Mfumo wa usagaji chakula (digestive system) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa usagaji chakula (digestive system)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 17, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  MFUMO WA USAGAJI CHAKULA (DIGESTIVE SYSTEM)

  Tunakula aina mbali mbali za vyakula ambavyo ndani yake vina kabohaiedreti (wanga), protini, mafuta (fats). Chakula tunachokula huvunjwa vunjwa na kuwa chembe chembe ndogo, ambazo zinaweza kufyonzwa na mwili. Hii harakati yote ya kuvunjwa vunjwa chakula ili kuweza kufyonzwa.

  Mwili una viungo kadhaa vinavohusika kwa pamoja na harakati za usagaji chakula navyo ni:-

  i. Mdomo: Harakati za usagaji chakula huanzia mdomoni. Mdomo una meno, ulimi pamoja na maezi ya mate (salivary glands). Meno husaidia kuvunja vunja chakula kuwa vipande vidogo vidogo zaidi. Matezi hutoa mate ambayo husaidia katika usagaji wa chakula kiwe kilaini zaidi baada kuvunjwa vunjwa, pia hukitia unyevunyevu zaidi vyakula vya wanga kiasi kwamba kiweze kumezwa kwa urahisi zaidi. Ulimi hukichanganya chakula kwa mate na tena hukiviringisha chakula kuwa matonge madogo madogo na kuyasukumiza kwenye koo.

  ii. Umio (Oespoghagus): Hili ni bomba la chakula. Kutoka mdomoni chakula huchukuliwa hado kwenye tumbo kupitia tyubu hii (tube)

  iii. Tumbo (Stomach): Huu ni mfuko wa misuli. Chakula hukaa katika tumbo takriban masaa manne. Kuta za tumbo hutoka maji (gastric juice) kuta hizo ni misuli ambayo hutanuka na kusinyaa ili kukichanganya chakula kwa maji, ambayo sehemu husaga protini.

  iv. Utumbo mdogo (Small intestine): Utumbo mdogo ni mwembamba, mrefu na ni tyubu iliyovirigishwa ugiligili (fluid) kutoka tumboni polepole huingia katika utumbo kwa mafungu madogo madogo. Na usagaji wa chakula huendelea kufanyika. Ini na kongosho (pancrease) huingiza ndani mnyunyizo wao. Nyongo kutoka katika ini huanza kufanyia kazi mafuta wakati maji ya kongosho (pancreatic juice) kutoka kwenye kongosho husaga sehemu ya protini na wanga ambayo haukusagwa. Kuta za utumbo pia hutoa maji ambayo husaidia kukamilisha usagaji wa wanga, protini na mafuta. Chakula kilichosagwa hufyonzwa kwenye damu, na damu hukipeleka chakula hicho katika sehemu zote za mwili.

  v. Utumbo mpana (Large intestine): Chakula kilichobaki amacho hakijasagwa na hakikufyozwa huingi katika utumbo mpana pole pole kwa mafungu madogo. Utumbo mpana ni mfupi zaidi ya utumbo mdogo lakini utumbo mpana hufyonzwa sehemu kubwa ya maji na kuyapeleka katika damu. Chakula ambacho hakikusagwa huhifadhiwa na utumbo mpana na kuwa uchafu (faeces) na baadae hutolewa. Ufyozanji wa chakula huaanza muda mfupi tu chakula kinapoyeyuka ndani ya maji kwahio ni muhimu sana kunywa maji mengi sana kila siku.  CHAKULA KUTOSAGIKA TUMBONI

  Dalili za kutosagika chakula tumboni:
  Kusikia maumivu tumboni
  Kiungulia (maumivu yachomayo nyuma ya mfupa wa kidari)
  Kujihisi mgonjwa au kutapika
  Kupiga miayo au kutoa upepo
  Kuleta ladha ya uchachu mdomoni baada ya kula.

