Kuna kesi kama hii ilitokea huko Indonesia binti wa ufilipino aliwekewa madawa ya kulevya na dada mmoja kisa alimtafutia kazi za ndani Indonesia alivyokamatwa akahukumiwa kunyongwa.Bahati yake siku ya kunyongwa masaa 24 kabla aliyemuwekea madawa hayo akajitokeza kwao Ufilipino akasema ni yeye kamuwekea raisi wa ufilipino akapiga simu kwa raisi wa Indonesia Joko Widodo hukumu ikasimamishwa kwa muda uchunguzi uendelee.Wale wenzake waliuwawa kwa firing squad usiku huo kina Myran na wengine.
Huyu dada yuko hadi leo hai fungueni google Mary Janet Veloso someni kisa hicho.
Msimhukumu huyu mdada huwezi jua naye kafanyiwa hivyo kwanza nashangaa kufungwa miaka 18 Indonesia adhabu yao ni kifo kwa kupigwa risasi watu nane na bunduki wanakulenga kwenye moyo.
Nahisi kuna kitu serikali ya huko wamegundua hakiko sawa ndio maana hawajamhukumu kifo