sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,000
Wakuu salaam....
Husikeni na kichwa Cha mada.
Mwaka 2010 niliajiriwa pamoja na rafiki zangu6 kwenye taasisi 1 ya Serikali. Katika kuturahisishia mazingira ya kazi tuliambiwa Kuna nyumba za wafanyakazi ambapo kwa wakati huo kulikuwa na nafasi ya kukaa wafanyakazi wa3 Kati ya wale6 tulioajiriwa.
Baada ya kujadiliana nani wakae na nani wakapange mtaani, nikabahatika kuwa miongoni mwa wale wa3 waliopata nafasi pale kwenye zile nyumba za taasisi.
Baada ya miaka mi5 wale wenzetu waliopanga nyumba kila mmoja akawa amejenga na kuhamia kwake. Sisi tuliobaki Kwenye nyumba za bure aliyejitahidi sana alikuwa na kiwanja tu.
Siku moja rafiki yangu Kati ya wale waliojenga akanambia "Sepema naomba utoke kwenye hiyo nyumba ya bure ukapange nyumba".
Alinieleza faida nyingi ambapo mwaka 2016 nilikubali kuanza maisha ya kupanga nyumba. Nikawaacha wenzangu wawili pale wasijue nini kimenipata .
Mwaka 2019 nikafanikiwa kujenga nyumba kwenye kiwanja changu nilichokua nimekinunua wakati nipo kota.
Kilichonifanya nijenge ni zile hasira za kuishi kwa masharti kwenye nyumba za watu. Hasira zenye faida.
Wenzangu bado wapo na hawana mpango wa kujenga kwa Sasa.
Nimechunguza wafanyakazi wenzetu wengi tuliowakuta kwenye zile nyumba hawajajenga bado... kwanini hawajajenga ilhali wangine wana zaidi ya miaka 20 pale? Jibu ni moja, zile nyumba za bure wanazoishi hazina usumbufu wowote. Umeme na maji vipo free, wameridhika!
Mwisho, tuishi kwenye hizo nyumba za bure Ila tukumbuke Kuna kesho.
Tafakari, chukua hatua!