Mganga toka nigeria - mafuta toka congo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga toka nigeria - mafuta toka congo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Aug 14, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 14, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Miaka michache iliyopita Filamu za kiafrika haswa Nigeria na Ghana zimekuwa zinavuma sana , kuna wakati nasema hizi filamu zimechangia sana kwa baadhi ya jamii kubadilisha vitu haswa mila na desturi zao , katika fulamu hizo mambo ya kishirikina yako sana , mambo ya dini pia yako haswa ukristo matokeo yake tunayaona sasa .

  Wachungaji na viongozi wengine wa dini ni wapenzi wakubwa wa filamu hizi haswa wa makanisa ya kilokole , upenzi huu umeambukizwa mpaka kwa waumini wao pamoja na jamii kwa ujumla , ukienda majumbani mwa waumini hawa ni filamu hizi za kishirikina toka afrika ya magharibi .

  Hata waigizaji wetu wa filamu sasa wamepata soko kuigiza vitu hivyo hivyo vya kishirikina ambavyo inaonyesha watanzania wamekubali ujio huo wa mila na desturi za wengine , sasa hivi mitaani kukutana na waganga wanaojiita ni wenyeji wa naigeria ni kawaida sana .

  Ukipita sehemu kadhaa jijini dar es salaam lazima utakutana na vibao au vitambaa vyenye matangazo ya waganga wa kienyeji toka nchini Nigeria au sehemu zingine za afrika ya magharibi , sijawahi kudhibitisha kama kweli ni waganga toka sehemu hiyo ya afrika ya magharibi au la , lakini hii imenishangaza sana , hatimaye tumeingiliwa hata katika soko la sayansi ya asili .

  Hata wachungaji wengi maarufu hapa nchini kwa namna moja au nyingine wamewahi kusoma au kupata mafunzo Fulani ya kiuchungaji wao toka nchini Nigeria au nchi zingine za afrika ya magharibi haswa wa makanisa ya kilokole .

  Kwa dada zetu ambao ndio watumiaji wa madawa ya nywele na ngozi basi wao hupendi kupata vitu vyao hivyo toka nchini ivory coast au congo na wakati mwingine Nairobi lakini zaidi ni congo au ivory coast , wale wapenzi wa muziki watakwambia wanapenda mambo ya congo , mambo ya kimagharibi , kihindi na mengine mengi toka nchi za watu .

  Juzi juzi hata nilikuwa arusha na rafiki yangu mmoja hivi , wakati anakuja arusha aliambiwa kabisa kwamba anunue maziwa Fulani ambayo huzalishwa Kenya , katika kazi zetu mbali mbali kila alipohitaji basi ilibidi kwenda kumtafutia hayo hayo tokea Kenya .

  Tukaja kwenye suala lingine , rafiki yangu akataka kupiga picha na wamasai kati kati ya mji ule , wale jamaa wakataka pesa kila mmoja ili aweze kupiga nao picha , wakati anakuja alipofika uwanja wa ndege Nairobi alipiga picha bure alifika mpaka katika sehemu kadhaa akapiga picha na watu wa huko .

  Kama umesikiliza nyimbo moja inaitwa Nchi Ya Kitu Kidogo , ingawa imeongelea masuala mengi yanayoikabili nchi hiyo lakini mtunzi wa nyimbo hiyo amefanikiwa pia kusifia vitu vyao mfano kuna sehemu anasema ukitaka Chai Nenda Nakuru , ukitaka Fanta Nenda sehemu Fulani akamtaja mpaka Msanii mmoja maarufu wan chi hiyo .

  Nyimbo hiyo imenikumbusha nyimbo kadhaa ambazo ziliwahi kuimbwa na wanamuziki wetu enzi za Mwalimu , Kuna nyimbo kama TUNAYATANGAZIA MATAIFA YOTE , DR KLERUU , TANZANIA NCHI YANGU , Pamoja na nyingine nyingi ambazo katika vipindi vya kawaida katika radio zetu nyumbani hazipigwi hata kidogo .

  Kuna wakati Fulani Kwenye kona ya kutokea uwanja wa Ndege wa JK nyerere kulikuwa na tangazo la Huduma ya Internet pale toka Kampuni ya Vodacom , kulikuwa na picha inayoonyesha ukurasa wa HI5.COM wakati kuna tovuti nyingi sana nchini sijui kama HI5.COM walilipia tangazo lile Kampuni ye Voda ingeomba radhi watanzania kwa Utovu ule wa Nidhamu , siku hizi pia kuna Tangazo moja la Kampuni ya Zain Dada mmoja anamwambia mwenzake kuhusu facebook.com afungue hiyo kwa kutumia mtandao wake .

  Ukiangalia visa vya hapo juu , inaonyesha kwamba uzalendo na ari ya kuendeleza nchi hii iko chini sana ,Kilichobaki sasa ni mashindano ya kuagiza vitu toka nje pamoja uingizwaji wa mila na desturi za watu wa nje ambazo hazina tija kwetu .
   
 2. kibanzi

  kibanzi Member

  #2
  Aug 14, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo yote uliyo ongea ni sawa , ila kuna haya:

  Kuna wakati Fulani Kwenye kona ya kutokea uwanja wa Ndege wa JK nyerere kulikuwa na tangazo la Huduma ya Internet pale toka Kampuni ya Vodacom , kulikuwa na picha inayoonyesha ukurasa wa HI5.COM wakati kuna tovuti nyingi sana nchini sijui kama HI5.COM walilipia tangazo lile Kampuni ye Voda ingeomba radhi watanzania kwa Utovu ule wa Nidhamu , siku hizi pia kuna Tangazo moja la Kampuni ya Zain Dada mmoja anamwambia mwenzake kuhusu facebook.com afungue hiyo kwa kutumia mtandao wake .

  mimi nafikiri kuwa sio sawa kwani lile tangazo ni lakutumia internet za zile compuni za simu hazina uhisiono na kulipia face book au HI 5 kwani hizo kampuni hazina haja ya kulipa matangazo kwani zenyewe tayari zimeshajitangaza na zina wateja dunia nzima zaidi ya mamilion.:eek:
   
Loading...