Jana nikiwa Runzewe nikitokea Mwanza, nilipaki gari na kwenda kula kwa jamaa zangu kando ya barabara. Jamaa yangu mmoja maarufu sana Runzewe akaniambia
'Mheshimiwa, unajua kilichotokea jana? Pale ambapo huwa unafikia (Zambabwe Guest) yule jamaa mmiliki wake kulitokea ugomvi na askari police na jamaa kauwawa'.
Nikashtuka sana, maana jamaa alikuwa ni mfanyabiashara hususan akinunua madini ya vijana wanayokwapua toka mgodi wa African Barrick Gold (Tulawaka), na kiukweli alikuwa na chenji nzuri tu.
Kwamba ugomvi ulitokea kituo cha polioce Runzewe na kweli huyo mfanyabiashara alikuwa kalewa na alimfyatulia risasi police.
Baada ya kumfyatulia risasi police, jamaa akaondoka kurudi kwake na kweli alifaulu kufika kwake. Police walifaulu kumfata kwake na wakamchukua kwenda naye mpaka Ushirombo ambapo ndipo makao makuu ya wilaya yapo na hospitali ya wilaya ilipo. Lengo likiwa aambatane na majeruhi askari ili watoe maelezo kwa intelijensia kwa kilichojiri.
Habari za kuaminika kabisa jamaa hakufia nyumbani kwake kama inavyodaiwa, aliwashwa naye risasi Ushirombo na hao hao wana-intelijensia. Vijiwe vyote pale Runzewe wanalijua hilo, na marehemu ikimbukwe alikuwa kawabeba vijana wengi wa Runzewe kuwapa ajira za kutafuta dhahabu.
Usiku uleule police walipomchukua nyumbani kwake marehemu akiwa hai, waliondoka na furushi 2 za begi zilizojaa fedha (noti) ambazo marehemu hukaa nazo kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu. Marehemu alikuwa akipendelea zaidi kununulia dhahabu maeneo ya 'mwembeni' na 'mavota', hivi ni vijiji jirani kabisa ya mgodi wa Tulawaka.
Kweli alilewa, ila kauwawa akiwa Ushirombo. Ila kwa haraka sana usiku uleule police walitangaza jamaa kajiua akiwa nyumbani kwake, wananchi wakajiuliza 'mbona wamekuwepo nyumbani kwake na hawajaona maiti kubebwa kupelekwa Hospital kuhifadhiwa?'. Ndipo ufatiliaji ulianza na wananchi kuwasha pikipiki kwenda Ushirombo kushuhudia, waliyoyakuta huko...mh!!!
Source: Wananchi wa Runzewe center, hususan kundi kubwa la vijana linalomsikitia marehemu kuuwawa.