Mfupa uliomshianda fisi mbwa atauweza?

Mfupa uliomshianda fisi mbwa atauweza?

joshydama

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
4,623
Reaction score
5,052
Heshima zenu wana JF, wakubwa kwa wadogo. Ni matumaini yangu kuwa mko salama wote kabisa na wenye afya njema, na kama kuna mtu ambaye afya yake imeyumba kidogo basi Mola akutangulie ili uweze kukaa vizuri.

Napenda kutumia nafasi hii kushea jambo moja na nyie ndugu zangu wa MMU. Jambo lenyewe ni kwamba Usione mwanaume amemuacha mwanamke wake wa ndoa ambaye ni mwanamke mzuri sana na ana sifa na vigezo vyote vya kuitwa mwanamke mzuri ukamdharau na ukamuona lofa kwa kitendo cha kutengana nae au ukamatamani na kumpenda huyo mwanamke aliyeachika ukiwa na lengo la kuishi nae kama mume na mke hapo utakuwa umepotea kiukweli.

Ni kwamba mwaka jana nilikutana na mwanamke mzuri sana pale posta nikamuelewa sana na nilizidi kuonesha hisia zangu mwisho wa siku akanielewa. Kabla ya kuingia rasmi kwenye mahusiano nilitaka nijue kama ana mtoto au hana. Pia sikuishia hapo bali nilizidi kufanya tafiti mbalimbali kuhusu yeye baada ya kujiridhisha tukawa tumeingia kwenye uhusiano lengo langu likiwa ni kumuoa awe mke wangu. Huyo mwanamke kiukweli ni mzuri na alikuwa na maisha yake mazuri tu.

Kadiri muda ulivyozidi kusogea mbele nikagundua kuwa alishawahi kuolewa na ana watoto wawili na hao watoto 2 wapo nyumbani kwao. Niligundua kuwa ana watoto 2 baada ya kuhamia kwangu tukaanza kuishi pamoja. siku moja nikiwa natafuta nyaraka zangu ndipo nilikutana na picha za watoto wake, vyeti vya kuzaliwa vya hao watoto. Nilipomuuliza na kumbana sana akasema ukweli wake kuwa ana watoto wawili na aliolewa akaachika. Ndoto zote za kumpeleka home kumtambulisha zikayeyuka kwa sababu sipendi na sikupenda nioe mwanamke ambaye tayari ana mtoto.

Ingawa sikutilia manani sana hilo jambo la yeye kuwa na watoto hivyo tukaendelea kuishi pamoja kama kawaida kumbe huyu mwanamama alikuwa anaficha makucha. Huyu mwanamama ni mkorofi, kiburi na mwenye dharau kwa sababu kwanza hapendi ushauri ule wa kumwambia ukweli mtupu na mchungu anapenda umsifie tu hata kama kafanya jambo la hovyo. Endapo ukimwambia ukweli kama ilikuwa ni usiku basi mtagombana na mtapigana mpaka asubuhi. Ni mwanamke lakini huwa anajifanya Mohammed ALi.

siku moja nilirudi toka kazini nikamkuta amejilaza tukasalimiana kama kawaida then nikakaa kama dakika 10 nikisubiri ashuke kitandani anitengee msosi nile lakini hakufanya hivyo. Ikabidi nimuulize vipi mama mbona haunitengei msosi? akajibu amechoka kupika na akasema alijua nitakula hotelini nikiwa narudi home. Nilikwazika sana nikajikuta namwambia una akili za kijinga. Ghafla nilishangaa anaruka toka kitandani na kuniparamia. Kiukweli nilimchapa sana mpaka akazimia. Nikampeleka hospital akawekewa dripu ya maji baadae akawa poa. Pia nikawaelekeza kuwa wampime ugonjwa wa shinikizo la damu na wakafanya hivyo. kwa bahati mbaya ana pressure.

Daktari akanishauri kuwa niwe nahakikisha ana furaha ili asiwe katika danger zone na nisijaribu kumpiga wala kumfanyia chochote kibaya. Nikawa nautekeleza huo ushauri wa daktari lakini sasa huyu mwanamke haelewi wala cha nini na hajihurumii anapenda ugomvi sana.

Kumbuka tangu nimejuana nae na kuhamia kwangu hajui hata nauli ya mwendokasi ni shilingi ngapi kwa sababu kwa huruma zangu na upendo wangu nilimpa gari aina ya IST kikawa kinamsaidia safari za hapa na pale ingawa ana kazi yake lakini hata mafuta huwa namuekea mimi ukimwambia chukua hela yako uweke mafuta anasusa hataki tena gari na maneno kibao kuwa hastahili kwanza kuendesha kigari kama hicho yeye ni mwanamke mzuri sana hivyo hlo gari siyo type yake. Mimi huwa ni mtu kupuuzia sana maneno kama hayo nikapotezea.

Pia huwa hapendi umpe hela chini ya laki moja akiwa anaenda shopping au hata kwa safari zake binafsi. Endapo utampa chini ya hapo atapokea na kuitupa chini na kulaumu kuwa hajazoea maisha ya hivyo na kujilaumu kwanini aliachana na mume wake maana alikuwa akimpa hela nyingi kuliko anazopewa leo. Anasema hajazoea kwenda shopping na hela ndogo. Kwangu mimi huwa naona ni changanoto ya kunisukuma nizidi kusaka mkwanja ila sasa hivi naona natumia nguvu nyingi ili nimfurahishe mtu ambaye hajitambui.