  Kama baada ya kula na kupata dalili yoyote miongoni mwa hizo tutaiita hali hiyo ni kutosagika kwa chakula (Indigestion). Watabibu huiita " Dyspepsia" dalili hizo hutokeza kama kuna kitu kinaleta matatizo katika koo au tumboni.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Wakati tunapomeza chakula husukumwa hadi tumboni kupitia kwenye koo (gullet). Tumbo ni kama mfuko wa misuli na hukaa na chakula kabla ya kukisukuma kupitia kwenye deodeni (duodenum) ambao ndio mwanzo wa utumbo. Chakula kinapowasili kunyazi cha tumbo huanza kuzalisha asidi ili kuvunja vunja chakula na kukifanya kiwe rahisi kusagika. Asidi ina nguvu sana na kama ingekuwa peke yake bila kuwepo tabaka la mnyunyizo uliogandana unaoitwa utelezi (mucus) ambao huzifunika kunyazi ili kuilinda, asidi basi ingeweza kulimong'onyoa tumbo lote.

  Hakika shukurani zote anastahili Allah S.W kwa mpango wa uumbaji wake wenye hikma kubwa mno.
  " YEYE (MWENYEZI MUNGU) NDIE ANAEWATENGENEZENI SURA MATUMBONI JINSI APENDAVYO HAKUNA WA KUABUDIWA ILA YEYE, MWENYE NGUVU MWENYE HIKIMA" (3:6)


  Uislam umekataza kula kwa kupindukia kiasi. Madhara yake ni mengi mno, lakini mojawapo katika hayo ni kuharibu ustawi wa afya. Mwenyezi Mungu ametuonya juu ya jambo hili kwa kusema:
  " ....... NA KULENI (VIZURI) NA KUNYWENI (VIZURI), LAKINI MSIPITIE KIASI TU. HAKIKA YEYE (MWENYEZI MUNGU) HAWAPENDI WAPITAO KIASI." (7:31)


  Sababu hasa ya kutosagika chakula tumboni ni kula sana au kunywa kupita kiasi au kula mlo usio sawa pombe vyakula vya mafuta mengi kama chipsi vyakula vyenye asidi nyingi kama vile machungwa lakini kwa bahati mbaya au nzuri hakuna seti moja ya kanuni juu ya ule nini au usile nini. Watu hutofautiana katika kudhurika na vyakula, hivyo ni suala tu la kuainisha mwenyewe ni chakula gani ambacho kinakudhuru na halafu akakiacha.

  Baadhi ya watu, hukutana na matatizo ya kutosagika chakula chochote kile watakachokila. Hawa wanaweza kuwa wanasumbuliwa na mojawapo ya matatizo kadhaa kwa mfumo wa usagaji chakula.

  UVIMBE (GASTRITIS)
  Kama kuna asidi nyingi sana na utetelezi (mucus) unaofanya kazi ya kuizua asidi ni ndogo tumboni, hapo asidi huanza kudhuru kunyazi za tumbo (stomach lining). Kwa hali hiyo utakabiliwa na tatizo la kutosagika chakula kwahio huo unakuwa ni uvimbe-tumbo (uvimbe mwasho wa kunyanzi za tumbo)

  Namna mbalimbali za vyakula vinaweza kuuvuruga ulingano wa asidi na utetlezi. Vile vile uvutaji sigara madawa (kama vile aspirini) au matatizo ya mhemko (emetional problems) huwa ndio sababu kuu, na mara nyengine hakuna sababu ya wazi zaidi. Mara kwa mara tatizo la aina hii la kutosagika chakula hujimaliza wenyewe hatimaye. Utakapoacha kutumiwa dawa au kubadilisha dawa na kutumia aina nyengine za dawa za matatizo ya mihemeko yataondoka kunyanzi za tumbo nazo zitajikarabati wenyewe na tatizo la kutosagika chakula litakwisha Inshallah.

  Mara nyingi zaidi unaweza kujitibu mwenyewe matatizo ya kutosagika chakula lakini kama utakumbana na mojawapo wa dalili hizi zinazofuatia utatakiwa umuone doktari.:

  1. Maumivu makali ambayo huzui shughuli zako kila siku.
  2. Maumivu ya kila siku zaidi ya siku 3
  3. Maumivu ya mara kwa mara ambayo huendelea kurudi kwa baada ya wiki 2
  4. Maumivu ya mgongo baada ya kula.
  5. Kupoteza uzito bila sababu.
  6. Kupoteza hamu ya kula.
  7 Maumivu nyuma ya mfupa wa kidari wakati wa mazoezi au baada ya mazoezi


  KUJITIBU MWENYEWE
  I.Kula kwa makini
  Epuka vyakula na vinywaji vinavyokudhuru.
  Usile mara kwa mara
  Usile muda mfupi tu kabla ya kulala
  Epuka vinywaji vyenye asili ya maziwa.


