Mgao wa umeme mikoa mbalimbali

Mgao wa umeme mikoa mbalimbali

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
5,182
Reaction score
2,330
Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Mr. Mramba amesahau kumfukuza kazi Meneja wa TANESCO mkoa wa Arusha hususani manispaa.

Baada ya kuanza kwa mvua za vuli Arusha tumerudi tena kwenye mgao mkubwa wa umeme ambao hauna ratiba inayoeleweka (mara ukatike saa 6 mchana, saa 11 asubuhi au jioni saa 12 , saa 1 jioni) Kwa ufupi tangu June mwaka huu Arusha iko kwenye tatizo kubwa la kukatika umeme na liliisha wakati wa uchaguzi lakini limerudi tena kwa nguvu.

Ni kana kwamba Meneja wa TANESCO Arusha hafanyi lolote kuondoa hali hii ambayo wakazi wengi wameiona kama mambo ya maksudi. Mfano Manyunyu tu yakianza lazima hapa arusha umeme ukatwe.

Umeme wa Arusha hauwaki ikiwepo mvua ni lazima ukatike na hata mvua ikikatika saa 6 mchana lazima umeme urudi saa moja jioni. Hata ikitokea manyunyu yameanza yakakatika baada ya dakika 10 basi hiyo ni sababu tosha ya kukata umeme kwa masaa 7.

Hii kwangu ni uzembe wa meneje ambaye hajawahi toa ufafanuzi kuhusu hili tatizo.
Timu ya kukata umeme iko makini na ina training kuliko ile ya kurudisha umeme. Yaani imekuwa kana kwamba kazi ya Meneja TANESCO Arusha ni kukata umeme.

Tunataka kujua mgao wa umeme Arusha utaisha lini
 
Unawazia wenzako tu kufukuzwa. Ungekuwa wewe ungekuwa tayari kufukuzwa?
 
Unawazia wenzako tu kufukuzwa. Ungekuwa wewe ungekuwa tayari kufukuzwa?

Afukuzwe kwa sababu alitakiwa ahakikishe umeme unawaka lakini anachosimamia sasa ni kuhakikisha umeme unakatwa na haurudi mapema kwa hiyo mtu wa namna hiyo unataka afanywe nini?

For six months jjij kama la Arusha umeme haupo wa uhakika watu wamepata hasara za kutosha tunahitaji mtu mwenye akili mbadala atakayewaza solution badala ya problems
 
sisi huku tanga tushazoea bado kuchoka tu,umeme unakatika mpk tunatia adabu
 
Unawazia wenzako tu kufukuzwa. Ungekuwa wewe ungekuwa tayari kufukuzwa?

Hujui adha wanayopata wakazi wa Arusha wewe. Kwa mfano jana umekatika mara kadhaa ukakatika tena saa moja jioni hadi saa 2. Ilipofika saa 11:30 asubuhi leo umeme ukakatwa na hakuna maelezo hakuna nini. Ni bora wangezima umeme kabisa wamalize tatizo for good.

Kama mtu hawezi kusimamia kazi inayomweka mjini ila anataka kila mwezi aone mshahara kwenye akaunti huyo ni mwizi na dawa ya mwizi ni kumfukuza tu
 
Huyu Meneja utakuta ni wale wafanya kazi walioanza kwa vyeo vya kishoka, mafundi wa kawaida hadi ngazi ya meneja kwa hiyo utendai wao ni ule ule.
 
Net group solutions walipokuja improvement ilikuwa kubwa na hata tukasahau kitu kinaitwa kukatikati kwa umeme iwe mvua iwe jua. Pia wakati Masasi akiwa Meneja ilikuwepo improvement kubwa na huyu mzee alikuwa serious.
Kinachokata umeme Arusha siyo tatizo la miundombinu bali Meneja wa Arusha hayuko serious na hata siku moja hatumii muda kutafuta solution kwani yeye ni business as usual type

Umeme wa Aru
 
Arusha tunateseka sana wakati Mramba alisema ikifika November tutakuwa tuna enjoy umeme wa Gesi na suala la kukatika katika litabaki kwenye vitabu vya historia
 
Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Mr. Mramba amesahau kumfukuza kazi Meneja wa TANESCO mkoa wa Arusha hususani manispaa.

