Mfumuko wa Bei ulifikia 4.2% Mwezi Desemba 2021

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,853
Reaction score
14,082
Mfumuko wa bei nchini ulifikia 4.2% mwaka jana mwezi wa 12 huku ukipanda kwa toka 4.1% mwaka jana mwezi wa kumi na moja.

Kiwango hiki hakijawahi kufikiwa ndani ya miaka 5.

====

Tanzania Business Insight Tanzania ended 2021 with an annualized inflation rate of 4.2% in December, up from
4.1% in Nov., National Bureau of Statistics (NBS), said today.

This is the highest inflation rate in five years.

But the inflation rate is still below the government's medium-term target of 5%

Warning
Rising Prices

=====

Mfumuko wa bei wazidi kupaa Tanzania

Umepanda hadi kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Desembe 2021 kutoka asilimia 4.1 iliyorekodiwa Novemba 2021.
Hiyo ni baada ya kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula na zisizo za vyakula.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma Tanzania imepanda hadi kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Desembe 2021 kutoka asilimia 4.1 iliyorekodiwa Novemba 2021, ikichagizwa zaidi na kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula na zisizo za vyakula.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishi Desemba 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka ulioishia mwezi Novemba 2021.

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2021 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2021.

“Kwa upande mwingine, mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Desemba 2021 umepungua hadi asilimia 3.9 kutoka asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2021.” inasomeka sehemu ya ripoti ya mfumuko wa bei ya NBS iliyotolewa leo (January 10, 2022).

Zinazohusiana:

NBS imesema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupanda kwa kasi ya bei kwa mwezi Desemba ni pamoja na mchele kwa asilimia 3.7, mahindi (asilimia 5.2), unga wa ngano (asilimia 3.4), unga wa mahindi kwa (asilimia 3.3) na nyama ya ng'ombe kwa asilimia 2.3.

Pia nyama ya mbuzi imepanda kwa asilimia 1.6, samaki (asilimia 5.3), matunda (asilimia 3.7), mbogamboga (asilimia 2.3) na viazi kwa asilimia 3.2.

Bidhaa nyingine zisizo za vyakula ambazo kasi ya mfumuko wa bei imepanda ni vifaa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za makazi kwa asilimia 5.0, gesi (asilimia 2.3), mafuta ya taa (asilimia 1.7), dizeli (asilimia 6.7) na petroli kwa asilimia 3.0.
6cbaa6ec5db6ce5db609399598f2eaee4681ed06.png

Bidhaa za vyakula hutumika zaidi katika kaya za Tanzania kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya kila siku na pia ni chanzo cha kipato kwa familia zinazojishughulisha na kilimo cha mazao na uzalishaji viwandani.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa mfumuko wa bei kupanda baada ya kuduma kwa miezi miwili katika robo ya nne ya mwaka 2021.

Kasi ya mfumuko wa bei wa Taifa katika mwaka ulioshia Novemba 2021 ilikuwa asilimia 4.1 kutoka asilimia 4 iliyorekodiwa Oktoba 2021 baada ya kung’ang’ania katika kiwango kimoja kwa miezi miwili mfululizo.

Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba 2021 ilikuwa asilimia 4 sawa kabisa na ilivyokuwa Septemba mwaka huu jambo lililoonyesha mwenendo imara wa mabadiliko ya bei katika kipindi hicho.

Chanzo: Nukta
 
Hawa wanafiki unaweza kuwaamini! Hawasimamii taaluma ni full propaganda! Vitu vimeoanda bei kila sehemu! Wapuuzi sana hawa!
 
Yaani sabuni ilikuwa 350 leo 600 Hangaya naye anacheka anasema bado ipo normal hiyo rate ya inflation.
Wananchi wa kawaida hawajui hiyo rate, itakuja imugharimu.
 
Mfumuko wa bei nchini ulifikia 4.2% mwaka jana mwezi wa 12 huku ukipanda kwa toka 4.1% mwaka jana mwezi wa kumi na moja.

Kiwango hiki hakijawahi kufikiwa ndani ya miaka 5.

====

Tanzania Business Insight Tanzania ended 2021 with an annualized inflation rate of 4.2% in December, up from
4.1% in Nov., National Bureau of Statistics (NBS), said today.

This is the highest inflation rate in five years.

But the inflation rate is still below the government's medium-term target of 5%

Warning
Rising Prices

=====

Mfumuko wa bei wazidi kupaa Tanzania
Umepanda hadi kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Desembe 2021 kutoka asilimia 4.1 iliyorekodiwa Novemba 2021.
Hiyo ni baada ya kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula na zisizo za vyakula.
Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma Tanzania imepanda hadi kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Desembe 2021 kutoka asilimia 4.1 iliyorekodiwa Novemba 2021, ikichagizwa zaidi na kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula na zisizo za vyakula.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishi Desemba 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka ulioishia mwezi Novemba 2021.

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2021 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2021.

“Kwa upande mwingine, mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Desemba 2021 umepungua hadi asilimia 3.9 kutoka asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2021.” inasomeka sehemu ya ripoti ya mfumuko wa bei ya NBS iliyotolewa leo (January 10, 2022).

Zinazohusiana:

NBS imesema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupanda kwa kasi ya bei kwa mwezi Desemba ni pamoja na mchele kwa asilimia 3.7, mahindi (asilimia 5.2), unga wa ngano (asilimia 3.4), unga wa mahindi kwa (asilimia 3.3) na nyama ya ng'ombe kwa asilimia 2.3.

