Mfumo wa utawala wa CCM Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa utawala wa CCM Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 29, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  -Kuhakikisha wanapora mali za Watanzania walizozalisha na kuzifanya za familia.
  -Kuhakikisha wanatoa elimu mbovu isiyomsaidia mtoto wa Kitanzania kuihoji Serekali.
  -Kuhakikisha inabariki rushwa rohoni lakini mdomoni wanapiga vita na kukemea.
  -Kuhakikisha inawaua waandishi wote wenye kutaka kuvuruga utawala wao wa kifisadi.
  -Kuhakikisha Demokrasia Tanzania haipati nafasi kabisa.
  -Kuhakikisha rasilimali za Tanzania zinanufaisha watoto wao tu.
  -Kuhakikisha wanawagawa Watanzania kwa imani za kidini waendelee kutawala.
  -Kuhakikisha wanawagawa Watanzania kwa imani za Kikabila waendelee kutawala.
  -Kuhakikisha wanawagawa Watanzania Kikanda waendelee kutawala.
  -Kuhakikisha wanakuwa na mfumo wa fedha chafu ziwasaidie kwenye chaguzi.
  -Kuhakikisha kila muwekezaji anayewekeza Tanzania anaigia kwenye mfumo wao.
  -Kuhakikisha Rais wa Tanzania anapatikana kwenye mfumo wao.
  -Kuhakikisha kila Wizara inakuwa na kijana wao anayetokana na mtandao wao.
  -Kuhakikisha Tanzania biashara zote kubwa ni mali yao.
  -Kuhakikisha wanaua viwanda vyote kuwanyima Watanzania ajira.
  -Kuhakikisha biashara zote za uagizaji bidhaa nje wanafanya wao.
  -Kuhakikisha Watanzania wanazidi kuwa wajinga ndio maana wakaua elimu ya watu wazima.
  -Kuhakikisha elimu ya uraia haitolewi Tanzania ili wasijue Mtandao wa utawala wa CCM

  ONYO KWA WATANZANIA.
  -CCM inatumia Udini ili kubakisha mtandao wa rushwa unabaki madarakani mwaka 2015.
  -CCM imewaingiza watoto wao kwenye nafasi muhimu za chama kulinda mtandao wao.
  -CCM inawatumia wawekezaji wakubwa kupata fedha za kuimarisha mtandao wao.
  -CCM inawanyima watu kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015
  -CCM inawanyima Watanzania elimu ya uraia ili kuimarisha mtandao wao.
  -CCM inawaua waandishi wa habari wanaojaribu kuwaelemisha Watanzania.
  -CCM inawatumia Polisi kuwatia hofu Watanzania kupata haki zao za msingi.
  -CCM imeuza ardhi za Watanzania kwa wawekezaji ili kuwadhoofisha kiuchumi.
  -CCM inatumia fedha chafu kuwapa rushwa Watanzania ili wabaki madarakani.
  -CCM inafanya biashara ya mafuta, yakipungua bei yanafichwa.

  TUFANYE NINI WATANZANIA
  -Lazima tuwe na mshikamano bila kujali Dini zetu, kabila zetu, jinsia zetu na rangi zetu kuhakikisha haturuhusu Mtandao wa Mafisadi kufanya Tanzania ni koloni lao. Chukua fedha zao na piga kimya maana ni sehemu ya kodi yako unarudishiwa.

  -Lazima kuishitaki Serekali nzima ya CCM na washirika wake kwenye Mahakama ya Kimataifa ICC kwa kuwaua Watanzania zaidi ya 24 bila hatia yoyote na kuvunja Makazi ya watu kwa ajili ya kuweka wawekezaji.

  -Lazima kuishitaki Serekali nzima ya CCM na washirika wake kwa kuendekeza rushwa na kuifanya iwe ndio sala yao.

  -Lazima kuishitaki Serekali ya CCM na washirika wake kwa kuua viwanga na mashirika ya umma na kujiuzia mali za Taifa kwa bei za kutupa. Angalia ulikotoka, au uklikozaliwa watu wanavyotaabika. Watanzania tuko tayari kutoa ushahidi kama Waliberia walivyotoa kwa CHARLES TAYLOR.

  Waswahili walisema ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni anaweza fanana na ndugu yako, mjomba wako, au vinginevyo. Watanzania tusitumiwe na CCM katika Dini zetu, Kabila zetu ili kuendelea kuwaweka madarakani. Jiulize watu wana mabilioni wameficha ulaya, majumba ya kifahari, magari ya kifahari, mashamba, viwanda, makampuni je wewe Mmatengo, Msukuma, Mhaya, Mmakua, Mkerewe, Mdigo, Mzaramo, Mrangi, Mmbulu, Mmatumbi, Mpogoro, Mdengereko, Mchagga, Mpare, Msambaa, Mmwera, Mnyiramba, Mnyaturu, Muikizu, Mjita, Mha, Mholoholo, Mvinza, na wengine wengi kama mimi Mhaya tuna nini wametuwekezea CCM kwa ajili ya watoto wetu na wajukuu zetu kwa miaka 50. Mbaya kabisa wanamtania mtani wangu wanamwambia ukitaka mzigo ufike mpe Mnyamwezi.

