Mfumo dume ni nini?

Lady niece

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
953
Reaction score
414
Mwadilla


Kuna wanawake fulani nilikuwa nao jana kwenye semina niliwasikia wakisema kuwa wamechoka na mfumo dume yaani ile kugandamizwa
kwa kila kitu kwao imeshawachosha wanadiliki hata kukaa na kuambiana niini wafanye ili kutokomeza mfumo huu. sasa mm nimekaa nikajiuliza huu MFUMO DUME ukojena nini maana yake?

KWA WANAUME

Wanaume wamekuwa ni wanyonyaji sana dhidi ya wanawake Katika kuadhimisha siku ile ya wanawake slogan kubwa ilikuwa ni ugandamizaji na kuondoa mfumo dume ulioko unaowakumba wanawake wengi, Wengi wao wamekuwa hawana usemi juu ya waume zao na wengine wanapigwa utadhani wanapiga ngoma kumbe ni mtu hii iko kanda ya ziwa mkoa fulani, eti wanadai kuwa ni mapenzi na kumbe si chochote ni ugandamizaji na unyanyasaji uliokithiri juu ya wanawake.

Marafiki zangu je mwalionaje hili hebu tusongeeni tujadili kwanini huu mfumo dume umekuwa kwa kasi sana duniani na hasa bara hiili la afrika. Toeni maoni yenu hasa wanawake
wa hapa JF na wale.
 
Mfumo dume ninavyoelewa ni kwamba Mwanaume anakuwa na sauti kuliko mwanamke... yeye ndo kila kitu na akisema kitu lazima kifwatwe. Kuhusu kupingana na mfumo Dume, hebu kwanza tuache haya mambo ya haki sawa kwa wote kwa kutaka kupata nyadhifa burebure kwa viti maalum.. tusimame wenyewe kwa miguu yetu na kugombea.. tuachane na Mwanamke akiwezeshwa anaweza bali tujiwezeshe wenyewe kwanza.
 
asante kwa kunifungua macho rafiki

 
Mfumo dume unaanzia kwenye familia yako, wewe kama mzazi unapokuwa na watoto wa kike na wa kiume na ukawa unawalea kwa kuwagawa hawa wa kiume na hawa wa kike basi hiyo hubaki kichwani mwao hata ukubwani, mfano kama ni kupika wapike wote, kuna kufanya usafi wafanye wote, wewe baba usifanye maamuzi ya familia mara zote pasipo kumshirikisha mama, usigombane na kupigana au kuzozana na mkeo mbele ya wanao, wapeleke shule wote, orodha inaendelea...
 
#Rafiki nadhani unaongelea vitu viwili tofauti MFUMO DUME na UNYANYASAJI WA WANAWAKE.

Unataka tuongelee kipi?

Kama ni mfumo Dume tu huo ni asili. Me ni superior to Ke. Ila likija swala la kuonewa na kunyanyaswa, huo sio mfumo bali ni ukatili na kutokujitambua kwa baadhi ya watu waliopo kwenye huo mfumo, au pengine mila na destruri za pahala na pahala ikiwemo pia imani potofu juu ya nafasi ya mwanamke kwenye jamii.

 
ninachozungumzia rafiki ni MFUMO DUME ambao unawagandamiza wanawake wasipate haki zao kimisingi

 
mfumo dume na udumu.....

laizma sheria zifuatwe, ziliwekwa toka enzi na enzi!! wewe umekuwa nani mpaka kuhoji leo??

kwanza kumbuka bila mwanaume, mwanamke usingekuwepo...
 

Mwanamke akiwezeshwa anaweza. Bila kuwezeshwa hawezi. Mwanaume awezeshwe au asiwezeshwe, anaweza. Tofauti hiyo ndio inazaa mfumo dume!
 
Mie nadhani huu udume fumo utaisha pale tu mwanamke atapojitambua na kujua kuwa hata yeye anaweza bila kutegemea mwanaume. Yes inawezekana tukiamua sio kila kitu utegemee mwanaume asipokohoa jiko haliwashwi. wake up ladies. Yale maneno ya kuwa bila mwanaume huweziishi yaondoe maana mwanaume sio pumzi yako.
 
wanawake tulikuwepo tangia mwanzo wa kuumbwa dunia na tulifichwa sehemu tukingojea majira ya kutokea ndipo Mungu akasema tutoke hivyo wewe si mtu wa kutumbia kuwa eti pasipo mwanaume tusingekuwepo bali niwaulize ninyi wanaume Je Mungu asingeweka sehemu ya kupitishia viumbe kwetu mngeonekana nyie au ndo yaleyale

mfumo dume na udumu.....

laizma sheria zifuatwe, ziliwekwa toka enzi na enzi!! wewe umekuwa nani mpaka kuhoji leo??

kwanza kumbuka bila mwanaume, mwanamke usingekuwepo...
 
umeongea vyema rafiki waambie hata wenzao wajue hili kwani wao wamekuwa chanzo cha mfumo dume

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…