Mfuko wa Hijja ni halali kikatiba?

Mfuko wa Hijja ni halali kikatiba?

jMali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
8,412
Reaction score
5,013
Nimeona kwenye taarifa ya habari ITV leo kuwa serikali ya Zanzibar inaanzisha mfuko wa hija kuwasaidia waislamu wasioweza kwenda hija, kutimiza ibada yao hii. Kwa wanaofahamu (msiofahamu tafadhali piteni pembeni),

1. Fedha za mfuko huu zinatoka kwenye kodi za wazanzibari wote au wazanzibari waislamu tu?

2. Ni halali kikatiba kwa serikali kuwa na mfuko wa uwezeshaji wa ibada ya dini moja? mfano, je? serikali ya zanzibar inaweza vile vile kuwezesha watu wa dini nyingine kutimiza ibada za dini zao?

Maswali haya ni kwa wanaofahamu tu, epukeni mihemuko ya kidini please kuna sheria ya cybercrime.

Nawasilisha.
 
Si Halali, Wala Haihitaji Sheria, Wanachofanya Wanatumia Rup Hall Ya Uchache Wa Wakristo Kuwakandamiza Wakristo, Kama Ni Hija Hata Wakristo Wanatakiwa Kwenda Hija Israel, Nani Anawalipia Hao Wakristo? Ukweli Lazima Usemwe.

Rup Hall ndio nini?
#hapa loophole tu
 
, hivi masuala ya fedha si ya muungano? maana yake kuna sehemu ya kodi ya wakristo kutoka tanganyika
 
mfuko wa hijja wa zanzibar, hii pia inaweza kuleta shida kwa sababu suala la fedha ni la muungano
 
Si Halali, Wala Haihitaji Sheria, Wanachofanya Wanatumia Rup Hall Ya Uchache Wa Wakristo Kuwakandamiza Wakristo, Kama Ni Hija Hata Wakristo Wanatakiwa Kwenda Hija Israel, Nani Anawalipia Hao Wakristo? Ukweli Lazima Usemwe.

Halafu ndo hawa hawa kila kukicha wanalalamika eti nchi inaongozwa na mfumo kristo,waislamu ni watu wa ajabu sana huwa hawaridhiki kwa kila jambo wanalotendewa,wao wanataka kila kitu serikalini wawe wao,yaani majeshi yote,bunge,wizara zote,wakuu wa mikoa na wilaya wooote wawe waislamu,kifupi wanataka nchi iwe ya kiislamu bila kufikiri kuwa kuna kundi kubwa la jamii ni wakristo,wengine wapagani,wakipata serikali ya kiislamu hata kama wengine mnaumia hapo ndo hamtawasikia wakisema ni mfumo kristo.
 
Achana na Zanzibar wewe fata yako. Kule ni 99% Muslims.

Hao 1% waliobaki kama utapenda unaweza kuwahamisha ili wasikatwe kodi yao ikaingia katika huo mfuko.
 
Achana na Zanzibar wewe fata yako. Kule ni 99% Muslims.

Hao 1% waliobaki kama utapenda unaweza kuwahamisha ili wasikatwe kodi yao ikaingia katika huo mfuko.

Una hoja kabisa- ndiyo maana tunataka Zanzibar yenye uhuru kamili.-Na kweli hayo masuala ya kisera na mfumo kwa vile yanafanyawa kwa nguvu ya wengi wape -inakuwa halina ubishi-muhimu lipitie mfumo wa Kidemokrasia-peleka Bungeni wawakilishi wa wapiga kura waamue.

Lakini pia kuna namna ya kuwasaidia wahanga wa tukio hili-kupitia mfuko wa Maafa-hawa ni watanzania wenzetu kwa hiyo hakuna suala la ohoooo walikwenda hija kwa hiari yao sijui na mambo mengine.

Kwa hiyo Serikali zote mbili zinatakiwa kuchukua hatua.

Achana na Zanzibar wewe fata yako. Kule ni 99% Muslims.

Hao 1% waliobaki kama utapenda unaweza kuwahamisha ili wasikatwe kodi yao ikaingia katika huo mfuko.