  Hivi kweli Watanzania tumekosa kabisa mtu wetu muaminifu kama Mwalimu Julius Kambara Nyerere wa kumuweka Ikulu. Hebu tuache udini, ukabila, ukanda, tufanye maamuzi sahihi. Dunia inatucheka, majirani zetu wanatucheka kwa utajiri tulio nao lakini hatuna mikakati ya kuondoa Umasikini, Ujinga na Maradhi. Rwanda wamepigana vita leo hii wana mandege yanakuja mpaka Tanzania.

  Kuanzia sasa mgeukie mwenzako alieko karibu nawe na mwambie acha Udini, acha ukabila, acha ukanda, acha kukumbatia rushwa na mafisadi wa CCM. Watanzania kwa pamoja tunaweza kuifanya Tanzania ikazaliwa upya. Nchi imeoza kwa utawala wa Kifisadi. Hivi mtoto wako akila chakula bila ridhaa yako mbona unamkanya. Mbona ndani ya CCM Wizi, rushwa, ubadhirifu, unyang'anyi, mauaji, uporaji, uhamishaji fedha za umma, udhalimu, vimetawala lakini mwenyekiti wao yuko kimya. Watanzania Tuchukueni tahadhari.

  "TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA"
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Pamoja na yote hayo kufahamika na takribani na 35% ya watz(wakaazi wa kwenye miji mikubwa na midogo) ila hali bado inaendelea kuwa mbaya kwamba watz bado wameendelea kuichagua ccm hiyhiyo, rejea mfano wa uchaguzi mdogo wa udiwani juzi!!

  Labda sipo sahihi na data zangu, ila mfano mwingine ni sehemu za mijini ambapo watu wake wanaupenyo na taarifa za mwenendo wa nchi yao na maendeleo ya mataifa mengine kwamba kuchagua njia nyingine ya utawala sio sumu wala dhambi, kwamba inawezekana kuchagua mfumo mwingine wa kujitawala na pia tusiporidhika nao tunaweza kubadilisha mwingine tena (mfano ndugu zetu Kenya), lakini bado jamii hizi za mijini mfano DSM bado watu wameamua kuifia CCM.....

  Kuna aina ya mfumo wa uchumi na elimu imewajenga watu kuamini katika "LEO TU"
  Kwamba as long as napata mkate wangu wa leo basi hayo mengine ni upuuzi tu.....

  Pia ukijumlisha kukata tamaa kwa watu na kuamini kuwa "Siasa ni Wizi mtupu".....

  Tunahitaji jitihada zaidi katika kuubadili huu umma kiakili na namna ya kuangalia mambo kuwa inawezekana kabisa kubadili uongozi wa nchi na kuweka mbadala vilevile na kubadili tena na tena kadiri umma utakavyoamua na kujisikia kulingana maendeleo husika.

  Jitihada kutoka wadau wengine mbali na wanasiasa sababu hii nchi ni yetu sote.

  Kwahali tulipofika ni haki kabisa kutangaza kuwa tuna janga la kitaifa, na lazima zichukuliwe jitihada za kiukombozi kama ambavyo inavyotakiwa wakati taifa linapokuwa kwenye janga.

  Haiwezekani kuwa na taifa kwamba kila mpango wa maendeleo lazima ugubikwe na ulaji wa wakubwa mfano ni sakata linaloendelea katika Umeme, Mafuta, Gesi na Madini kwa uchache kuvitaja...

  Kwa bahati mbaya sana hamna namna nyingine zaidi ya ELIMU kwa watu wetu kuwa INAWEZEKANA kabisa kubadili mfumo wa uongozi wa nchi na baadae kubadili tena na tena kwa kadili ya matakwa ya umma.

  Elimu hii ni ya kutoka pande zote kwamba bila kujali mipaka ya kisiasa tu, ni lazima wadau wote kwanzia mashirika ya dini na mpaka taasisi za kiraia na waandishi wa habari wapaze sauti zaidi katika kueleza uhitaji wa mabadiliko katika uongozi wa nchi.
   
 3. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Inawezekana tukaona labda waTanzania hawataki mageuzi ikawa ndiyo au hapana.Tuangalie na mwenendo wa siasa nchini kwetu je kuna demokrsia ya kweli Tanzania?Je vyama vya siasa sera zake ziko makini au viongozi ni wale wanaopenda kufaidika kwa kutumia elimu ndogo za watanzania?Je kuna uhalali wowote wa Daftari la wapiga kura kutofanyiwa marekebisho kila wakati?Kwanini kusiwe na ofisi za kudumu Tume ya uchaguzi za kanda wilaya ili kila siku daftari liwe linafanyiwa marekebisho au wazungu wanasema "UPDATES" na mwisho kwa nini daftari hili lisiwe computarised na kwamba ifike mahali Mtanzania popote alipo awe na haki ya kupiga kura kuliko ilivyo sasa?Kama ulijiandikisha Mbeya na unaishi Kilimnjaro huna haki ya kupiga kura mpaka ujiandikishe tena?
  Tunaenda na teknolojia ya kisasa tunatakiwa watanzania kwa umoja wetu kuibana TUME YA UCHAGUZI iandane na wakati.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  waliojenga tanzania ya leo wamekufa masikini wakihakikisha vizazi vijavyo vinaishi maisha wazuri

  wanaojenga maisha ya baadae wanataka kuhakikisha mtoto wa maskini wa nchi hii anakufa masikini na watoto wao na wajukuu wanaishi maisha ya kifahari.
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  mkuu nOOb natamani elimu yako ingefika vijijini ndani ya mashina na familia na sio iishie hapa JF!
   
Loading...