Mfumuko wa bei wapungua, wafikia asilimia 5.1

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
mfuko+pic.jpg

Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius Ruyobya amesema kupungua kwa mfumuko wa bei Oktoba, kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula.

Dar es Salaam. Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa Oktoba, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa Septemba, 2017.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba, 2017 imepungua ikilinganishwa na Septemba, 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius Ruyobya amesema kupungua kwa mfumuko wa bei Oktoba, kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula.

“ Kupungua kwa mfumuko wa bei Oktoba kumechangiwa na kushuka kwa gharama za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Oktoba, zikilinganishwa na bei za Oktoba, mwaka jana ‘’,amesema Ruyobya.

Ametaja baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kuwa ni pamoja na unga wa mtama umepungua kwa asilimia 2.6, samaki kwa asilimia 7.1, matunda kwa asilimia 2.7, mbogamboga kwa asilimia 7.4,maharage kwa asilimia 2.9, viazi kwa asilimia 14.4 na karanga kwa asilimia 7.8.

Mfumuko wa Bei ambao hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mwananchi
 
Kwa wanaojua uchumi, kupungua sana kwa mfumuko wa bei si kitu kizuri mara zote.

Mfumuko wa bei unatakiwa uwe katika wastani, usizidi sana, usipungue sana.

In a rather counter intuitive way, kupungua sana kwa mfumuko wa bei kunaweza kusababisha muanguko wa uchumi.
 
..siku hizi hata bei ya penzi imeshuka....short time unapata kwa bei ya uchee sana hadi masaki.....achilia mbali bei ya chakula...hela hamna mifukoni....
 
View attachment 626776

Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius Ruyobya amesema kupungua kwa mfumuko wa bei Oktoba, kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula.

Dar es Salaam. Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa Oktoba, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa Septemba, 2017.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba, 2017 imepungua ikilinganishwa na Septemba, 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius Ruyobya amesema kupungua kwa mfumuko wa bei Oktoba, kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula.

“ Kupungua kwa mfumuko wa bei Oktoba kumechangiwa na kushuka kwa gharama za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Oktoba, zikilinganishwa na bei za Oktoba, mwaka jana ‘’,amesema Ruyobya.

Ametaja baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kuwa ni pamoja na unga wa mtama umepungua kwa asilimia 2.6, samaki kwa asilimia 7.1, matunda kwa asilimia 2.7, mbogamboga kwa asilimia 7.4,maharage kwa asilimia 2.9, viazi kwa asilimia 14.4 na karanga kwa asilimia 7.8.

Mfumuko wa Bei ambao hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mwananchi
Mbona unrudia sana kitu kilekile
 
Kwa wanaojua uchumi, kupungua sana kwa mfumuko wa bei si kitu kizuri mara zote.

Mfumuko wa bei unatakiwa uwe katika wastani, usizidi sana, usipungue sana.

In a rather counter intuitive way, kupungua sana kwa mfumuko wa bei kunaweza kusababisha muanguko wa uchumi.
Unatakiwa uwe kwa wastani gani?
 
huku deni la taifa likiongezeka
 
Kwenye makaratasi sawa ila kiuhalisia tunajua tunaohemea kwa kibaba
 
Unatakiwa uwe kwa wastani gani?
Wastani ambao hautaondoa incentive ya production.

Disinflation (slowing down of inflation, but still with positive infalation) kabla haijafika kwenye deflation (negative inflation,inflation going in the negative direction past 0) maranyingi haina ubaya, hasa kama inflation ilikuwa kubwa, kitu ambacho nafikiri kilikuwapo Tanzania.

Lakini inflation ikishuka kwa kasi sana, kuna hatari ya kuingia katikadeflation, kitu ambacho si kizuri kiuchumi.

Ukifika kwenye deflation (negative inflation) tatizo linakuwa kubwa zaidi.Japan ilipata tatizo la negative inflation/ deflation kwa miaka mingi sana limeharibu ukuaji wa uchumi wao.

Uchumi una mambo fulani ambayo ukiyaangalia kwa juu juu unaweza kuonamazuri, kumbe mabaya.

Kwamfano, kuchapisha fedha kunaweza kuonekana kama kitu kizuri, kutaongezea watu utajiri, lakini kiukweli kunapunguza thamani ya fedha.

Vivyo hivyo, kushuka sana kwa bei ghafla kunaweza kuonekana kunaleta nafuu, lakini kunaweza kuharibu uchumi (hasa kukifikia deflation) kwa sababu kutaondoa incentive ya production.

