Mfumo wa ccm kutetea ndio unaoiangamiza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa ccm kutetea ndio unaoiangamiza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by benito musolin, Apr 20, 2012.

 1. b

  benito musolin New Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia bunge la tanzania kwa muda mrefu sasa tangu zama za spika sitta hadi sasa anne makinda a.k.a bi chau.nimegundua mapungufu mangi sana,lakini moja wapo lililo kubwa zaidi ni hili la chama cha mapinduzi kuweka uzalendo pembeni na kuteteana ili kuficha maovu.Tumeona ccm na serikali yake ilifanya kufanya kila aina ya mbinu il kuzuiya bwana edward lowasa asijiuzuli lakini kwa vile spika sitta alikuwa mzalendo aliruhusu hoja kuibuka ambazo zililazimu mawaziri watatu wajiuzulu,hili halikuwafurahisha ccm hata kidogo. Chuki ikajengwa kwa sitta akavuliwa uspika hivihivi.Huku wakidai eti ni zama za wanawake.

  Tumeona juzi ndugu zetu wakifa muhimbili anne makinda akizima hoja za wabunge kwa ubabe mkubwa bungeni ili kutetea wanaccm wenzake ambao wamevurunda.si ajabu hata hili likazimwa bila kujulikana limeishia wapi.Mfumo huu wa kulindana ndiyo uliotumika tena kwenye ishu za kina Jairo na Ngeleja walipohonga ili bajeti yao ipitishwe Luhanjo akasimama kati na kutakasa wizi wananchi walipokuwa wakali JK AJAJIDAI kutoa tamko na wala si kumfukuza kazi jairo.
  Sasa la Jairo mmelisikia tena? Mapendekezo ya kamati ya mwakyembe yako wapi? chenge na reda yuko wapi?WOTE HAWA NI WEZI WAKUBWA ila hawagusu kutokana na huu mfumo wa ccm wa kulindana.

  Hili nalo je mfumo utatumika ili kuwalinda au wajiuzulu na kufunguliwa mashtaka?kazi kwenu wana JF
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Minapenda waendelee kuteteana ndo ukombozi unakuja kwa haraka!
   
 3. b

  benito musolin New Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  wanateteana kuku wanaiba kwa sana tukisubiri mno watatuuua hawana utu kabisa.umeangalia hayo mabilioni kwenye ripot ya CAG?
   
 4. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila kweli, wakichukua hatua kwa hili watapata credits japo kidogo. Kwa sasa wako ICU, wakichukua hatua watarudi wodini na kupata matumaini kidogo ya kuishi. Bora wavurunde kwa kuuchuna ili wafe kabisa.
   
Loading...