Bottom