Mfumo wa elektroniki wafeli tena uchaguzi Malawi

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Ulianza kufeli Marekani, Ulifeli Malaysia, ukafeli Kenya, na sasa umefeli tena Malawi.
Kwa Tanzania ni sahihi zaidi tukajifananisha na Kenya na Malawi...

Nitashangaa sana endapo tume ya uchaguzi Tanzania wataendelea na mchakato wao wa kuandaa uchaguzi mkuu ujao ufanyike kwa mfumo huo...
======================================

Maafisa wa uchaguzi nchini Malawi, wanasema kuwa wamelazimika kutumia vipepesi na barua pepe kujumlisha kura za uchaguzi mkuu baada ya mfumo wa elektroniki kuharibika.
Makarani wa tume ya uchaguzi waliopo mashinani wameshindwa kutuma tarakimu za matokeo ya kura hizo.

Haya ndio matatizo ya hivi punde kushuhudiwa katika uchaguzi huo lakini maafisa wamesema wamejitolea kufanya kazi.

Shughuli ya kupiga kura iliongezwa muda kwa siku ya pili

Katika baadhi ya maeneo masanduku ya kura hayakuwasilishwa na baadhi ya vituo vilifunguliwa kuchelewa siku ya jumanne na kulazimisha maafisa kutumia ndoo na katarasi za plastiki kukusanya kura.

Raia wa sasa Joyce Banda anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wengine kumi na moja.
Baadhi ya vituo vilifungua kuchelewa Jumanne na kusababisha shughuli ya upigaji kura kuongezwa muda kwa siku ya pili.
Rais wa sasa Joyce Banda,anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wengine 11.

Chanzo:BBC
 
Mkya

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
668
0
2015 mtake mistake tunaenda kwenye digital mambo ya analogia hapana hii itasaidia kuwa kiisingizio ukawa kuwa wameibiwa kisasa
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,595
2,000
Jeshi la Ulinzi la Malawi(MDF) pamoja na Jeshi la Polisi wavamia Nyumbani kwa Mgombea Urais wa Upinzani Peter Mutharika anayeendelea kuongoza kwa asilimia 39 na kufuatiwa na Lazarus Chakwera 31% wa chama cha MCP

Malawi inaendelea kuonyesha jinsi watawala Afrika wasivyokuwa waumini wa Demokrasia

Nimepongeza msimamo mkali aliouonyesha Peter Mutharika na Kumuonya Joyce Banda juu ya jaribio lolote la Kuvuruga uchaguzi

Naibu Waziri Godfrey Kanyama aliyeshindwa Ubunge Huko Lilongwe amejipiga Risasi baada ya kuacha wosia na Suicide Note.Huyu ni Naibu waziri aliyekua mstari wa Mbele katika kukichafua chama cha upinzani cha DPP na kutamka kuwa chama hicho kinachoongozwa na Peter Mutharika ni Ugonjwa Mbaya utakaowaua Wamalawi

Sasa kama jumuiya ya Kimataifa na hasa jumuiya ya SADC kama haitakua makini kukemea tabia hii,taifa la Malawi litaingia katika Machafuko

Chama tawala cha Joyce Banda kinakituhumu chama cha Upinzani cha DPP kuwa kinafanya wizi wa Kura kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi.Leo chama tawala kinatuhumu upinzani kwa wizi wa Kura? Hillarious Indeed...!

Ni shambulio kwa Demokrasia(Assault on Demecracy) kutumia Jeshi kuzima sauti za Wapiga Kura.Hili halitakiwi kuvumiliwa hata kidogo.Kama SADC na Umoja wa Afrika zinakemea Mapinduzi ya Kijeshi (Coup D'tat)basi ni lazima zikemee mapinduzi ya Matakwa ya Umma (Coup Civillien).Kutumia nguvu kuzima sauti za Raia kupitia sanduku la kura hazina tofauti na kupindua tawala zilizochaguliwa Kidemokrasia

As long as namtakia Joyce Banda kushindwa uchaguzi huu,naendelea kuombea Matokeo mema kwa Upinzani na pia Msimamo thabiti dhidi ya Chama Tawala katika kipindi hiki.Tusishangae Joyce Banda akatangaza Hali ya Hatari na kutia doa na aibu nyingine

I don't know what's Wrong with Africa.
 
