Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Mr. Mramba amesahau kumfukuza kazi Meneja wa TANESCO mkoa wa Arusha hususani manispaa.
Baada ya kuanza kwa mvua za vuli Arusha tumerudi tena kwenye mgao mkubwa wa umeme ambao hauna ratiba inayoeleweka (mara ukatike saa 6 mchana, saa 11 asubuhi au jioni saa 12 , saa 1 jioni) Kwa ufupi tangu June mwaka huu Arusha iko kwenye tatizo kubwa la kukatika umeme na liliisha wakati wa uchaguzi lakini limerudi tena kwa nguvu.
Ni kana kwamba Meneja wa TANESCO Arusha hafanyi lolote kuondoa hali hii ambayo wakazi wengi wameiona kama mambo ya maksudi. Mfano Manyunyu tu yakianza lazima hapa arusha umeme ukatwe.
Umeme wa Arusha hauwaki ikiwepo mvua ni lazima ukatike na hata mvua ikikatika saa 6 mchana lazima umeme urudi saa moja jioni. Hata ikitokea manyunyu yameanza yakakatika baada ya dakika 10 basi hiyo ni sababu tosha ya kukata umeme kwa masaa 7.
Hii kwangu ni uzembe wa meneje ambaye hajawahi toa ufafanuzi kuhusu hili tatizo.
Timu ya kukata umeme iko makini na ina training kuliko ile ya kurudisha umeme. Yaani imekuwa kana kwamba kazi ya Meneja TANESCO Arusha ni kukata umeme.
Tunataka kujua mgao wa umeme Arusha utaisha lini[/
Upelekaji Umeme Katika Makao Makuu ya Wilaya na Vijijini
Serikali ilianzisha rasmi Mfuko na Wakala wa Nishati Vijijini mwezi Oktoba, 2007. Lengo ni kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika Makao Makuu ya wilaya na vijijini, na hivyo kufikia asilimia 36 ya wananchi walioungashiwa umeme mwaka 2015. Katika kufikia lengo hili na kutekeleza Ibara ya 63(c) ya Ilani ya 2010 ? 2015 ya CCM, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imepata mafanikio yafuatayo:
(i)Kukamilika kwa upelekaji umeme katika makao makuu ya wilaya kumi na saba (17). Wilaya hizo ni Bahi, Kasulu, Kibondo, Kilindi, Kilolo, Kishapu, Ludewa, Mbinga, Mkinga, Namtumbo, Ngorongoro, Nkasi, Rorya, Simanjiro, Songea, Sumbawanga na Uyui. Kazi hiyo pia ilihusisha ufungaji wa jenereta na ujenzi wa njia za umeme kwa ajili ya kusambaza katika maeneo husika. Aidha, katika kipindi hicho jumla ya vijiji 106 katika mikoa mbalimbali nchini vimepatiwa umeme. Pia mpaka sasa makao makuu ya mikoa yote Tanzania Bara na jumla ya makao makuu ya wilaya 119 kati ya 135 yamepatiwa umeme.
(ii)Mikakati ya Kupunguza Gharama za Kuunganisha Umeme kwa Wateja, Kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata na waliofikiwa na umeme: Katika kutekeleza azma yake ya kutimiza lengo la asilimia 30 ya wananchi watakaounganishiwa umeme ifikapo Mwaka 2015, Serikali ilipunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wananchi. Katika punguzo hilo, mathalan gharama ya kuunganishwa umeme wa njia moja (single phase) kwa wateja wadogo mijini na vijijini ilipungua kwa wastani wa kati ya asilimia 30 na 77. Kutokana na juhudi hizo za Serikali, idadi ya Watanzania wanaopata umeme imeongeka kutoka asilimia 11 Mwaka 2005?? hadi kufikia asilimia 24 mwaka 2015. Pia jitihada hizo zimewezesha Watanzania asilimia 36 kufikiwa na miundombinu ya umeme.