Mfanyakazi wa kike wa GGM ashikiliwa na Polisi kwa kumvisha Pete Mwanamke mwenzake

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,895
25,945
Amani iwe nanyi wapendwa katika bwana,

Mwanamke mmoja anayekwenda kwa jina Milembe ambaye ni Afisa wa mgodi wa Geita anayehusika katika kitengo cha manunuzi amekamatwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumuoa mwana mke mwenzake had kumvisha pete ya uchumba.

Jeshi la polisi linamshilikia mwanamke huyo kwa kosa la kumuoa mwanamke mwenzie na kumuvisha pete, jeshi la polisi limesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na nchi hairuhusu mambo hayo.

LONDON BABY

======================================

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtumishi wa mgodi wa GGM, Milembe Suleiman anayetuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

Mfanyakazi huyo ambaye ni Afisa Ugavi kitengo cha manunuzi anashikiliwa baada ya ‘video’ inayomwonyesha akimvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Video hiyo ambayo imezua mijadala hasa ikizingatia kwamba iko kinyume cha utamaduni wa Kitanzania na Serikali ambayo imekuwa ikikemea na kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsi moja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wanamshikilia kwa uchunguzi kwa kuwa nchi hairuhusu mambo hayo.

Ofisa Habari wa GGM, Dili Tenga amesema hayo ni masuala binafsi ya mfanyakazi hivyo wao kama mgodi hawawezi kuyazungumzia lakini wanaviachia vyombo vya dola viendelee na uchunguzi wake.

Mwananchi
 
Hivi inakuwaje mwanamke akubali kuolewa na mwanamke mwenzake wakati kuna midume kibao mingine inahitaji wake wawili hadi wanne?
Kwa nini usijipendekeze kwa mwanamme yeyote tu.
Vivyo hivyo kwa wanaume wanaooana, inakuwaje wakati kuna wana wa kike wazuri wengi tu katuumbia! yaani haiingii akilini.

Tumwombe Mungu sana ili anusuru kizazi hiki na tabia hizi ambazo hatimaye huleta laana katika jamii na nchi kwa ujumla.
 
Huwezi amini nilipoiona hiyo clip niliona kichefuchefu
Kwanza kulikuwa na watu wengi tena wanashanglia as if ni send off. Kwanza wale watu walionyesha kukubali kile kitendo cha laana. Jamani mkono wa sheria uonekane na uwe mkali iwe fundisho
 
Kama sikosei, Milembe ni jina la kisukuma, kama ni sawa, basi Watakuwa wamejichanganya, wasukuma wanawake wana mila yao inayoruhusu kuoa mwanamke, Halafu anamkabidhi yeyote ampendae, anamzalia watoto, haswa kama atakuwa hana uzazi yeye.
 
Back
Top Bottom