Pia nyama ya mbuzi imepanda kwa asilimia 1.6, samaki (asilimia 5.3), matunda (asilimia 3.7), mbogamboga (asilimia 2.3) na viazi kwa asilimia 3.2.

Bidhaa nyingine zisizo za vyakula ambazo kasi ya mfumuko wa bei imepanda ni vifaa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za makazi kwa asilimia 5.0, gesi (asilimia 2.3), mafuta ya taa (asilimia 1.7), dizeli (asilimia 6.7) na petroli kwa asilimia 3.0.
View attachment 2076663
Bidhaa za vyakula hutumika zaidi katika kaya za Tanzania kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya kila siku na pia ni chanzo cha kipato kwa familia zinazojishughulisha na kilimo cha mazao na uzalishaji viwandani.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa mfumuko wa bei kupanda baada ya kuduma kwa miezi miwili katika robo ya nne ya mwaka 2021.

Kasi ya mfumuko wa bei wa Taifa katika mwaka ulioshia Novemba 2021 ilikuwa asilimia 4.1 kutoka asilimia 4 iliyorekodiwa Oktoba 2021 baada ya kung’ang’ania katika kiwango kimoja kwa miezi miwili mfululizo.

Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba 2021 ilikuwa asilimia 4 sawa kabisa na ilivyokuwa Septemba mwaka huu jambo lililoonyesha mwenendo imara wa mabadiliko ya bei katika kipindi hicho.

Chanzo: Nukta
Kuna wakati NBS wawe realistic kwa consumable items ambazo wananchi wanatumia mara kwa mara.

mathalani, kama mtu alizoea kununua mche wa sabuni ya kufualia kwa sh 2,500 na akakuta umepanda kuwa 3,000; (20%)
au sukari toka 2700 mpaka 3000-3200 (zaidi ya 11%)
Mifuko wa cement toka 16500-22,000; (zaidi ya 30%)
mafuta ya kula toka sh 25,000 kwa lita 5 mpaka 32,000 (28% au zaidi
kipande cha sabuni ya kufulia kinachouzwa sh 500 kikiuzwa kwa sh 600 (20%)

Njoo kwenye mafuta ya petroli, pembejeo la kilimo.

Kuna wakati watu wanatoa takwimu as if wanaishi dunia tofauti na hii ya basic everyday consumables
 
Mfumuko wa bei nchini ulifikia 4.2% mwaka jana mwezi wa 12 huku ukipanda kwa toka 4.1% mwaka jana mwezi wa kumi na moja.

Kiwango hiki hakijawahi kufikiwa ndani ya miaka 5.

====

Tanzania Business Insight Tanzania ended 2021 with an annualized inflation rate of 4.2% in December, up from
4.1% in Nov., National Bureau of Statistics (NBS), said today.

This is the highest inflation rate in five years.

But the inflation rate is still below the government's medium-term target of 5%

Warning
Rising Prices

=====

Mfumuko wa bei wazidi kupaa Tanzania
Umepanda hadi kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Desembe 2021 kutoka asilimia 4.1 iliyorekodiwa Novemba 2021.
Hiyo ni baada ya kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula na zisizo za vyakula.
Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma Tanzania imepanda hadi kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Desembe 2021 kutoka asilimia 4.1 iliyorekodiwa Novemba 2021, ikichagizwa zaidi na kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula na zisizo za vyakula.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishi Desemba 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka ulioishia mwezi Novemba 2021.

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2021 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2021.

“Kwa upande mwingine, mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Desemba 2021 umepungua hadi asilimia 3.9 kutoka asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2021.” inasomeka sehemu ya ripoti ya mfumuko wa bei ya NBS iliyotolewa leo (January 10, 2022).

Zinazohusiana:

NBS imesema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupanda kwa kasi ya bei kwa mwezi Desemba ni pamoja na mchele kwa asilimia 3.7, mahindi (asilimia 5.2), unga wa ngano (asilimia 3.4), unga wa mahindi kwa (asilimia 3.3) na nyama ya ng'ombe kwa asilimia 2.3.

Pia nyama ya mbuzi imepanda kwa asilimia 1.6, samaki (asilimia 5.3), matunda (asilimia 3.7), mbogamboga (asilimia 2.3) na viazi kwa asilimia 3.2.

Bidhaa nyingine zisizo za vyakula ambazo kasi ya mfumuko wa bei imepanda ni vifaa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za makazi kwa asilimia 5.0, gesi (asilimia 2.3), mafuta ya taa (asilimia 1.7), dizeli (asilimia 6.7) na petroli kwa asilimia 3.0.
View attachment 2076663
Bidhaa za vyakula hutumika zaidi katika kaya za Tanzania kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya kila siku na pia ni chanzo cha kipato kwa familia zinazojishughulisha na kilimo cha mazao na uzalishaji viwandani.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa mfumuko wa bei kupanda baada ya kuduma kwa miezi miwili katika robo ya nne ya mwaka 2021.

Kasi ya mfumuko wa bei wa Taifa katika mwaka ulioshia Novemba 2021 ilikuwa asilimia 4.1 kutoka asilimia 4 iliyorekodiwa Oktoba 2021 baada ya kung’ang’ania katika kiwango kimoja kwa miezi miwili mfululizo.

Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba 2021 ilikuwa asilimia 4 sawa kabisa na ilivyokuwa Septemba mwaka huu jambo lililoonyesha mwenendo imara wa mabadiliko ya bei katika kipindi hicho.

Chanzo: Nukta
ccm imeshindwa kuongoza nchi
 
Back
Top Bottom