Mfanyabiashara ajipiga risasi mjini Moshi

mnyinda

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
277
0
Mfanyabiashara maarufu mjini Moshi leo asubuhi amejiua kwa kujipiga risasi.Mfanyabiashara huyo ajulikanae kwa jina AGUSTIN MALYA (kipumbu)amejiua na sababu za kifo chake bado hazijajulikana.

Mfanyabiashara Moshi ajimaliza kwa risasi

MWEZI mmoja baada ya mfanyabiashara wa Arusha, Timoth Mroki (36) kujiua kwa kujipiga risasi, mfanyabiashara mwingine maarufu wa Moshi, Augustino Mallya, naye amejiua kwa kujipiga risasi akiwa nyumbani kwake eneo la Karanga katika Manispaa ya Moshi.

Mfanyabiashara huyo alikuwa akijishughulisha na biashara za maduka ya bidhaa za jumla na nyumba za kupangisha katika eneo la Karanga. Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela.

Kamwela alisema lilitokea juzi majira ya saa 11 alfajiri na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa uchunguzi zaidi.

Kamwela alisema mke wa marehemu, aliyetajwa kwa jina la Elizabeth Mallya, ndiye aliyebaini tukio la mumewe kujiua kwa kujipiga risasi moja kifuani akiwa sebuleni kwake, ambapo alitoa taarifa polisi.

Shemeji wa marehemu huyo, Peter Masawe alidai shemeji yake alijiua kwa kutumia bastola aina ya Browing yenye namba 96682, iliyokuwa na risasi nane na inadaiwa alikuwa akiimiliki kihalali.

Masawe alidai tukio hilo lilitokea siku moja kabla ya mfanyabiashara huyo hajatakiwa kusafiri kesho kwenda India, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya tumbo kwa muda mrefu.
"Kwa taarifa za familia hii, tunafahamu kwamba Malya hakuwa na ugomvi na mtu yeyote akiwamo mkewe na wanawe wanne," alisema.

Alisema katika tukio hilo la kujipiga risasi, Mallya alifariki papo hapo akiwa nyumbani kwake na hakuna taarifa zaidi zilizotolewa juu ya chanzo cha tukio hilo.

Hata hivyo, Masawe alisema Mallya mara kadhaa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo, ambalo hujaa baada ya kumaliza kula.

Masawe alisema mipango ilikuwa imekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kufika siku ya safari.

Tukio hilo linakuja mwezi mmoja na wiki moja tangu mfanyabiashara mwingine wa Arusha, anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara mikoa ya Arusha na Manyara, Mroki kujiua jijini Arusha.
CHANZO: Habari Leo(11/12/2014)
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Kaskazini haswa Arusha na Kilimanjaro baadhi kama si wengi wanahitaji msaada wa kisaikolojia
 

BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,874
1,250
Pole kwa ndugu! Jamaa kajihukumu mwenyewe kwenda Jehanum moto kama Yuda Iskariote aliyejiua baada kumsaliti Yesu Kristo.
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,525
2,000
Jamani kaskazini kunani......???.
Mbona mabilionea wanazidi kuisha...........
Wengine wanafia vifuani mwa wadada wengine wanauwawa ,wengine wanajipiga risasi......

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Jamani kaskazini kunani......???.
Mbona mabilionea wanazidi kuisha...........
Wengine wanafia vifuani mwa wadada wengine wanauwawa ,wengine wanajipiga risasi......

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Na wengine wanazaliwa lol.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom