Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
8,652
Reaction score
2,642
Mfanyabiashara maarufu wa madini Mererani na Mmiliki wa SG RESORT ya Arusha, Bw. Erasto Msuya Amepigwa risasi ndani ya gari lake na kufa papo hapo mida hii akitokea Mererani kuelekea Moshi.

Yasemekana wauaji wamekimbia na briefcase lake.
erasto-maiti.jpg

PICHA: Mwili wa Erasto Msuya ukiwa umelala chini baada ya kushambuliwa kwa risasi na kuuawa​

----
Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri,

aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli ameuawa kinyama sana, alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomangombe.

Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomangombe, mji huo ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na Mererani.

Habari za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake walikuwa katika pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo, walimpora kibegi ambacho haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya fedha.

Kulingana na vyanzo vya habari, mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa Bomangombe na makutano ya Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai kwenda Arusha.

RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa saa 7:00 mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji wa Bomangombe na makutano ya barabara ya Kia.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eransto alikuwa akitokea Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la Mjohoroni alichepuka na kwenda meta 300 nje ya barabara, alisema.

Kamanda Boaz alisema alipofika eneo hilo, alikutana na vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani ya gari kwa lengo la kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.

Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye gari lake na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye gari la Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi.

vogue-erasto.jpg

Gari la Erasto Msuya likiwa eneo la tukio la mauaji​


VIDEO: Mauaji ya Erasto Msuya, Aneth Msuya na hukumu ya Miriam Mrita
Soma Sakata la Kifo cha Bilionea Msuya


MWENENDO WA KESI MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA

Septemba 17, 2013 watuhumiwa wakiwa kwa mganga wakijizindika wasikamatwe

Soma Waliomua Bilionea Erasto Msuya wakutwa kwa sangoma

Juni 12, 2014, Mahakama yaelezwa jinsi Erasto Msuya alivyouawa
Soma Mahakama yaelezwa bilionea wa madini Erasto Msuya alivyouawa

Oktoba 27, 2017, Shahidi adai kuahidiwa Tsh 17m kutekeleza mauaji
Soma Shahidi aelezea walivyoahidiwa kulipwa Sh 17 milioni kila mmoja kumuua bilionea Msuya

Mei 11, 2018, Shahidi alidai kuwa Mfanyabiasha wa Madini, Chusa ndiye alipanga mauaji
Soma SHAHIDI: Chusa alipanga mauaji ya Bilionea Msuya

Mei 14, 2018 Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu washtakiwa 6
- Kesi ya bilionea Msuya: Sita wana kesi ya kujibu huku mmoja akiachiwa huru

Julai 23, 2018 washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa
soma Washtakiwa watano mauaji ya bilionea Msuya wahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kunyongwa hadi kufa

Agosti 18, 2018 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa wakata rufani
Soma Waliohukumiwa kwa mauaji ya Bilionea Msuya wapinga kunyongwa

Jaji aliyetoa hukumu atishiwa kifo
Soma Jaji aliyesikiliza kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya na kutoa hukumu ya kifo atishiwa kuuawa

Pia soma Aliyeachiwa kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya aeleza mazito


MAUJI YA ANETH MSUYA NA MWENENDO WA KESI YA MAUAJI YAKE

Aneth Msuya aliuawa kinyama akiwa nyumbani kwake Kibada
Soma Aneth Msuya ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya auawa kinyama Dar

AUG 23, 2016 Mirima Mrita alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauji ya Aneth Msuya
Soma Mjane wa Erasto Msuya apandishwa Kizimbani Kisutu

SEPT 18, 2023 Mahakama ilimkuta Miriam Mrita na kesi ya kujibu Mauji ya Aneth Msuya
Soma Dar: Mke wa Bilionea Msuya akutwa na Kesi ya Kujibu mauaji ya wifi yake

FEB 23, 2024 Mahakama Kuu ilimuachia huru Miriam Mrita
Soma Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia mauaji ya Aneth Msuya


UGOMVI WA MALI ZILIZOACHA NA ERASTO MSUYA
Familia ilishindwa kuelewana suala la mirathi na kupelekea Serikali kuingilia kati
Soma Mali za Marehemu Bilionea Erasto Msuya, ndugu ngumi mkononi

Mama Mzazi wa Erasto Msuya adai kuwa mjane alikomba mali kabla ya mazishi
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Wadau wahoji uhalali wa ndugu wa Miriam Mrita kusimamia mali za Erasto Msuya
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Mama Mzazi wa Msuya akubali kuondoa shauri Mahakamani ili kulimaliza kifamilia
soma Mama wa Bilionea Msuya akubali kuondoa kesi kwa Muda Mahakamani

Mahakama yataka pande mbili za familia kukaa meza moja na kuondoa tofauti
Soma Ugomvi wa Mali za Marehemu Bilionea Msuya, Mahakama yanena

2021, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumuondoa Miriam Mrita kuwa msimamizi wa Mali
Soma Mahakama yamuengua mjane wa Bilionea Erasto Msuya kusimamia Mirathi ya Mumewe
 
ngoja kwanza.. Erasto huyu mwenye SG resort, pale sakina????
 
Bilionea wa madini ya Tanzanite Erasto ameuwawa kwa kupigwa risasi.Habari zaidi zitafuata baadae.
 
ngoja kwanza.. Erasto huyu mwenye SG resort, pale sakina????

Ndiyo huyo jamaa, nikweli amefariki kwa kupigwa risasi 8 kwa mujibu wa jamaa aliyeko karibu na eneo la tukio. Na inasemekana hawajachukua kitu chochote kwenye gari lake.
 
ngoja kwanza.. Erasto huyu mwenye SG resort, pale sakina????

Ndio yeye, alikuwa anatoka Mererani alipofika eneo liitwalo Majengo ndipo akavamiwa na kupigwa risasi nane akafia palepale. Alikuwa ametoka kununua mzigo mkubwa sana (madini) wamechukua. Jeshi la polisi mikoa ya Kilimanjaro na Arusha linawasaka watuhumiwa
 
Kudhulumu pesa sio sawa sawa na kutoa roho ya mtu ndugu zangu....
 
Duh...This is very sad

Mabilionea wa kanda ya kaskazini wanapukutika daily aisee. Nakumbuka hata Bishanga alipokuja hapa Arusha alifikia pale kwenye lodge yake SG Resort. Pia ndiye mweny Mezzaluna Hotel.
 
Last edited by a moderator:
Watuhumiwa wa ulimboka tuliwapata? Wa mabomu arusha?kanisa kurushiwa bomu,watuhumiwa walipatikana? Madawa ya kulevya ya akina masogange watuhumiwa wamepatikana?uchunguzi wa ndege iliyomuua bob sambeke vp ilishatoka?chadema walishatoa mkanda wa mauaji?
Samahani nilikuwa nje ya nchi kidogo sasa nataka kujua kinachoendelea nchini....
 
sad news kwakweli..hoteli itakufa ile.. damn the guy alikua anavaa cheni la gold nene saana dah.. rest in peace erasto.. he was a good guy
 
Back
Top Bottom