  Kwa kufanya hivo utazuia tumbo lako kuzalisha asidi nyingi.

  II.Acha kuvuta sigara
  Uvutaji sigara unaweza kusababisha chakula kisisagike.
  Wavutaji hupata vidonda vya tumbo kwa urahisi.


  III.Badilisha mtindo wa maisha yako
  Kutosagika chakula kunaweza kusababishwa na mfadhaiko unaotokana na shida za kimaisha, tabu dhiki, matatizo na mambo kama hayo.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Sala ambayo husaliwa mara tano kwa kila siku ni ibada yenye kuleta utulivu mkubwa wa kiroho. Sala humuondolea mja khofu, huzuni, wasiwasi kwa jambo ambalo linamtatiza au liko nje ya uwezo wake. Mtu baada ya kufanya juhudi zake zote za kimaisha, baadae humelekea Allah S.W na kumuomba uongozi na msaada. Kwahio ibada ya salaa inatosha kuwa kinga ya maradhi pamoja na balaa ya kila aina.

  Dhibiti uzito wako.
  Watu wenye uzuto mkubwa sana wanafursa zaidi ya kukubwa na tatizo la kutosagika kwa chakula, punguza uzito. Uislam umezungumzia juu ya habari hii ya kudhibiti uzito kwa ajili ya afya yako. Mtume S.A.W anasema: "Yatosha kwa mtu kuondosha njaa kwa matonge machache ili kuimarisha uti wake wa mgongo''. Kama unataka kula hadi kushiba, basi uache theluthi moja ya chakula theluji moja ya maji na theluthi moja ya hewa" (Tirmidh)

  Jaribu dawa.
  Kama kutosagika kwako chakula hakujakuletea tatizo kubwa sana, basi jaribu dawa za kuzima asidi (anti-acid) ambazo hufanya kazi ya kubatilisha asidi ya tumbo na kuifanya isiwe na madhara.


  MATIBABU MAALUM

  Inawezekana kwamba dalili zako (za kutosagika kwa chakula) zinamaanisha kuwa na hali ambayo inahitaji matibabu zaidi.

  Kupwa kwa asidi (Acid reflux)
  Asidi ndani ya tumbo zinaweza kuchoma chini ya koo na kusababisha kiungulia, maradhi yatokanayo na kupwa yanaweza kuwa na sababu tofauti tofauti.

  Ngiri (Hiatus hernia)
  Kiasi cha mpasuko wa sehemu ya juu ya tumbo kupitia kiwambo (diaphgram) husababisha ngiri, ni kawaida sana hasa kwa watu wenye uzito mkubwa wanawake na wagonjwa wanasikia kuingulia pindi wanapolala kwa kunyooka au kujikunja.

  Ugumu unaoota kwenye nyongo (gallstone)
  Nyongo ni maji maji yenye mchanganyiko wa rangi ya njano na kijani (yellowish-green) yanayotengenezwa kaika ini, kisha yakahifadhiwa katika kibofu nyongo (gall bladder) na kupelekwa katika mahala ambapo husaidia kuyeyusha mafuta. Wakati mwengine kutosagika kwa chakula kunaweza kusababishwa na ugumu unaoota kwenye nyongo.

  Vidonda vya tumbo (ulcer)
  Kidonda chenye pepsini ni baka bichi ambalo hutokea katika kunyazi za tumbo au duodeni aisha kwa sababu kuna asidi nyingi sana ama utetelezi wenye kuzui asidi ni mdogo.

  Kwahio ni muhimu kujitizama afya zetu ile tuepukane na matatizo madogo madogo kama hayo ambayo baadae huweza yakawa ni maradhi makubwa.
   
 4. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ubarikiwe Mzizi Mkavu, Elimu unayotoa hapa ni ya Bure, hailipiwi. Asante
   
 5. dony2680

  dony2680 JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ubarikiwe kwa elimu nzuri dk
   
Loading...