Mfanyabiashara Hanspaul Arusha,Afikishwa Mahakamani

Mfanyabiashara Hanspaul Arusha,Afikishwa Mahakamani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Mfanyabiashara Maarufu jijini Arusha,Kamaljit Hanspaul (58)na wengine watatu wenye uraia wa nje wamefikishwa mahakamani katika mahakama ya hakimu mkazi ,Arusha kwa makosa ya kuajiri na kuajiriwa kinyume cha sheria za nchi.


Watuhumiwa wengine ni Kumar Vemula (27), raia wa nchini India,Vinoth Krishanth (29) raia wa Sri Lankan na Raiph Leopold
Hruscka (54) ambaye ni raia wa Ujerumani.


Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka hayo na wakili wa serikali Khalili Nuda mbele ya
hakimu mkazi mfawidhi Niku Mwakatobe na kuieleza mahakama kuwa
mtuhumiwa wa kwanza Hanspaul ,Novemba 12 mwaka aliajiri raia hao wa
kigeni bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini huku akijua
kuwa ni kinyume cha sheria.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo watuhumiwa wote kwa pamoja walikiri kutenda makosa ,hata hivyo kesi yao iliahirishwa kwa muda hadi alhamis ijayo Desemba 6,mwaka huu ambapo mahakamani itatoa uamuzi.

Hata hivyo washtakiwa hao wamenusurika kwenda mahabusu gerezani baada ya kutokuwa na wadhamini mahakamani wakiamini kukiri kwao mahakamani Wang dries hatiani na kuwatoza faini.


Hakimu alidai dhamana ipo wazi kwa wadhamini wawili kila mmoja wenye vitambulisho pamoja na fedha kiasi cha sh milioni tano.


Baada ya kuwaeleza watuhumiwa masharti hayo wakili wa utetezialiyefahamika kwa nina moja la Ngereka aliieleza mahakama hiyo kuwa wateja wake hawana wadhamini na kuomba muda kwa ajili ya kuwatafutia
wadhamini hao vya Idara ya Kazi.


Awali Afisa kazi Mkoa wa Arusha Wilifred Mdumi alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakifanya kazi katika kampuni tatu
ambazo zote zinamilikiwa na Mfanyabiashara huyo Hans Paul.


Mfanyabiashara huyo Hans Paul alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi
wa nyumba 31 za Polisi zilizoungua mwaka jana 2017 na amekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo katika mkoa wa Arusha.

Ends........

IMG_20181204_131933.jpeg
 
Wahindi ni vinara wa kuvunja sheria. Wanaajiri wenzao utafirikiri hamna wafanyakazi hapa Tz.
 
Back
Top Bottom