Baada ya kuanza kwa mvua za vuli Arusha tumerudi tena kwenye mgao mkubwa wa umeme ambao hauna ratiba inayoeleweka (mara ukatike saa 6 mchana, saa 11 asubuhi au jioni saa 12 , saa 1 jioni) Kwa ufupi tangu June mwaka huu Arusha iko kwenye tatizo kubwa la kukatika umeme na liliisha wakati wa uchaguzi lakini limerudi tena kwa nguvu.

Ni kana kwamba Meneja wa TANESCO Arusha hafanyi lolote kuondoa hali hii ambayo wakazi wengi wameiona kama mambo ya maksudi. Mfano Manyunyu tu yakianza lazima hapa arusha umeme ukatwe.

Umeme wa Arusha hauwaki ikiwepo mvua ni lazima ukatike na hata mvua ikikatika saa 6 mchana lazima umeme urudi saa moja jioni. Hata ikitokea manyunyu yameanza yakakatika baada ya dakika 10 basi hiyo ni sababu tosha ya kukata umeme kwa masaa 7.

Hii kwangu ni uzembe wa meneje ambaye hajawahi toa ufafanuzi kuhusu hili tatizo.
Timu ya kukata umeme iko makini na ina training kuliko ile ya kurudisha umeme. Yaani imekuwa kana kwamba kazi ya Meneja TANESCO Arusha ni kukata umeme.

Tunataka kujua mgao wa umeme Arusha utaisha lini[/
Upelekaji Umeme Katika Makao Makuu ya Wilaya na Vijijini
Serikali ilianzisha rasmi Mfuko na Wakala wa Nishati Vijijini mwezi Oktoba, 2007. Lengo ni kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika Makao Makuu ya wilaya na vijijini, na hivyo kufikia asilimia 36 ya wananchi walioungashiwa umeme mwaka 2015. Katika kufikia lengo hili na kutekeleza Ibara ya 63(c) ya Ilani ya 2010 ? 2015 ya CCM, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imepata mafanikio yafuatayo:

(i)Kukamilika kwa upelekaji umeme katika makao makuu ya wilaya kumi na saba (17). Wilaya hizo ni Bahi, Kasulu, Kibondo, Kilindi, Kilolo, Kishapu, Ludewa, Mbinga, Mkinga, Namtumbo, Ngorongoro, Nkasi, Rorya, Simanjiro, Songea, Sumbawanga na Uyui. Kazi hiyo pia ilihusisha ufungaji wa jenereta na ujenzi wa njia za umeme kwa ajili ya kusambaza katika maeneo husika. Aidha, katika kipindi hicho jumla ya vijiji 106 katika mikoa mbalimbali nchini vimepatiwa umeme. Pia mpaka sasa makao makuu ya mikoa yote Tanzania Bara na jumla ya makao makuu ya wilaya 119 kati ya 135 yamepatiwa umeme.
(ii)Mikakati ya Kupunguza Gharama za Kuunganisha Umeme kwa Wateja, Kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata na waliofikiwa na umeme: Katika kutekeleza azma yake ya kutimiza lengo la asilimia 30 ya wananchi watakaounganishiwa umeme ifikapo Mwaka 2015, Serikali ilipunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wananchi. Katika punguzo hilo, mathalan gharama ya kuunganishwa umeme wa njia moja (single phase) kwa wateja wadogo mijini na vijijini ilipungua kwa wastani wa kati ya asilimia 30 na 77. Kutokana na juhudi hizo za Serikali, idadi ya Watanzania wanaopata umeme imeongeka kutoka asilimia 11 Mwaka 2005?? hadi kufikia asilimia 24 mwaka 2015. Pia jitihada hizo zimewezesha Watanzania asilimia 36 kufikiwa na miundombinu ya umeme.
 
