Mfurahishe mwenzi wako

Mfurahishe mwenzi wako

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,589
Habari za saa hizi wadau wote hapa

Nafurahi kuwepo tena jamvini kuwaletea mambo mapya yahusuyo MAHUSIANO MEMA
kumekuwepo na vitabia vya ajabu kati yetu wanadamu hususan wale walioko kwenye
mahusiano yawe ya ndoa au ya kiblashata tu yaani wenye wenzi wao ndo maana yake

Leo nitawaambia namna ya kumfurahisha au kutengeneza ndoa mpya na mwenzi uliyenaye

Fuatilia hatua hizi utajifunza mengi yahusuyo kufurahishana na kupendana kwa dhati sio majuju

Kufurahisha mahusiano yako
Endapo ndoa au mahusiano yako yako hatarini na huoni tatizo nini kati yenu ni vyema ukagundua
chimbuko la tatizo lako na kasha kuanza kuleta furaha katika mahusiano hayo,

anza sasa kukubili tatizo na chanzo cha ndoa yako au mahusiano yenu kwenda mrama

Kubali kuwa ndoa yako /mahusiano yako yana hali mbaya na hayapo sawa. Usipoteze muda na nguvu kuhuzunika na kujuta badala yake fikiria furaha na burudiko la moyo ambalo mnalikosa wewe na mwenzi wako kutokana na mifarakano kwenye ndoa yenu. Jambo hili liwe msukumo wa kuhakikisha unafanya jitihada zote ili uweze kuponya ndoa yako au mahusiano yenu.

Bomoa ndoa yako iliyoharibika na uijenge upya

Wakati wana wa Israeli wanajenga ukuta wakati wa Nehemia, walipogundua kuwa wamekosea msingi waliubomoa na kuanza upya. Sababu umegundua kuwa ndoa yako imeharibika, bomoa na anza upya kuujenga msingi na kuisimamisha upya. Simamisha nguzo imara za kuishikilia isianguke tena ambazo ni Kusogea karibu na Mungu kwa maombi, kusoma neno lake na kuhudhuria kanisani; Kila mmoja wenu kuwa tayari kufanya kazi ya kuijenga ndoa yenu pamoja bila kulaumiana au kutegeana; na kuwa na muda wa pamoja kila siku ili kuimarisha uhusiano wenu.

Jadili makosa yenu na kufanya kazi kuyarekebisha

Kaeni chini pamoja na kila mmoja wenu kwa hiyari yake akiri makosa yake yaliyopelekea ndoa yenu /mahusiano yenu kuharibika na kuomba msamaha kwa mwenzake na kutafakari pamoja nini kifanyike ili makosa hayo yasijirudie tena. Jitahidi kuwa ‘positive’ katika majadiliano yenu ili muweze kufikia muafaka ambao utaiboresha na kuijenga upya ndoa yenu. Hakikisha mnafanya kazi ya kuyakabili na kuyarekebisha makosa yenu kwa pamoja ili yasiweze kurudi tena.

Samehe

Amua kumsamehe mwenzi wako yale yote aliyokukosea na umweleze hivyo kuwa umemsamehe kabisa na upo tayari kusahau yote na kuanza upya. Usisamehe kwa kutegemea kitu Fulani, samehe kutoka moyoni.

Timiza mahitaji ya kila mwenzi wako

Zungumza na mwenzi wako ujue ni nini hasa anahitaji toka kwako na hakikisha unayatimiza mahitaji yake kwa kadiri uwezavyo. Kuanzia mahitaji ya kiroho, kihisia, kimwili na kiuchumi. Patikana pale anapokuhitaji, saidiana naye shughuli mbalimbali za nyumbali, nenda naye matembezi (mtoane outing) na pia uwe naye katika wakati anapokuwa na huzuni.

Hayo ni baadhi tu ya yale mengi ambayo unaweza kuyafanya na kutengeneza ndoa au mahusiano mema pale ulipo

Rafiki natumai utaweza kujifunza hapa na kupata kile ambacho kitakusaidia kwenye mahusiano yako na kuleta FURAHA katika mahusiano yenu wewe na mwenzi wako

Nawatakia furaha na fanaka njema marafiki zangu

Wasalaam

Ladyf
 
Ahsante mumy kwa ujumbe mzuri na wa kueleweka.
 
Back
Top Bottom