Mfumo wa kisasa kuwabana wakwepa kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa kisasa kuwabana wakwepa kodi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Herry Kitilya akionyesha mashine mpya za matumizi mapya ya mfumo wa kodi wa kutumia za regista zilizozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.Mashine hizo zitakuwa zimeunganishwa kwenye mfumo wa TRA kukwepa ulipaji kodi

  Jackson Odoyo

  MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imekuja na mbinu mpya ya kuwabana wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kuanzisha rejesta za kodi za kielektroniki.

  Kamishina Mkuu wa TRA, Harry Kitillya aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana kuwa hivi sasa watatumia mashine hizo maalum zitakazopokea taarifa za wafanya biashara wote nchini.

  “Tumeanzisha mfumo maalum wa kutumia umeme kwa ajili ya kuwabana wakwepa kodi wote na mfumo huo, utaanza rasmi Julai Mosi mwaka huu kwa wafanyabiashara waliojiandikisha na VAT. Wafanyabiashara hawa hawatatumia tena rejesta za fedha bali mashine hizi mpya," alisema.

  Alisema mashine hizo, zitatumika kutoa risiti na kuhifadhi kumbukumbu za wafanyabiashara wote nchini na baada ya miaka mitano kupita,taarifa zinafutwa na kuanza upya.

  Alisema wafanyabiashara wote watatakiwa kununua mashine hiyo kwa Sh1 milioni na Sh5 milioni na watarejeshewa fedha zao kila wanapolipa kodi.

  “Mashine hizo, zina uwezo wa kutoa kumbukumbu za mfanyabiasha kila anapouza bidhaa zake na kumkatia mteja risiti na akiuza bidhaa bila kutoa risiti pia mashine hiyo itatoa taarifa kwenye mitambo yetu,”alisema Kitillya.

  Alifafanua kuwa mashine hizo zitaisaidia TRA kuwabana wafanyabiashara wanatumia mtindo wa kuuza bidhaa bila kutoa risiti kwa lengo la kukwepa kodi na watakaobainishwa kwa njia ya mashine kuwa wanakwepa kodi watatozwa faini ya Sh2 milioni.

  "Wamiliki wa mashine hizi watatakiwa kutunza kumbukumbu sahihi za biashara zao. Lengo ni kuhakikisha tudhibiti taarifa za kodi na hasa kupunguza au kuondoa kabisa utoaji risiti zisizo sahihi,"alisema.

  Kuhusu ubora wa mashine hizo, Kitillya alisema zina uwezo wa kutoa taarifa sahihi na kutoa ishara pale hujuma yoyote itafanyika katika mashine hiyo.

  Kamishna huyo alifafanua kuwa kumbukumbu zote katika mashine hiyo, haiwezi kuharibiwa na kemikali yoyote wa muingiliano wowote wa sumaku na kwamba zina uwezo wa kutoa taarifa ya mauzo kila baada ya saa 24 na kutuma taarifa za kodi moja kwa moja TRA.

  “Mashine hizo haizimruhusu mfanyabiasha kubadili tarehe, zinatoa risiti ambazo ni vigumu kughushiwa, zitatumika nchi nzima huku zikiwa na uwezo wa kufanya kazi kwa saa 48 katika maeneo yenye umeme na yasiokuwa na umeme zitatumika kwa sababu zina mfumo wa betri," alifafanua Kitillya.

  Alisema mashine hizo zinatengenezwa katika nchi za Italia na Bulgaria na kwa Italia zinatengezwa na kampuni za Custom Engineering SPA na RCH-ASP na nchini Bulgaria ni kampuni za Datecs Ltd pamoja na Incotex Systems Ltd.

  Kuhusu wasambazaji wa mashine hizo nchini Kitilya alisema a zinasambazwa na wasambazaji sita ambao ni Business Machines Tanzania Ltd, Advatech Office Supplies, Techno Crats Ltd, Pergamon Ltd, Total Fiscal Solution pamoja na Compulynx na kwamba zote zimedhibitishwa na TRA.

  Katika hatua nyingine Kitilya alisema kuwa TRA imekusanya kodi kwa asilimia 92.6 ambayo ni sawa na trilioni 3 na kuvuka lengo lengo waliojiwekea mwaka huu.
  Mfumo wa kisasa kuwabana wakwepa kodi
   
Loading...