Deflation - Wikipedia
 
Kwa wanaojua uchumi, kupungua sana kwa mfumuko wa bei si kitu kizuri mara zote.

Mfumuko wa bei unatakiwa uwe katika wastani, usizidi sana, usipungue sana.

In a rather counter intuitive way, kupungua sana kwa mfumuko wa bei kunaweza kusababisha muanguko wa uchumi.
huo ni sana au kidogo?
0.2
 
huo ni sana au kidogo?
0.2
Hapo perfect,ukianza kushuka kutoka 0 kwenda negative tu ni habari mbaya kwa uchumi.

Na hata hapo 0.2 napo panaweza kuwa katika margin of error, kwa hiyo ni bora iwe 0.2 katika margin of error ya plus/minus 0.0002%, ikiwa 0.2 katika margin of error ya plus/minus 0.4 hapo napo ni tatizo.
 
Wastani ambao hautaondoa incentive ya production.

Disinflation (slowing down of inflation, but still with positive infalation) kabla haijafika kwenye deflation (negative inflation,inflation going in the negative direction past 0) maranyingi haina ubaya, hasa kama inflation ilikuwa kubwa, kitu ambacho nafikiri kilikuwapo Tanzania.

Lakini inflation ikishuka kwa kasi sana, kuna hatari ya kuingia katikadeflation, kitu ambacho si kizuri kiuchumi.

Ukifika kwenye deflation (negative inflation) tatizo linakuwa kubwa zaidi.Japan ilipata tatizo la negative inflation/ deflation kwa miaka mingi sana limeharibu ukuaji wa uchumi wao.

Uchumi una mambo fulani ambayo ukiyaangalia kwa juu juu unaweza kuonamazuri, kumbe mabaya.

Kwamfano, kuchapisha fedha kunaweza kuonekana kama kitu kizuri, kutaongezea watu utajiri, lakini kiukweli kunapunguza thamani ya fedha.

Vivyo hivyo, kushuka sana kwa bei ghafla kunaweza kuonekana kunaleta nafuu, lakini kunaweza kuharibu uchumi (hasa kukifikia deflation) kwa sababu kutaondoa incentive ya production.

Deflation - Wikipedia
USA inflation rate by semptember 2017 is 2%
 
That number must be interpreted in a relative way, as in, what was it last month, in the last six months, last year, what is the size of the economy, is the economy a mature one or a developing one?

So you can't just read much into a percent number for inflation, just like you can't read the same in a percent number for economic growth.

A large economy growing at 2% may be doing better than a small economy growing at 7%.

Context is paramount.
 
Hapo perfect,ukianza kushuka kutoka 0 kwenda negative tu ni habari mbaya kwa uchumi.

Na hata hapo 0.2 napo panaweza kuwa katika margin of error, kwa hiyo ni bora iwe 0.2 katika margin of error ya plus/minus 0.0002%, ikiwa 0.2 katika margin of error ya plus/minus 0.4 hapo napo ni tatizo.
inakadiliwa kuwa kwa miezi kumi na mbili ijayo itashuka kutoka hapo hadi 4.3 robo ya tatu ya mwaka 2018
lakini hadi mwaka 2020 itafika 6.6.
hiyo ni kwa mujibu wa forecast za tradingeconomics

nini maana yake?
kwa mujibu wa ukokotozi wako.
 
That number must be interpreted in a relative way, as in, what was it last month, in the last six months, last year, what is the size of the economy, is the economy a mature one or a developing one?

So you can't just read much into a percent number for inflation, just like you can't read the same in a percent number for economic growth.

A large economy growing at 2% may be doing better than a small economy growing at 7%.

Context is paramount.
In last 12 months the rate was 2% ...

Je kwa Tanzania in last 12 months ilikuwaje?

Context!!
 
Kichwa cha thread kina mislead.

Kuna tofauti kati ya "mfumuko wa bei wapungua kwa asilimia 5.1" na "mfumuko wa bei wapungua kufikia asilimia 5.1"

Wapungua kwa asilimia 5.1 ni kutoka asilimia 10.2 mpaka 5.1.

Wapungua kufikia asilimia 5.1 inaweza kuwa kutoka asilimia 5.3 kwenda 5.1.

Ndiyo maana nilivyosomaheading nikashangaa kwa nini namba kubwa hivyo?

Kumbe heading misleading.

Mfumuko wa bei ukipungua kwa asilimia 5.1 ni hatari kwa uchumi.

Ukipungua kutoka asilimia 5.3 mpaka 5.1 ni kitu cha kawaida.
 
Usiseme cha kawaida sema ni kizuri
 
Back
Top Bottom