Mfuko wa taifa wa bima ya afya (nhif) jirekebisheni.

GREGORY J

Member
Jul 7, 2011
10
45
Kwa masikitiko makubwa napenda kuuandikia uongozi wa mfuko huu kuchukua hatua na za haraka ili kurekebisha uzembe unaofanywa na maafisa wa mfuko huu. Mimi ni mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, mnamo mwezi wa sita nilijaza fomu kwa ajili ya kupata kadi ya uanachama ya mwanangu. Nilipeleka fomu yangu makao makuu ya mfuko kurasini na nikaahidiwa kwamba kadi ingetoka baada ya mwezi mmoja na ingetumwa kwa mwajiri wangu. Lakini cha ajabu hadi ninapoandika ujumbe huu kadi haijulikani ilipo. Kadi haijapokelewa na mwajiri wangu hadi ninapoandika ujumbe huu. Nilianza kuifuatilia tangu mwezi wa saba, jibu walilonipa ni kuwa kadi imeshatoka na wakaniambia nikaangalie kwenye ofisi za kanda zilizopo Tumbi Kibaha. Nilipofika Tumbi sikuikuta wala hakukuwa na document yoyote inayothibitisha kuwa kadi ilitumwa kibaha. Walipojaribu kufuatilia wakasema ilikuwa imetumwa Morogoro kimakosa kwa hiyo walinipa namba ya simu ya afisa wa Morogoro. Nilipofatilia kwa hiyo jamaa akasema yeye hana hiyo kadi. Baadae nilirudi tena makao makuu wakajaribu tena kucheki jibu walilonipa ni kuwa kadi imetumwa kimakosa katika wilaya ya mafia, nilipewa namba ya simu ya coordinator wa Mafia na nilipofatilia nae akasema kwamba kadi hiyo haikutumwa kwake. Tatizo lililopo ni kwamba kadi haijafika mikononi mwangu tangu itengenezwe mwezi wa saba tarehe 12. Jukumu la kufuatilia upotevu huu wameniachia mimi naona hakuna hata afisa mmoja wa mfuko huu anayechukua hatua. Wiki iliyopita mwanangu aliugua na nilipoenda kwenye ofisi za bima nikaambiwa hawezi kupatiwa matibabu kwa sababu hana kadi na hawawezi kutoa barua ili akatibiwe kwa sababu kadi yake ilishatengenezwa sasa wanandungu hapo nifanyeje??? naomba kuwasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom