Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote, Wazo zuri katika wakati sahihi

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Takwimu za Kidunia juu ya afya zinaonyesha takribani nusu ya watu Duniani hawapo kwenye mfumo wa Bima ya afya na hutumia zaidi ya asilimia 10 ya mapato yao katika matibabu.

Serikali kupitia Wizara ya afya imekuja na mfumo wa huduma ya Bima ya Afya kwa wote kuwasaidia wananchi kuweza kumudu gharama za matibabu.

Serikali umeufanyia mfuko marekebisho na kuwa mfuko wa Bima kwa wote uweze kuwanufaisha Wananchi wote kwanza kupata matibabu, Uhakika wa kupata dawa pamoja na kupata huduma ya ushauri wa kidaktari.

Katika mambo nimeyapenda kwenye mfumo huu wa Bima ya afya kwa wote ni namna Serikali imejaribu kuyajumuisha na kuyaongeza makundi ya wanufaika katika mfuko huu wa Bima ya afya kwa wote pamoja na kupunguza gharama za kuchangia kwa wanufaika.

Mwanzoni kifurushi cha mtu mmoja ilikuwa ni shilingi 192,000 kwa Mwaka na Pendekezo la sasa ni shilingi 84,000 tu. Bima ya familia ilikuwa shilingi milioni moja na Laki tano kwasasa imeshuka hadi shilingi 340,000 hii bei zinaleta maana ya Bima ya afya kwa wote.

Ufafanuzi wake ni kwamba kwa bei ya shilingi Laki 340,000 kwa watu sita inamaanisha gharama ya uchangiaji ni shilingi 931 kwa watu 6 Sawa na shilingi 155 kwa mtu 1 kwa siku. Hii ya mtu mmoja ya shilingi 84 elfu, ni Sawa na shilingi 230 kwa siku na sio mbaya.

Ni wazi unajaribu kuona Bima ya afya kwa wote ni dhamira njema ya kusaidia kila Mtanzania anapata matibabu kwa gharama nafuu. Uzuri Bima hii ya Afya kwa wote imelenga pia kuwasaidia hata wale wenye kipato duni kuwa ndani ya mfuko watafikiwa na kuunganishwa lengo la serikali ni kila mwananchi awe na Bima ya afya.

Bima kwa kwanza mengine baadaye. Afya ni muhimu.

Mwanzo mfuko wa Bima ya Afya upatikanaji wa huduma za matibabu kwa ulikuwa kwa watumishi wa Serikali, Umma, Binafsi, Wanafunzi na makundi mbalimbali ya watu ili kupata huduma za matibabu kupitia vituo vya Serikali, Madhehebu ya dini, Binafsi na Maduka ya Dawa ambayo yamesajiliwa na Mfuko.

Tofauti na sasa mfuko huu umelenga kuwanufaisha watu wote katika maeneo yote yatakayokuwa yamesajiliwa kwa ajili ya huduma.
 
Nakubaliana na wazo zuri la Bima ya afya kwa wote japo kazi kubwa sana inayohiyaji umakini wa hali ya juu unahitajika.

Ni lazima Bima hii igawanywe kwa makundi kulingana na mahitaji yao. Yaani kuwe na ile ya misingi ambayo uchangiaji wake umezingatia wananchi wa kipato cha chini na hii ya sasa iendelee.

Nia isiwe kuwashusha chini walio juu tayari badala yake ijaribu kuwasukuma juu walio juu.
Utekelezaji wa Sera Bima ya afya kwa wote usije ukavuruga mafanikio ambayo tayari yamepatikana kwa sasa.

Ikiwezekana uanzishwe Mfuko mwingine wa ziada kwa ajili ya kutekeleza Sera hii.
 
Hiyo gharama kwa watu wenye kipato cha chini ni kubwa sana na hiyo ni mwendelezo wa michango ktk Serikali ya CCM isiyo na kikomo,mapata yanayo kusanywa ktk nchi hii kwa nyanja mbalimbali ni mengi sana na mwananchi bila bima hiyo upo uwezekano mkubwa kupata matibabu bule kabisa. Hawa jamaa wameshindwa kuendesha hii nchi kabisa wanatakiwa kuachia madaraka aisee.
 
lengo la serikali ni kila mwananchi awe na Bima ya afya.

Bima kwa kwanza mengine baadaye. Afya ni muhimu.
Tofauti na sasa mfuko huu umelenga kuwanufaisha watu wote katika maeneo yote yatakayokuwa yamesajiliwa kwa ajili ya huduma.
Naunga mkono hoja!.
P
 
Back
Top Bottom