Mfumo wa kukuwezesha kujua taarifa za hospitali/vituo vya afya

Dr. Wansegamila

Verified Member
Feb 3, 2012
2,260
2,000
Mfumo wa Hospital Info inarahisisha upatikanaji wa taarifa kuhusu hospitali na vituo vya afya (huduma zinazotoa,kadi za afya zinazokubaliwa kwenye hospitali husika,muda wa kazi,umiliki wa hospitali na mahali ilipo na maelezo mafupi kuhusu huduma husika) kupitia application ya android, Web App, pamoja na SMS za kawaida,kiasi kwamba hata wenye simu ambazo sio smart phones watanufaika na kuweza kupata taarifa hizo kiganjani mwao.
Pia, taarifa hizi zitapatikana kwa lugha za kiswahili na kingereza.
Unaweza kuufanyia majaribio mfumo huo sasa kwa kutuma meseji yenye aina ya huduma unayoulizia + Wilaya (mfano Uzazi wa mpango Ilala) kwenda namba *0765 034981* utapata maelezo ya hospitali/vituo vya afya ambavyo vinatoa huduma hiyo na maelezo mengine.
Mfumo huu kwa sasa bado uko katika majaribio, na kwa sasa wilaya ambazo unaweza kupata majibu ninwilaya mbili tu za *Ilala* and *Kyela*.
Maoni na ushauri zaidi yanakaribishwa.
c63a049be24731c2d1fec38864c0273a.jpg
 

Dr. Wansegamila

Verified Member
Feb 3, 2012
2,260
2,000
Gazeti la The Citizen la tarehe 22 December limeandika kuhusu Project hii ya ku develop "Hospital Info" System; Mfumo ambao utawezesha upatikanaji wa taarifa za hospitali na vituo vya afya kiganjani mwako, soma hiyo makala hapa chini


98b387f586b6d19989b755667c1b42e9.jpg

Mr.laravel
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom