RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Tanzania inatumia mfumo wa kupata taarifa za kiusalama kuhusu watu wanaotoka na kuingia nchini bila kuwa na udhibiti wa moja kwa moja wa mfumo huo kwa kutokuwa na nywila(Password) ambayo inashikiliwa na Marekani.
Mfumo huo wa kielektroniki unafahamika kwa jina la PISCES(Personal Identification Security Comparison and Evaluation System) ulifungwa nchini mwaka 2003 na bado unamilikiwa na kampuni ya Booz Allen Hamilton ya Marekani inayodaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Idara ya Usalama wa Taifa wa Marekani.
Kutokana na kutokuwa na umiliki wa password ya mfumo huo, inabidi idara ya Uhamiaji hapa nchini iombe kibali kutoka kampuni hiyo endapo kuna kitu kinahitajika.
Kwa mujibu wa taarifa kwenye mitandao mbalimbali Tanzania ilipewa mfumo huo kama sehemu ya msaada kutoka wizara ya mambo ya nje ya marekani kupitia idara yake ya kupambana na ugaidi.
Mfumo huo umefungwa katika viwanja tano vikubwa vya ndege hapa nchini na katika vituo vya mpakani kama Namanga, Holili na Tunduma.
Mfumo huo umeunganisha vituo hivyo na makao makuu ya idara ya uhamiaji.
Mmoja wa waajiriwa maarufu wa zamani wa kampuni ya Booz Hamilton ni Edward Snowden.
Chanzo: Raia Mwema