Mfuko wa Maendeleo Jimbo la Vunjo watoa kipaumbele Miradi ya Elimu, Afya na Miundombinu ya barabara

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ameongoza kikao cha kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo hilo kilichosimamia ugawaji wa fedha kwa miradi mbalimbali ambayo imeibuliwa na jamii katika sekta za elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Katika kikao hicho Mhe Mbunge amesema fedha zitaelekezwa zaidi kwenye elimu, afya na barabara kwenye maeneo ambayo wananchi wamejitolea kuibua na kuichangia miradi husika mpaka kufikia ngazi mbalimbali iliyopo sasa ili iweze kukamilika na kutoa huduma.

Jumla ya shilingi milioni 47.87 zimepokelewa kwenye mfuko wa maendeleo ya jimbo na kupangiwa matumizi na kamati kwa kuzingatia miongozo inayosimamia mfuko husika.

PAMOJA TUNAWEZA
IMG-20210227-WA0025.jpg
 
Back
Top Bottom