Wanamlinda raisi wao siyo wamevamia wanasema wanaangalia usalama wake
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
3,950
2,000
Kwa kweli kushindwa kwa mama Joyce Banda na chama chake tawala cha PP ni kidonge kichungu - lakini busara kwake ingekuwa kukimeza bila makeke, kwani kwa kuleta ubishi (uwezao kuleta machafuko) anazidi kujichafua mwenyewe.
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,363
2,000
Mama alimtunishia misuli Rais wetu mpaka tukamwona mwoga kama mbwa koko sasa ngoja achezee kichapo cha raia! Itakuwa faraja sana kwa familia ya Wa Mutharika kutokana na jinsi Joyce Wowowo Banda alivyoigeuka ile familia mara tu baada ya kuingia madarakani. Nahisi kama atakimbia nchi huyu! Hongera Peter, hongera DPP!!
 
Balacuda

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,390
2,000
Mbona Botswana walipiga kura ndani ya masaa mawili matokeo yalishatoka. wote walipiga kwa njia ya simu, hakuna aliekwenda kituoni labda kwa watu wenye mahitaji maalum sana
 
NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
its a shame with all the advancements in technology kama tutashindwa kitu kidogo kama kupiga kura, najua kuna implications kibao na watu wanahofia hacking pia, maana kuweka kitu kikubwa kama urais kwenye mikono ya programmer yaweza kusiwe na uaminifu.. hii system ni ngumu kuifanikisha ukizingatia hata vitambulisho vya taifa si kila mtu mwenye nacho na havifati system nzuri ya electronics... hakuna database iliyosimama vizuri yenye data za kila mtanzania, hiyo ingerahisisha hili kufanikiwa, by 2015 sidhani kama tutaweza, ni mapema mno.. labda wajipange for 2020
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,300
2,000
Ukiskia eti mfumo wa electronic ume-fail hasa katika nchi zetu za kiafrika mwenye akili anajua Serikali ambayo hiko madarakani inatafuta mbinu za kuchakachua matokeo, mambo yalikuwa hayamwendei vizuri mama Banda, sina shaka wapambe wake wamemshauri avuruge uchaguzi kwa kusingizia mitambo ya electronic.

Nikichekesho kabisa, Serikali inasema eti watumie simu kutuma message za matokeo kutoka kila kituo as if mitandao ya simu sio za ki-electronic, wako crafty kweli kweli wanajua ni rahisi sana kuchakachua messanging servers za Makampuni ya simu kwa kupewa amri na Serikali wakishirikiana na ma CEO wa makampuni ya simu - kumbuka hili ndilo lililo tokea kwa majirani zetu siku za nyuma, mama Banda ni rahisi kuomba msaada kutoka kwa jamaa hao akihisi mambo yanamwedea KOMBO, na hiki ndicho kinacho endelea nchini Malawi hivi sasa.
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,300
2,000
Mbona Botswana walipiga kura ndani ya masaa mawili matokeo yalishatoka. wote walipiga kwa njia ya simu, hakuna aliekwenda kituoni labda kwa watu wenye mahitaji maalum sana

Viongozi wa Botswana wanajali sana demokrasia na ni wastaarabu hawana tofauti na India, chama kikishindwa kinaondoka madarakani bila labsha, lakini tatizo la nchi nyingi za Kiafrica ni kuongoza nchi ki-dikteita ni vig'ang'anizi hawataki kuondoka madarakani kwa kuhofia kushtakiwa kwa makosa ya nyuma, watatoa visingizio vya kila sampuli vya kuwawezesha kuendelea kubaki madarakani, kama sio wao watahakikisha chama kilicho madarakani kinaongoza milele au kinabaki madarakani in his/her lifetime; hawafikirii mara mbili kutumia iron fist kutimiza malengo yao uki-cross redline uta endup in a slammer kwa visingizio mbali mbali.
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
19,650
2,000
Ulianza kufeli Marekani, Ulifeli Malaysia, ukafeli Kenya, na sasa umefeli tena Malawi.
Kwa Tanzania ni sahihi zaidi tukajifananisha na Kenya na Malawi...

Nitashangaa sana endapo tume ya uchaguzi Tanzania wataendelea na mchakato wao wa kuandaa uchaguzi mkuu ujao ufanyike kwa mfumo huo...
======================================Chanzo:BBC

Wabongo mmechelewa hapa, labda 2020 lakini uchaguzi ujao sio practical kuufanya kielektroniki. Mimi kama mtaalamu wa maswala ya systems na nilihusika pakubwa kwetu Kenya hapa kwenye analysis, jameni sio jambo rahisi. Pia ikumbukwe hili ni jambo linawahusu wanasiasa na wengi wao ufaulu kupitia lack of transparency.
 
mimi sio mtaalam wa computer lakini kwa uelewa mdogo nilionao nashindwa kujua tatizo lilipo, is it a programming problem? (how?), lack of experts or lack of other resources like servers and laptops? hebu fafanua.
 
Kaka, system kama hii huwa sio tu maswala ya hardware ama software, bali kuna mengi uhusika kwenye system implementation, haswa kama hii ya inayogusa wanasiasa na ambao wanajijua hawawezi jimudu kwenye fair and transparent approach. Mimi mwenyewe (programmer mzoefu) nilihusika kutengeneza system hapa kwetu kipindi kile tukifanya lobbying, na tulikumbana na mengi. Haswa changamoto nyingi
- Vita toka kwa makampuni yale hukodiwa wakati wa uchaguzi, kama ya usafirishaji, uchapishaji, brokers n.k.
- Wanasiasa wakongwe wasiojua hata kutumia tarakilishi, hawaamini chochote kinachohusiana na elektroniki
- Wanasheria hawakuchelewa na vipengee kwenye sheria vya kutuzuia
- Waafrika kutoaminiana hadi uamuzi ukafanyika wa kununua system tokea nje ambayo ilianguka tu siku ya kwanza
- Asilimia kubwa ya jamii kuogopa teknolojia na kutoiamini

Yaani kuna mengi naweza nikaandika kurasa kadhaa. Changamoto nyingi lazima zitatuliwe hata kabla hujaanza kuwaza ni system ipi utatumia. Bongo naona muna mwaka mmoja tu, ni vigumu sana kufaulu kwa muda mfupi huo.
 
wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
3,989
2,000
Ulianza kufeli Marekani, Ulifeli Malaysia, ukafeli Kenya, na sasa umefeli tena Malawi.
Kwa Tanzania ni sahihi zaidi tukajifananisha na Kenya na Malawi...

Nitashangaa sana endapo tume ya uchaguzi Tanzania wataendelea na mchakato wao wa kuandaa uchaguzi mkuu ujao ufanyike kwa mfumo huo...
======================================Chanzo:BBC
Nltaka kushangaa mwanamke kuwaongoza waafrika tena weus tii kwa awam 2 hio haiwezekan
 
Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Mbona Botswana walipiga kura ndani ya masaa mawili matokeo yalishatoka. wote walipiga kwa njia ya simu, hakuna aliekwenda kituoni labda kwa watu wenye mahitaji maalum sana

Ni vigumu sana kwa Tz kujifananisha na Botswana. Wenzetu wapo mbele sana kimaendeleo na kidemokrasia...
 
jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,937
2,000
Afrika kuna msemo.....'' Usihangaike na wapiga kura, hangaika na wahesabu kura''
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom