Mfanyakazi wa kike wa GGM ashikiliwa na Polisi kwa kumvisha Pete Mwanamke mwenzake

Hakuna mila kama hiyo usukumani, nadhani umedanganywa na ukadanganyika.
Hiyo tabia haina uhusiano wa kikabila bali ya kishetani na inaweza kumpata mtu wa kabila lolote kama hana Kristo Yesu ndani yake, wahusika wanaongozwa na mapepo.

Msome vizuri nafikiri anasema wanaoa ili wazaliwe watoto

 
Huh! Polisi bana, upuuzi wanajua kweli kuufuatilia, kazi za msingi zero kabisa!!
Hapana ni kwamba Tanzania hairuhusu tabia za Ushoga na Usagaji.
Kama isivyo rubusa kuvuta bangi.
Mtu anayejihusisha na masuala hayo ni lazima akamatwe na ahojiwe, ni kwanini anafanya mambo yasiyo ya maadili ya Nchi.
Hapo wote wanamakosa na watakamatwa wote ili watoe maelezo kwa kukiuka miiko ya Utamaduni wetu tuliourithi kwa mababu zetu.
Kama mtu anapenda hayo mambo ni vizuri aombe uraia katika nchi zinazoruhisu hizo tabia, ili akawe huru kuyafanya.
 
Kwanini hujajiridhisha kwa kufanya karisechi kidogo kabla ya kubisha tu, bila hoja na mihemuko yako ya kidini, ya dini ambazo hata inawezekana huijui kweli yake, na maarifa yanawezekana pia hujayaongeza Mkuu?

Mi niko huku Usukumani, ninachokiongea sio cha kusimuliwa, bali nakishuhudia daily, ambacho labda hujanielewa ni kwamba, hawa wanawake wanaooa huku, dhumuni linakuwa kumpatia watoto, mwanamke tajiri ambaye hana uwezo wa kuzaa, au kujiongezea kipato kupitia watoto alomzalia, na kwamba hawaingiliani, nimesema hapo juu, kwamba muoaji humchagua mwanaume yeyote yule amzalishe mke wake, na watoto watakaozaliwa ni wa yule mwanamke aliyeoa, na mume wa muolewaji ni mwanamke mwenzake akimiliki kabisa kama mke.
Hiyo sio mila ya wasukuma, rudi kafanye research upya.......ni mila ya kabila moja huku kanda ya ziwa lkn si wasukuma
 
Kama sikosei, Milembe ni jina la kisukuma, kama ni sawa, basi Watakuwa wamejichanganya, wasukuma wanawake wana mila yao inayoruhusu kuoa mwanamke, Halafu anamkabidhi yeyote ampendae, anamzalia watoto, haswa kama atakuwa hana uzazi yeye.
Acha kupotosha ndugu, mimi ni msukuma hatuna mila kama hiyo. Tabia hizi zipo sana hasa migodini. Wakati nafanya kazi mgodini walikuwepo maboss wengi wa Kitanzania magays na wasagaji. Hata majina yao yanajulikana na katika hali ya kushangaza wengi walipewa vyumba kuishi ndani ya mgodi
 
Mungu tunusuru Mwisho wa dunia ndo huu!
Hawa ni wasagaji waliovishana Pete huko Mwanza



Polisi Wamtia Mbaroni mwanamke Aliyeonekana kwenye Video Akimvisha mwenzake pete ya uchumba Geita

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtumishi wa mgodi wa GGM, Milembe Suleiman anayetuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

Mfanyakazi huyo ambaye ni ofisa ugavi kitengo cha manunuzi anashikiliwa baada ya ‘video’ inayomwonyesha akimvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Video hiyo ambayo imezua mijadala hasa ikizingatia kwamba iko kinyume cha utamaduni wa Kitanzania na Serikali ambayo imekuwa ikikemea na kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsi moja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wanamshikilia kuwa uchunguzi kwa kuwa nchi hairuhusu mambo hayo.

Ofisa Habari wa GGM, Dili Tenga amesema hayo ni masuala binafsi ya mfanyakazi hivyo wao kama mgodi hawawezi kuyazungumzia lakini wanaviachia vyombo vya dola viendelee na uchunguzi wake.
 
kwa kuwa anaitwa Milembe ni wazi alitakiwa apelekwe kwa wenzake kule dodoma - Milembe
 
Kama sikosei, Milembe ni jina la kisukuma, kama ni sawa, basi Watakuwa wamejichanganya, wasukuma wanawake wana mila yao inayoruhusu kuoa mwanamke, Halafu anamkabidhi yeyote ampendae, anamzalia watoto, haswa kama atakuwa hana uzazi yeye.

Hilo ulilosema linafanya kazi huko Mkoa wa Mara.
 
Back
Top Bottom