Mfanyabiashara Arusha kizimbani kwa kunajisi mwanawe

Mfanyabiashara Arusha kizimbani kwa kunajisi mwanawe

Dunia haiko salama tena. Watoto wanapata shida iwe kutoka kwa mama zao au baba zao au house helpers awe houseboy au housegirl na hata wapita njia. Watoto wetu wako kwenye maisha hatarishi sana. wanadamu tumekuwa katili kupita maelezo.☹️☹️☹️
 
Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na mkazi wa kata ya Sakina, Alistalius Silayo (45) amefikishwa mahakamani akituhumiwa kumnajisi mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11.

Akisomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Pennina Joackim ilidai kuwa mfanyabiashara huyo alitenda kosa hilo katika vipindi tofauti kati ya Januari na Septemba mwaka huu.

Mwendesha Mashitaka alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Patricia Kisinda kuwa mshtakiwa alikuwa akifanya kosa hilo mara kwa mara katika miezi hiyo eneo la Sakina kwa Iddy yaliko makazi yake.

Alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha Kifungu cha 158 Kifungu kidogo cha 1(a) cha Sheria na Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 na kufanyiwa marekebisho 2002.

Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana shitaka hilo na hakimu alisema dhamana iko wazi ya wadhamini wawili wanaotambulika kisheria.

Mbali ya hilo, pia wadhamini hao lazima wawe na mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi Sh milioni 10 na wadhamini hawaruhusiwi kutoka nje ya Mkoa wa Arusha bila ya kibali cha Mahakama.

Hata hivyo, wadhamini hao walishindwa kukamilisha taratibu za dhamana mahakamani hapo na hakimu aliwapa muda kukamilisha taratibu katika saa za kazi na kuamuru mshtakiwa kurudishwa rumande hadi taratibu zitakapokamilika.

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 10, mwaka huu kwani Mwanasheria wa Serikali alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
hapo wamemuonea tu mtu kala chake mwenyewe shida ikowapi angekula cha mtu je
 
Kwayanayo tendeka sinabudi kuamini dunia imeshakwisha kama ni movie basi ishatoa maandishi
 
Huyo boya lazma ni kutoka moshi pande flani ambao bila kuloga hela hapati,imani za kishirikina zinazidi kupamba moto
 
Bora kuwa na pesa ya kawaida na mnafuraha na familia yako kuliko kuwa na pesa za masharti sasa huyo binti hicho kitu alichofanyiwa hakita futika akilini mwake atakuwa na chuki sana na huyo mzazi wake!

-Nyerere-
 
Back
Top Bottom