Net group solutions walipokuja improvement ilikuwa kubwa na hata tukasahau kitu kinaitwa kukatikati kwa umeme iwe mvua iwe jua. Pia wakati Masasi akiwa Meneja ilikuwepo improvement kubwa na huyu mzee alikuwa serious.
Kinachokata umeme Arusha siyo tatizo la miundombinu bali Meneja wa Arusha hayuko serious na hata siku moja hatumii muda kutafuta solution kwani yeye ni business as usual type

Umeme wa Aru

VYOMBO VYA HABARI.
1. HALI YA UZALISHAJI UMEME NCHINI
Hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika licha ya changamoto mbali mbali tunazokabiliana nazo kwa sasa. Kuanzia taerehe 17 Septemba tulipoanza kutumia gesi inayotoka Mtwara tumeweza kuongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi kutoka Megawati 260 zilizokuwepo kabla hadi Megawati 560 ikiwa ni ongezeko la jumla ya Megawati 300 au asilimia 115 ya umeme wa gesi uliokuwa unazalishwa. Hii imechangia sana kuboresha hali ya umeme tofauti na ilivyokuwa hapo kabla. Tunategemea kuongeza umeme wa Megawati 130 zaidi kutokana na vyanzo vya Gesi kati ya sasa na mwishoni mwa mwezi Januari 2016. Hii itafanya jumla ya umeme wote unaotokana na gesi kufikia Megawati 700 sawa na asilimia 70 ya umeme wote kwenye Gridi ya Taifa. Haya ni mapinduzi makubwa kwani kwa miaka mingi vyanzo vya maji ndivyo vimekuwa vikichangia zaidi ya asilimia 70 ya umeme nchini na hivyo kusababisha athari za mara kwa mara kila unapotokea ukame.
Pamoja na hayo yaliyokwishafanyika, Mkandarasi wa mradi wa pili wa Kinyerezi (KII) wa Megawati 240 anatarajia kuanza kazi wakati wo wote kuanzia sasa baada ya kuwa amekwishalipwa sehemu ya fedha za awali za kuanza kazi hiyo.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Maelezo kuhusu Hali ya Umeme kwa baafhi ya Maeneo Mkoa wa Arusha.

Shirika la Umeme linapenda kueleza kile kinachoendelea mkoani Arusha kama ifutavyo; Eneo la Olasiva, Kwa kuanzia tunamalizia, mradi wa Olasiti Meckson school wiki hii. Hivyo wateja wa eneo Hilo watapata umeme mzuri. Pia miradi wa Sanawari Kati na shangalai uko Kwenye hatua za mwisho kufikia tarehe 15.12.2015 itakuwa imekamilika. Mradi wa kuboresha, huduma Olasiva uko 40% hivyo mwisho wa mwezi huu, tunaimani kuukamilisha.

Kumalizika kwa miradi hapo juu ambayo tayari imeanza, ulitatupa nafasi kuanza miradi ya Olasiti Kati, Ngaramtoni, na Engosheratoni. Ni matumaini ya mkoa tatizo la umeme mdogo litakuwa historia ndani ya miezi mitatu ijayo. Asante.
 
Acheni siasa, kwanini msitutangazie muda wote mpaka muone malalamiko huku jf ndio mtolee ufafanuzi:what: nyie kama ni mgao tangazeni na mtoe ratiba ya mgao:what: sio mnakatakata umeme kipuuzi bila taarifa, au mnafanya biashara ya majenereta nini:what:
 
Kumalizika kwa miradi hapo ambayo tayari imeanza, ulitatupa nafasi kuanza miradi ya Olasiti Kati, Ngaramtoni, na Engosheratoni. Ni matumaini ya mkoa tatizo la umeme mdogo litakuwa historia ndani ya miezi mitatu ijayo. Asante.
 
Kwa TANESCO kukaa kimya naamini lwamba huu mgao Arusha ni wa kutengeneza, Sijawahi sikia viongozi wa TANESCO wakizungumzia huu mgao,
kwa staili hii TANZANIA YA VIWANDA LABDA KIZAZI CHA 10 KUTOKA SASA.
 
Back
Top Bottom