Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 425
- 1,027
Kwa siasa za sasa hivi jinsi zilivyo za kusifu na kuabudu, zinafanana na hadithi fulani ya Kidenmark inayozungumzia mfalme mmoja aliyependa sana kusifiwa na watu wake, huku akishindwa kujua kuwa sifa zile zilikuwa zikizidi kumfanya mpumbavu bila yeye kujijua. Lakini siku moja mtoto mmoja mdogo akaamua kuvunja ukimya na kuwasababisha watu wote wamuone Rais huyo ni mpumbavu kweli kweli.
Ni Hadithi ya Nguo Mpya za Mfalme, iliyoandikwa na Hans Christian Andersen, iliyochapishwa mwaka wa 1837. Lakini inaakisi maisha yetu waafrika wa sasa, kama una D mbili hutatumia nguvu nyingi kujua nini funzo lake kwetu.
Hadithi yenyewe inasema: Zamani za kale, kulikuwa na Mfalme ambaye alijali sana suala la unadhifu wa mavazi yake na alipenda kuonyesha kwa watu wote. Siku moja, wajanja wawili walimwendea na kumwambia wanaweza kumtengenezea suti ya nguo bora kabisa kutoka kwenye kitambaa kizuri sana. Walisema kitambaa hicho kilikuwa maalum sana. Kitambaa hicho kilikuwa hakionekani na wapumbavu na watu wa hali ya chini, yaani ukiwa mtu mpumbavu huwezi kukiona hicho kitambaa.
Kwa kuwa alikuwa na wasiwasi kidogo kama yeye mwenyewe angeona kitambaa hicho, mfalme alituma washauri wake wawili waaminifu waende kwanza kuona hicho kitambaa maalum. Bila shaka, hapakuwa na kitambaa kabisa, lakini hawakuwa tayari kukiri kwamba hawakuweza kukiona na hivyo wakakisifu.
Ujumbe wa kitambaa hicho maalum ulisambaa, watu wote wa mji walijawa na hamu ya kujua ni jinsi gani majirani zao walivyokuwa wapumbavu.
Mfalme aliruhusu wajanja hao wamvike suti yake mpya maalum, iliyotengenezwa kwa kitambaa hicho maalum, kwa ajili ya msafara kupitia mji. Ingawa alijua yu uchi, kamwe hakukubali kwa sababu alihofia kwamba labda alikuwa hafai na mpumbavu kwa kutoona kwamba alikuwa hajavaa chochote. Yeye pia alihofia kwamba watu wa mji wangedhani kwamba yeye ni mpumbavu.
Bila shaka, watu wote wa mji walimsifu sana Mfalme kwa mavazi yake mazuri, wakiogopa kukiri kwamba hawakuweza kuona mavazi hayo, mpaka mtoto mmoja mdogo aliposema: "Lakini hana nguo!"
Wazazi wa mtoto walishangaa na kujaribu kumnyamazisha mtoto, lakini mtoto hakuwa tayari kunyamaza. Walipojaribu kumziba mdomo mtoto huyo, aliwatoa mikono wazazi wake kinywani mwake, aliendelea kusema, "Mfalme yu uchi!" Baadaye, watoto wachache walianza kucheka na kujiunga naye.
Baadaye watu wazima walijiunga na watoto wao na kuanza kusema kwa sauti ya chini, "Lakini Watoto wako sahihi! Yule mzee hana nguo. Yeye ni mpumbavu na anatarajia sisi tuwe wapumbavu pamoja naye!"