Mbali na hilo anaweza kuwa amekosea yeye lakini hataki kujishusha wala nini na huwa anaondoka hata muda wa siku 3 anaenda kulala kwa marafiki zake ingawa sina ukweli kama huwa anaenda huko na sitaki kujua huwa anaenda wapi maana naweza nikamtoa roho bure.

Sasa juzi amerudi bila gari nikamuuliza mbona hujaja na gari hakutoa majibu yanayojitosheleza. ikabidi nimcheki rakfiki yake, huyo rafiki yake akaniambia hivi nanukuu gari imeuzwa na huyo mwanamke wako alisema kuwa wewe umemwambia aliuze ili umuongezee hela akanunue gari lingine. Kiukweli nilichoka sana.

Ingawa nilimvumilia sana kwa mambo yake mengi ya ajabu sana ambayo mengine siwezi elezea hapa lakini hili limesababisha na limenivunjavunja moyo wangu na nimeamua kuachana nae.

Je ndugu zanguni wa MMU mliokwisha oa au ambao mna wapenzi wenu na mnaishi pamoja ndivyo hali ilivyo katika ndoa na uhusiano wenu au inatokea kwangu tu?

Tafadhali shea mawazo yako kama ulishawahi kuwa na uhusiano wa namna hii na mwanamke aliyeachika huenda nikaendelea kuvumilia.




 
We ni mbwa ... u sijaelewa mada

eti mimi nachekesha [emoji23][emoji23]
 
Duhh wee ni mvumilivu sana na hongera,pole kwa unayopitia, binafsi niliwahi kuwa kwenye mahusiano ya aina yako kwa mambo kama hayo huwa sijiulizi mara mbili huwa ni mwisho wa mahusiano,hakika nakwambia kwa aina hiyo ya mwanamke usipomuacha wakati huu basi jiandae kisaikolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni ishu ya uvumilivu basi nakutunuku PhD ya heshima

Sent using Jamii Forums mobile app
Na akiendelea nae basi atapewa u-professor kabisa. In short, huyo umemvumilia sana Mkuu, tena hapo haujamuoa wala haujazaa nae anakuwa hivyo, mshukuru Mungu kwa maana hayo yametokea mapema kabla ya ndoa, achana nae atakusumbua sana huko mbeleni ukiwa nae.
 
kwa uwezo wa bwana atauweza (cjasoma mada)
 
Hapa kuna mambo mawili au matatu ambayo nimeyahisi kutoka kwenye story yako na mambo yenyewe ni haya;
1.Huenda ni story ya kweli,na kama yote uliyoyasimulia ni ya kweli basi wewe ndyo mwenye makosa na siyo huyo mwanamke kwa kuwa hata Biblia inasema "ewe mkristo uwe na kiasi katika mambo yako yote uyafanyayo"
Naona hauna kiasi
2.Umeamua kutafuta mke hapa Jamii forum kwa njia zisizo za moja kwa moja kwa kuwa unajua kwa maelezo uliyoyatoa yanaonyesha kuwa wewe ni mtu mwenye maisha mazuri na wanawake wanahitaji watu wenye maisha mazuri au fedha kama kinga kwao so,unajua kuwa utawapata tu...yote kwa yote nakupongeza kwa uvumilivu huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kuna mambo mawili au matatu ambayo nimeyahisi kutoka kwenye story yako na mambo yenyewe ni haya;
1.Huenda ni story ya kweli,na kama yote uliyoyasimulia ni ya kweli basi wewe ndyo mwenye makosa na siyo huyo mwanamke kwa kuwa hata Biblia inasema "ewe mkristo uwe na kiasi katika mambo yako yote uyafanyayo"
Naona hauna kiasi
2.Umeamua kutafuta mke hapa Jamii forum kwa njia zisizo za moja kwa moja kwa kuwa unajua kwa maelezo uliyoyatoa yanaonyesha kuwa wewe ni mtu mwenye maisha mazuri na wanawake wanahitaji watu wenye maisha mazuri au fedha kama kinga kwao so,unajua kuwa utawapata tu...yote kwa yote nakupongeza kwa uvumilivu huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu monde arabe, siwezi tafuta mwanamke hapa hata siku moja kwa sababu I'm too matured to find a woman in JF.
 
Mwanamke atakuheshimu kama hana Mchepuko! Ukiona heshima imepungua jua kuna anayempa jeuri. Nakumbuka zamani Rafiki yangu alikuwa na Mchepuko ambaye ni mke wa mtu, kila akitaka walale wote hadi asubuhi, mwanamke alikuwa akilianzisha na Mume wake anahama kwao na kurudi kwa mumewe asubuhi na mapema amechooooooka ile mbaya sababu ya libeneke la usiku nadhani hata wako ni mtindo wa chungu hakiinjiki kwa jiwe moja. Tafakari na chukua hatua
 
Hapa kuna mambo mawili au matatu ambayo nimeyahisi kutoka kwenye story yako na mambo yenyewe ni haya;
1.Huenda ni story ya kweli,na kama yote uliyoyasimulia ni ya kweli basi wewe ndyo mwenye makosa na siyo huyo mwanamke kwa kuwa hata Biblia inasema "ewe mkristo uwe na kiasi katika mambo yako yote uyafanyayo"
Naona hauna kiasi
2.Umeamua kutafuta mke hapa Jamii forum kwa njia zisizo za moja kwa moja kwa kuwa unajua kwa maelezo uliyoyatoa yanaonyesha kuwa wewe ni mtu mwenye maisha mazuri na wanawake wanahitaji watu wenye maisha mazuri au fedha kama kinga kwao so,unajua kuwa utawapata tu...yote kwa yote nakupongeza kwa uvumilivu huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
unafikiria nje ya box sana mkuu.
 
Back
Top Bottom