Nadhani kutakuwa na mfuko maalumu wa hayo mambo, sidhani kama ni P.a.y.e au zssf zetu, watachangishana misikitini na kwenye mihadhara yao
 
Nadhani kutakuwa na mfuko maalumu wa hayo mambo, sidhani kama ni P.a.y.e au zssf zetu, watachangishana misikitini na kwenye mihadhara yao

Dr shein ndie aliyesema katika baraza la idd hapo jana. Ingekuwa ni mfuko wa dini kama dini nisingekuwa na swali.
 
Dr. FaizaFoxy Una hoja kabisa, ndiyo maana tunataka Zanzibar yenye uhuru kamili. Na kweli hayo masuala ya kisera na mfumo kwa vile yanafanyawa kwa nguvu ya wengi wape -inakuwa halina ubishi-muhimu lipitie mfumo wa Kidemokrasia-peleka Bungeni wawakilishi wa wapiga kura waamue.

Lakini pia kuna namna ya kuwasaidia wahanga wa tukio hili-kupitia mfuko wa Maafa-hawa ni watanzania wenzetu kwa hiyo hakuna suala la ohoooo walikwenda hija kwa hiari yao sijui na mambo mengine.

Kwa hiyo Serikali zote mbili zinatakiwa kuchukua hatua.

Huyu faizafoxy udokta kaupata lini? anyway, swali langu linahusu uhalali wa kutumia fedha za wasio waislamu kwenye ibada za waislamu. Ni hapo tu. Hoja ya kwamba wasio waislamu ni wachache ni hatari. Hapo huwezi kutofautiana na kina sheikh ponda waliotaka tuhesabu sensa kwa misingi ya idadi ya wenye dini. Hatuwezi kuendesha nchi namna hiyo, kwamba mahala pakiwa na dini fulani wachache na fulani wengi basi wale wengi wawaburuze wale wachache.
 
Si halali kwanza Zanzibar wanapata kodi yao kutoka kwenye madanguro,pombe na nk halafu fedha hizo unampatia mtu akahijji kama si kufru ni nini.
 
Kwa zanzibar hakuna tatizo.ile ni nchi wanahaki na taratibu za kujitawala.
 
Its unconstitutional, wakiendelea itabidi tuwawekee vikwazo vya kiuchumi tu, maana hamna manna.
 
Mbona waislam huku Bara tunalipa pesa zetu zinaenda kwenye hospitali zinazomilikiwa na mashirika ya kikristo? Anyway kwa Zanzibar ni maamuzi yao after all zaidi ya 99 % ni Muslims haina shidaa.
 
Mbona waislam huku Bara tunalipa pesa zetu zinaenda kwenye hospitali zinazomilikiwa na mashirika ya kikristo? Anyway kwa Zanzibar ni maamuzi yao after all zaidi ya 99 % ni Muslims haina shidaa.

Hospitali sio ibada ni huduma ya kijamii, ni hospitali gani unaulizwa dini yako kama sharti la kupata matibabu? Mfano huo hauswihi.
Pili, ukiongelea idadi ya waumini huoni unavunja umoja wetu. Je utakubali kuwa sehemu iliyo na wakristo wengi basi hata waislamu walazimishwe kuchangia ujenzi wa makanisa kwa kodi maalum? au uenezaji wa injili/crusade kinguvu?
 
Mbona waislam huku Bara tunalipa pesa zetu zinaenda kwenye hospitali zinazomilikiwa na mashirika ya kikristo? Anyway kwa Zanzibar ni maamuzi yao after all zaidi ya 99 % ni Muslims haina shidaa.
Pia ukiangalia asilimia Kubwa ya wagonjwa kwenye hizo hospital ni waislam
 
In controversial statements, African pilgrims have been blamed for this indiscipline. Saudi-owned al-Arabiya TV reportedly quoted the head of the central Hajj committee, Prince Khaled al-Faisal, blaming the stampede on "some pilgrims with African nationalities".
wataleta majanga tena huko
 
Back
Top Bottom