Mfanyabiashara wa Mabasi ya KIMOTCO alia na Trafiki kwa Rushwa Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mfanyabiashara na Mmiliki wa Mabasi ya kusafirisha abiria mikoani kutoka kampuni ya KIMOTCO ,Benedict Mberesero,amewalalamikia askari wa usalama barabarani katika Jiji la Arusha,kwa vitendo vya Rushwa iliyokithiri akidai wamegeuka mamlaka ya mapato TRA.

Akiongea katika kikao cha wadau wa usafirishaji jijini Arusha,mbele ya Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Nchini,(SACP)Futunatus Silima, alimshutumu Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha ,RTO Joseph Bukombe kuwa amekuwa kinara kwa kuongoza kikosi cha askari kukusanya Rushwa kutoka kwa wasafirishaji .

Amedai kuwa vibanda vya ukaguzi wa mabasi katika eneo la kituo kikuu cha mabasi jijini hapa ,vimegeuka vibanda vya kukusanya Rushwa kwa mabasi mbalimbali yanayoelekea mikoani na fedha hizo huwasilishwa kwa wakubwa .

"Napenda niseme ya Moyoni naona watu wamekuwa waoga kusema ,ukweli ni kwamba suala la Rushwa ni kubwa kwa Trafiki hapa Arusha naomba uchunguze mwenyewe ujionee" Alisema Ben

Aliongeza kuwa hivi karibuni alibambikiwa kesi ya matumizi mabaya ya Silaha ambapo alipigwa na askari wa usalama barabarani na kutupwa selo kituo cha Polisi kwa makosa aliyodai ni ya usalama barabarani.

"Namshukuru RPC alilishughulikia suala langu na bila yeye bila shaka ningekuwa nimefungwa kwa kubambikiwa kesi za uongo kwani si kweli kwamba Mimi nilitishia askari kwa silaha" Alisema .

Alimtuhumu RTO Bukombe kutoa ushirikiano pindi anapopigiwa Simu kwa nia ya kuomba msaada.

Akijibu hoja hizo ,RTO Bukombe Alisema tuhuma zilizoelekezwa kwake hazina ukweli Bali ni chiki zilizolenga kumchafua.

Alisema mabasi ya Kimotco yanaongoza kwa kuvunja sheria za usalama barabarani na pindi anapochukua hatua inaonekana kwamba RTO Bukombe mbaya na kuanza kumchafua kwa kusema askari anawatuma kukusanya Rushwa.

Ends.....

IMG_20190703_145224.jpeg
IMG_20190703_152509.jpeg
 
Arusha Trafik wamekuwa keroo, Arusha inaongoza kwa usumbufu wa Trafik.

trafiki arusha punguzeni rushwa na kubambikiza makosa. au waombeni wakubwa wenu wawapunguzie kiwango cha MALENGO ya kukusanya kwa siku.
 
Mfanyabiashara na Mmiliki wa Mabasi ya kusafirisha abiria mikoani kutoka kampuni ya KIMOTCO ,Benedict Mberesero,amewalalamikia askari wa usalama barabarani katika Jiji la Arusha,kwa vitendo vya Rushwa iliyokithiri akidai wamegeuka mamlaka ya mapato TRA.

Akiongea katika kikao cha wadau wa usafirishaji jijini Arusha,mbele ya Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Nchini,(SACP)Futunatus Silima, alimshutumu Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha ,RTO Joseph Bukombe kuwa amekuwa kinara kwa kuongoza kikosi cha askari kukusanya Rushwa kutoka kwa wasafirishaji .

Amedai kuwa vibanda vya ukaguzi wa mabasi katika eneo la kituo kikuu cha mabasi jijini hapa ,vimegeuka vibanda vya kukusanya Rushwa kwa mabasi mbalimbali yanayoelekea mikoani na fedha hizo huwasilishwa kwa wakubwa .

"Napenda niseme ya Moyoni naona watu wamekuwa waoga kusema ,ukweli ni kwamba suala la Rushwa ni kubwa kwa Trafiki hapa Arusha naomba uchunguze mwenyewe ujionee" Alisema Ben

Aliongeza kuwa hivi karibuni alibambikiwa kesi ya matumizi mabaya ya Silaha ambapo alipigwa na askari wa usalama barabarani na kutupwa selo kituo cha Polisi kwa makosa aliyodai ni ya usalama barabarani.

"Namshukuru RPC alilishughulikia suala langu na bila yeye bila shaka ningekuwa nimefungwa kwa kubambikiwa kesi za uongo kwani si kweli kwamba Mimi nilitishia askari kwa silaha" Alisema .

Alimtuhumu RTO Bukombe kutoa ushirikiano pindi anapopigiwa Simu kwa nia ya kuomba msaada.

Akijibu hoja hizo ,RTO Bukombe Alisema tuhuma zilizoelekezwa kwake hazina ukweli Bali ni chiki zilizolenga kumchafua.

Alisema mabasi ya Kimotco yanaongoza kwa kuvunja sheria za usalama barabarani na pindi anapochukua hatua inaonekana kwamba RTO Bukombe mbaya na kuanza kumchafua kwa kusema askari anawatuma kukusanya Rushwa.

Ends.....

View attachment 1145508View attachment 1145509
Mabasi yake ni mabovu mabovu bila kuyaficha
 
Kwa nini RTO wa Arusha asibadilishiwe kitengo ili haya malalmiko yakome. Ukisemwa sana na watu ujue kuna ukweli ndani yake.
 
Back
Top Bottom