Mfumo wa kuwapata Wakurugenzi wa Halmashauri uwe wa kuomba kazi, wanaopata ndio wateuliwe

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wakati umefika sasa kama kweli tunataka maendeleo basi hatuna budi kuachana na kufanya kazi kwa mazoea.

Wakurugenzi ni watu wenye taaluma ni wakati sasa watu wote wanaotaka kazi ya ukurugenzi waandike barua zao za maombi wakiambatanisha vyeti na uzoefu wao wa kiutendaji bila kujali itikadi za chama kuna watendaji wazuri sana nje ya chama wenye sifa nzuri zaidi ya waliomo kwenye chama ila wameshindwa kupata nafasi kutokana na ukurugenzi kuwa kisiasa zaidi.

Baada ya mchujo wa maombi wale watakaoshinda ndio rais awateue kuwa wakurugenzi badala ya utaratibu wa sasa wakuteua tu.
 
E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Siyo kwa CCM hii kaka, wanateua wale ambao watakubali kumtangaza mgombea wa CCM hata kama hajashinda uchaguzi.
 
Back
Top Bottom