Mganga awezi kukupa mke/mume sahihi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga awezi kukupa mke/mume sahihi!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BASIASI, Aug 14, 2011.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,095
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Na Luqman Maloto
  Tupo kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Leo ni chungu cha 13. Jumatatu tutakuwa tunazungumzia habari ya kuugawa mwezi. Namshukuru Mungu kwamba tunaendelea kukutana kwa njia ya maandishi. Mimi naandika, wewe unasoma, hakika Mungu ni mtakatifu kweli kweli.

  Tuanza mada yetu msomaji wangu: Si ajabu hapo ulipo ukawa na mawazo tele. Unajiuliza kwa nini hupati mchumba. Watu wa rika lako uliokua nao, hivi sasa wanajenga familia zao, wewe bado unakomaa na maisha ya usimbe au bachela (neno la kutohoa kwenye Kiingereza.

  Kama mwanamke, taratibu unaanza kuwa mnyonge. Upweke unakusumbua, kwa mbali unashawishika kuwa kuna mkono wa mtu katika tukio lako la kukosa mwanaume ambaye amehitaji kukuoa.
  Kundi hili la wanawake ambao wamekaa muda mrefu bila kuolewa huhisi wana upungufu mkubwa kwenye jamii, hivyo huamua kwenda kwa waganga wa kienyeji kama sehemu ya kutafuta dawa ya tatizo la kukosa waume wa kuwaoa.

  Wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji hupoteza njia. Wanapaswa kuchunguza hulka zao. Sangoma hana ubavu wa kumpa mtu dawa ili akikatiza barabarani wanaume wawe wanamuangalia kwa jicho la kutaka kumuoa.

  Hata kwa mwanaume, japo si sana kutokana na asili ya maumbo yao kuwabeba lakini bado na wao wakati mwingine hujikuta wanazeeka bila kuwa na wake kutokana na hulka zao. Mada hii ina majibu ya kile kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kilikuwa kinakuumiza kichwa kuhusu ndoa.

  Jambo ambalo ni vema kila mtu akalijua ni kuwa ndoa ni mtu mwenyewe. Jinsi ambavyo wewe mwenyewe unajiweka ndivyo unavyoweza kuolewa au kupata mke wa kuoa mapema. Ukiwa macho juu unadhani nani atakubali ujiweke kwake?

  Naishi kwenye jamii kama yako msomaji wangu. Nakutana na watu wa aina mbalimbali. Inawezekana mimi nawajua wengi wanaoteseka lakini sipingi kama wewe utakuwa umeshuhudia idadi kubwa zaidi yangu. Hebu tugawane elimu ndogo niliyojifunza mtaani.
  Kuna pointi ambazo nitazieleza lakini kabla yake lazima nifafanue kuwa inawezekana ukawa unapata wapenzi wengi. Ukifumba macho na kufumbua wapo wamejaa. Hata hivyo, wanabaki kuwa watu wa kujifunzia mapenzi kwako.

  Wanakuacha unaendelea kuzeeka nyumbani. Matokeo yake vijana wanakuona mzee, kwa hiyo kimbilio lako linakuwa ni kujifariji kwa waume za watu. Unaiba mwanaume wa mwanamke mwenzako.
  Kutokana na kukata tamaa ya kuolewa, unakata shauri la kuzaa kabla ya ndoa. Huna wa kuzaa naye, kwa hiyo huyo mume wa mtu ambaye unatoka naye ndiye unabeba mimba yake. Kosa lako linamgharimu mtoto kuwa na baba wa kuiba.

  Ni wa kuiba kwa sababu wenye baba yao halali wapo nyumbani, akitoka wanajua amekwenda kazini na atarudi jioni, mtoto wako yeye anamuona kwa msimu. Wakati mwingine akija unamwambia amwite ‘Anko’, ni kosa kubwa.

  Je, ingekuwa ni wewe, ungefurahi kuambiwa umwite baba yako mzazi Anko? Kama utajisikia vibaya ni kwa nini umfanyie hivyo mwanao? Unayo nafasi ya kumtafutia baba yake halali, tena aliyetokana na ndoa inayokubalika.
  NINI SABABU YA WATU KUCHENGWA NA NDOA?
  Zipo sababu nyingi ambazo nitaziweka kwenye makundi ambayo itakuwa rahisi kuyaelewa. Katika kila kundi, nitaeleza tiba ambayo kama mtu atajiona linamhusu, basi akiitumia inaweza kumsaidia na atapata mwenzi wake wa maisha.

  KUNDI LA KWANZA
  Kuna aina ya watu ambao ni rahisi kuwaita vimbelembele ili kueleweka kwa wepesi zaidi. Ni mwanamke lakini anaamini ana nguvu nyingi kuliko mwanaume. Hajui kushuka chini daima yeye ni mtu wa kupanda juu.
  Ni mwanamke lakini anataka awe na sauti yenye mamlaka na kumkoromea mwenzi wake anavyotaka. Akikaa na marafiki zake, anazungumza namna anavyoweza kukabiliana na wanaume kwa ubavu na kuwamudu. Anadhani sifa kumbe anaharibu sifa yake.
  Itaendelea wiki ijayo.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naenda kufuturu kwanza ntarejea kusoma manake ndefuuu....
   
 3. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Wanawake wanatafuta wanaume wa kufikirika ila kwa uhalisia duniani hakuna mwanaume mkamilifu amtakaye hivyo hupoteza muda mwingi kuchagua na kuacha, kuja kushtuka umri unamtupa mkono
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  BASIASI ndie Pdidy???

  watu wanaenda kwa waganga out of desperation,ila waganga hawawezi kufanya lolote kwa yeyote,kama wanaweza waambie walete umeme tuondokane na mgao lol,mie ningekuwa rais ningewafungia waganga wote kasoro wale wa mitishamba,nahisi ni matapeli wanaojipatia fedha kwa njia ya udanganyifu! hawana tofauti na wezi wengine.....
   
Loading...