Kuna mawili inawezekana Gadner alijisahau pesa yake akaishia kutanua au ana mali zake(nyumba) ya siri ambayo Jide hajui. Imeandikwa''enyi waume ishini na wake zenu kwa akili'' yeye hakuishi kwa akili mpk mwanamke akamzidi akili .
Huu msemo wa "...enyi wanaume, ishini na wake zenu kwa akili" haueleweki kabisaaaaaaaaaaa!
Sasa itakula kwake, ukiwa jeuri kwenye mahusiano inapaswa uwe umejiandaa na matokeo, sasa yeye anahangaika na michepuko halafu hana hata pa kulala.
Gadner naye aache uchizi mimi pia naamini mali ni za Jide , hakuna mwanaume ambaye atanunua magari,kiwanja na ajenge nyumba halafu vyote aandike jina la mke wake, wanaume ni wabnafsi sana.Jide kwahapo namsifu alikuwa mjanja sana.
Gadner atafute hela akaanze maisha aache kulilia mali za mwanamke, yani mali za Jide zigawanywe halafu Gadner akatanue na mwanamke mwingine aha hapana sikubali. Hapa Jide akaze buti hasikubali
Unaambiwa mali zote ni za jide, na zimeandikwa kwa jina la jide, kama kuchuma wote watakuwa walichuma maembe na sio mali, apeleke makende kwa michepuko yake uko
Lakini hapa ilikuwaje Gadner akaruhusu mali zote ziandikwe jina la Jide?? Halafu Gadner si alikuwa anafanya kazi Clouds fm/Times Fm na analipwa Mshahara?? Ina maana hela zote alikuwa anaweka kwenye kapu la Jide?? halafu watu mbona hawajishugulishi kuhoji zilipo mali za Gadner??
Unaambiwa mali zote ni za jide, na zimeandikwa kwa jina la jide, kama kuchuma wote watakuwa walichuma maembe na sio mali, apeleke makende kwa michepuko yake uko
Lakini hapa ilikuwaje Gadner akaruhusu mali zote ziandikwe jina la Jide?? Halafu Gadner si alikuwa anafanya kazi Clouds fm/Times Fm na analipwa Mshahara?? Ina maana hela zote alikuwa anaweka kwenye kapu la Jide?? halafu watu mbona hawajishugulishi kuhoji zilipo mali za Gadner??
Huyo Gardener ana mali gani?angekua nazo unadhani angehangaika hivi?
Nadhani, mie nimecheka kuliko weweuzi huu unachekesha sana
HALI tete !
Gardner anataka mgawo wake, lakini sasa utata ulioibuka ni kwamba, inaonekana kama
mali zote ni za Jide kwa vile zimeandikwa majina yake hivyo jamaa ana wasiwasi kwamba Jide anaweza kusema mahakamani
kuwa alizichuma mali hizo kabla ya ndoa , kilisema chanzo hicho kilicho jirani na familia hiyo .
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, utata huo umemfanya Gardner kuwa bize ili kuhakikisha anaumaliza hususan kwenye
nyumba yao iliyopo Mbezi ambapo wengi wanaamini ilijengwa kwa kutumia fedha ya Jide kabla hawajafunga ndoa .
MALI ZINAZOTAJWA
Mali zinazotajwa kuibua utata ni Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Kinondoni, Dar ambao hivi karibuni Jide aliubadili jina na
kuuita M .O . G Restaurant . Mgahawa huo walipangishwa na mtu.Gari aina ya Range Rover Evoque linalomilikiwa na Judith Wambura Lady Jaydee .
Kuna madai kwamba, Jide na Gardner kabla ya ndoa yao kuparaganyika walikwenda kwa
mmiliki huyo na kusema wameamua kuuacha baada ya mkataba wao kumalizika . Lakini kilichoonekana baadaye, Jide alirudi kwa njia
ya uani na kuanzisha mkataba mpya bila Gardner na kuuita M. O .G .
Mali nyingine mbali na nyumba na mgahawa ni mabasi madogo mawili aina ya Toyota Hiace , moja la Machozi Band na la M .O .G Restaurant . Mabasi hayo yameandikwa Lady Jaydee & Machozi Band .
Hata hivyo , yapo madai kwamba Machozi Band nayo imebadilishwa jina, sasa inaitwa Lady Jaydee
& The Band .
Mali nyingine ni Albamu zote za Jide alizotoa tangu mwaka 2005 wakiwa tayari kwenye ndoa ambapo kwa kawaida mauzo yake ni
endelevu na gari la kutembelea aina ya Range Rover Vogue .
Albamu hizo ni Moto ( 2005) , Shukrani, The Best of Lady Jaydee ( 2006 ) na Nothing But the Truth ( 2014 ) .
Una maana kubwa na pana sana , mimi huwa nautafakari sana ,mwanamke ni kiumbe wa ajabu inahitaji akili, hekima na busara kuishi nae.
Unapoacha mwanamke awe na akili ndio hapo mali zote anaandika jina lake, mwanaume ni kichwa cha nyumba sasa ukiacha mwanamke awe kichwa cha nyumba ndio matokeo yake hayo.
Gardner ni haki yake kisheria as long as mali zilipatikana ndani ya ndoa. Haijalishi kachangia sh. ngapi, support ni mchango tosha. Ndio maana hata mama wa nyumbani hudai mgao wake pindi wakitalakiana. Jide aache kabisa ubinafsi