Mfalme Zumaridi, Mama huyu ni nani na kwanini Serikali imemuacha tu?

mubindi

Member
Jun 25, 2017
89
98
Jamani nawasalimia wote kwa kila mtu Na imani yake.

Kule jijini Mwanza kumeibuka mwanamama mmoja anajiita Mfalme Zumaridi na ana kanisa au sijui niseme nini, maeneo ya Nyegezi.

Yeye haamini ktk Biblia au Quran yaani ni shidaa. Na Ana watu wengi kinoma Na wafuasi wake wanamsujudu na mpaka wengine wamekua Na alama Kama ya sigda.

Ukifuatilia clips zake utashangaa ya ni upinga Kristo tupu. Wakazi wa Mwanza na waTz wote tuwe makini na huyu mtu.



Pia tazama hii:



SOMA PIA: Mchungaji 'Mfalme Zumaridi' adai kuwasiliana na Kanumba, Mama yake azungumza - JamiiForums
 
Maswala mengi ya imani watu huwa kama vichaa hata katika hizi dini zinazojulikana!

Jiulize tu kwa nini katika dini moja imani sio moja! ukikaa pembeni unaitwa muasi ukijikita ni imani hii napo wengine watakuambia umepotea.

Natamani Mungu angemtuma mtume mwingine wa mwisho!
 
Kwa mara ya kwanza nimeona video yake moja YouTube leo ndio nika search kujua zaidi, Mungu awahurumie sana maana hata hatumii akili nyingi kuwapotosha, na yeye anajiita mungu/mfalme etc.

Halafu waumini wake wanatoa ushuhuda na kukiri kuwa wamesema uongo!! ( eg niliitwa nikawaambia sina nauli na nauli nilikuwa nayo kwa vile nilikua sitaki kwenda!! Mwingine akasema nilisema mganga ndio aliyeniponya lakini nilikuja kwa mfalme zumaridi akaniponya) Biblia inasema shetani ni baba wa uongo!

That woman is a witch in a high different level, if she do not change she will have a very special place in hell.
 
Wadau , jana katika kupoteza poteza muda na TV ..

Nikakutana na mwanamama mrembo anajiita mfalme Zumaridi wa kule Mwanza....kwa kweli nimeshangaa mpaka basi....yeye anasema anaponya kwa kupitia maono ya Mungu...

Halafu tofauti yake na watumishi wengine ni kwamba yeye wote anaowahudumia wanakuwa na vielelezo toka hospitali nk kwamba walishapimwa na wakagundulika na ugonjwa fulani...yeye ndiye anauondoa huo ugonjwa....
1550295043219.png

Jana kuna mgonjwa mmoja alitoa ushushuda wa ajabu kwamba amepona magonjwa ya ajabu ajabu sababu maono yalionyesha alikuwa amepindikizwa mafigo /maini ya wanyama , macho pia ya wanyama ndiyo maana akawa ana matatizo yasiyo tibika hospitali zooote na kwa waganga , watumishi wa Mungu woote ila hapo kwa mfalme Zumaridi amepona kabisa....

Sasa najiuliza inakuwaje mwanamke akawa na cheo cha ufalme? halafu anatumia nguvu za aina gani huyu mama? Je hili jina la Zumaridi limetokea wapi?Hii ni mara yangu ya kwanza kumuona huyu mama..

Je huko Mwanza aliko ananguvu kiasi gani?
 
Duh.....Mpaka sasa nimeshindwa kujua yupi ni Nabii wa ukweli katgijka hawa tunaowaona
 
Du ndg yangu umenikumbusha kisa kimoja ,kuna shemeji yangu alikuwa anasari kanisani kwake basi siku moja akaja nyumbani kwangu huyo shemeji akamchukua binti yangu mwenye miaka 16 akawa anaenda naye kanisani kwa zumaridi weee wiki mbili tu binti akawa anaanguka et mapepo ya zumaridi ndg zangu nilipiga marufuku mara moja kwenda kwenye kanisa lake ,toka siku hiyo binti hajawahi kuanguka kisa mapepo,namuogopa sana yule mama,
 
Back
Top Bottom