Mfungwa ni Binadamu na Haki si hisani! Conjugal Visit sio Starehe, ni Haki halali na stahiki ya Mfungwa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Habari za masiku.

Leo naendelea na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Leo nawaelimisha kidogo tuu kuhusu wafungwa.



Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, ambapo mtuhumiwa aliyeko gerezani, anahesabika "not guilt, untill proven" hivyo wafungwa wote wanaotuhumiwa, bado hawana hatia hadi wathibitishwe na mahakama na kuhukumiwa, hivyo wakiwa watuhumiwa tuu ni binadamu wenzetu, kama binadamu nao pia wana haki zao, na miongoni mwa haki hizo ni haki ya kutembelewa na mwenza na kupata faragha, ambayo inaitwa " Conjugal Visit".

Hii conjugal visit, sio starehe, sio favours, ni haki, ni stahiki, na inafanyika kwa mujibu wa sheria.

Msingi wa sheria zetu zote ni katiba, hivyo conjugal visit iko kwa mujibu wa katiba!.

Haiwezekani akajitokeza mtu kuzuia kwa kauli tuu, jambo ambalo limeruhusiwa na katiba na lipo kisheria.

Kwa vile sheria zetu nyingi, tumezirithi kutoka kwa wakoloni Waingereza, inawezekana lengo la conjugal visit ni starehe tuu na sii miongoni mwa haki za msingi za binaadamu na haki za wanandoa!.

Tukiona sisi hatuzihitaji, the right thing to do, sio kutoa kauli kuzifuta, bali ni kupeleka bungeni muswada wa kukifuta kipengele kinachoruhusu conjugal visits kwa watuhumiwa walioko magerezani. Kwa hapa naomba tutofautishe mtuhumiwa na mfungwa, na kutofautisha jela na mahabusu. Kwa nchi za wenzetu wanaoheshimu haki za binaadamu, wafungwa wanatenganishwa na watuhumiwa, wafungwa ni inmates na ndio wanaokaa jela zao, na watuhumiwa ni remandees wanakuwa na magereza yao ambako hawachanganywi na wafungwa na wana haki zote za kutembelewa hadi haki ya conjugal visits. Haku kwetu, wafungwa wanachanganywa na mahabusu na wanakuwa treated almost the same!.

Ila kiukweli tunakokwenda...
Sijui!.

Kama tumefika mahali haki zinageuzwa kuwa favours kwa kauli tuu, na watu wakakubali, na wakanyamaza, then inawezekana kabisa hata haki ya kuishi pia ikaja kuwa treated as its just a favour!.

Nitafanya mpango wa kuendesha vipindi vya uelimishaji umma kuhusu haki za msingi za binaadamu kupitia vituo mbalimbali vya TV ikiwemo TBC yetu sio tuu ili Watanzania tuelimike na kuzijua haki zetu, bali pia vipindi hivi vitawasaidia sana viongozi wetu kuelewa, umuhimu wa haki za binaadamu na kujua kuwa hakuna aliye juu ya katiba, haiwezekani kiongozi akaibuka na kuzuiahaki zilizotolewa kikatiba na kisheria, na tukawa tunamwangalia tuu au akaachwa hivi hivi bila kuambiwa.

Kwa sasa naomba ninyamaze nisije... maana wale wanaoibuliwa kwenye viroba ndio wenye bahati viroba vyao viliibuka, wasio na bahati, vinazama jumla, na kwa vile huwezi jua bahati yako ikoje, ni busara zaidi kujinyamazia!.

Paskali
 
Amesema inabidi wafungwa wafanye kazi usiku na mchana, amelaani askari magereza kulala nje na familia zao, kwenye nyumba mbovu mbovu huku wafungwa wakilala ndani kwa starehe.

Amesikitika magereza kuomba bajeti ya kujengea nyumba zao, wakati wafungwa wapo wa kufyatulisha tofali....

Amesema mfungwa anafungwa ili ahenyeke.

Ameongeza kuwa kuna baadhi ya wafungwa wanapelekewa wake zao ndani ya jela ili kumaliza hamu zao wakati wao ni wafungwa na sheria hairuhusu.....amehoji pia wafungwa kuingia na simu ndani ya gereza huku lawama zote likitupiwa jeshi la magereza.

Amesisitiza wafungwa inabidi "wahanyeke" na kazi ya askari magereza ni "kuhenyesha" wafungwa....

Amempongeza kamishina mpya kwa uteuzi ila amempa pole kwa kazi anayoenda kuifanya....

Naona hili onyo kwake kuwa anaweza kutenguliwa muda wowote, akifanya tofauti.
 
..nimesikia Magereza wakielekezwa kwamba wafungwa wafanye KAZI.

..sasa ili ueleweke ungejenga hoja kwamba conjugal visits ni "KAZI."

..mwingine nikamsikia anadai eti wafungwa hawazalishi, wanakaa tu magerezani na "kula bata" na "kuku kwa mrija."

..nadhani wako wanaoamini kwamba wafungwa wanapaswa kunyooshwa kwa kazi ngumu na mateso.
 
Huyu nae asipotiii maelekezo tunatoa Press release ya kustaafu kwake Hata Kama ana Miaka 53 tunateua Mwingine then Huyu tuna sema kastaafu Kwa kufikisha Miaka 60 Nani atabisha!

Asienyooka Kwa Nabii Huyu hanyooki mpaka anakufa


Ukifungwa Hata Miezi mitatu ya Kiangazi lazima ukalime Gereza Sio hostel

Senk yuu vere macheeeee
 
Kiukweli tunakokwenda...
Sijui!.

Kama tumefika mahali haki zinageuzwa favours na watu wakakubali, wakanyamaza...

Naomba ninyamaze nisije...

Paskali
Pascal Mayalla,
Umesahau kuna mtawala wetu alituambia SEGEREA sio Sheraton?
Elimu ya haki za binadamu kwa nchi yetu inatakiwa aanze kupewa mkuu, maana haielewi kabisa, ndipo ishuke chini hadi kwenye ngazi ya familia
 
Back
Top Bottom