Wazo la kabwela
JF-Expert Member
- Feb 13, 2013
- 1,883
- 1,465
sdfg
MFALME HAAMBILIKI
..basi, hali ikazidi kua mbaya sana kijijini pale: mfalme akaota mapembe,hakutaka kusikia lolote lenye ukweli usiompendeza.
Na,kwakua wapambe wa mfalme walitambua hili ,wakahakikisha wanakijiji wanaosema kweli zisizompendeza mfalme wanashughulikiwa.
Mwanakijiji mmoja toka kaskazini mwa kijiji hiko ,aliamka katika mojawapo ya siku katika juma;aliamka na kuwahadithia wanakijiji wenzie ndoto yake juu ya kifo cha mfalme Haambiliki.
"nimeota mfalme Wetu atakufa,mungu atamchukua mfalme kama anatakavyotuchukua sisi wengine"! ..ndoto hiyo ikasambaa kijiji kizima na kuwafikia wapambe wa mfalme.
Wapambe wa mfalme wakamkamata na kumwambia .."lala na uote mfalme ataishi milele,na kisha upite kwenye masoko na magulio utangaze ndoto hiyo mpya".
Kukutaa kutimiza agizo lile la kuota tena kukamponza ,akakamatwa ,akasweka ndani mpaka mfalme atakapojiskia atolewe ..wanakijiji wenzie wakapoozwa na mikate 200 ili wasimlilie mwenzao.
Mwanakijiji mwingine alijitokeza kuhoji maarifa ,elimu na uelewa wa mfalme.Siku chache baadae akapotea kijijini asijulikane alipo na asionekane mpka Leo.
Hofu kuu ikatanda kijijini,wanakijiji walinyang'anywa si tu Uhuru wa kusema hata Uhuru wa kuota ndoto!!ukiota unakamatwa unawekwa kolokoloni kwa maelekezo toka juu.
-----------------------------
Kijiji cha Fikara ,kinapatikana mashariki mwa bara la Giza.Bara ambalo si tu wakazi wake ni weusi kwa rangi ya ngozi zao ,bali pia weusi huo upo hata ndani ya vichwa vyao.
Waoga,hawalalamiki hata wakiibiwa,rahisi kudanganyika...ujinga wao ni utaona wanapokua tayari kufa na kuua kuzipigania dini walizoletewa na watesi wao waliowatawala kabla ya Uhuru.
Kijiji hiki cha Fikara pamoja na kutawaliwa na wafalme watano kwa vipindi tofauti;ni mfalme mmoja tu anayekumbukwa mpaka sasa.Huyu ni mfalme wa kwanza wa kijiji hiko.
Mfalme mwingine aliyekua na uangalau mfalme wao wa pili.Huyu anakumbukwa kwa kuruhusu vitu vyote ikiwemo holela.Wanakijiji wakambatiza jina la "Mzee sawa"
-------------------------------
Mapambe ya Mfalme Haambiliki yakazidi urefu,kiburi,ukali nk vikaongezeka.
Akatangaza ni marufuku kwa wanakijiji kutembea wakiwa wamefumbua macho mawili.
"kuanzia leo,ni marufuku kwa mwanakijiji yoyote kutembea akiwa amefumbua macho yote mawili"..akaendelea kwa sauti yake ya kukwaruza iliyojaa ubabe na ulevi wa madaraka.."ni mimi tu na marafiki zangu ndio tunaruhusiwa kutembea tukiwa tunatizama kwa macho yote mawili"...akasimama kidogo na kuchukua pombe iliyokua mezani kwake na kisha akaendelea..."mtatembea mkiwa mmefumba macho mpka kwenye sherehe yangu ya kuzaliwa nitakayotimiza miaka 61"..(ilibaki miaka 4 kufika mwaka huo.)
....haiwezekani,haiwezekani kabisa,yaani tutembee bila kutazama?kwa nini mungu ametupa macho haya?.....huu ufalme uchwara hatuutaki...hatuutaki ufalme uchwara kijijini kwetu..!!..hayo yalikua maneno ya mwanakijiji mmoja kijijini hapo maarufu sana kwa ujuvi wake wa masuala ya sheria kijijini pale.
Akaendelea kusema kwa sauti ya juu..tutapinga ufalme uchwara popote pale...na mimi nasem..(kabla hajamaliza kundi la wapambe wafalme likamvamia na kumfunga kamba mkono na mguu yake na kumburuza mpaka kwa mfalme)
..baadaye akahifadhiwa kolokolono.
-------------------------------
Pakalala pakaamkwa,pakakucha na kuchwea,masaa yakakatika mithili ya pepo za kusi,hatimaye mzee moja mwenye nywele nyeupe kichwa kizima akajitokeza kutia neno kijijini pale.
Mzee huyu ndiye hasa wanakijiji wanapenda awe mfalme wao.Inaaminika ana sifa zote zenye kukidhi hitaji la nafasi ile ya ufalme,hekima,upole,uungwana na upendo.Inashindikana kua mfalme kwa sababu ufalme ni nafasi ya kurithishana.
Kama hutoki kwenye ukoo wa kifalme huwezi kua mfalme(hii ipo pahala popote pale).Katika kijiji kile cha Fikara, mfalme alikua anapaswa kutoka kwenye hoop wa kijani tu.Hii ndio sababu inayofanya mzee huyu mwenye mvi nyingi kushindwa kua mfalme wa Fikara.
Basi mzee huyu aliyejulikana kwa nywele zake nyeupe,akadhani huenda mfalme angeheshimu busara zake na angetengua amri hiyo ya kutembea bila kutumia macho.
"Mzee nywele nyeupe, wakati anakaribia kumaliza mazungumzo yake na wanakijiji wenziwe ...gafla wakiwa ndani wakafuatwa na wapambe wa mfalme na kuambiwa wanaitwa haraka sana na mfalme..na huo ukawa mwisho wa mazungumzo yale.
-------------------------------
...."hatukubali ,hatukubali,hatukubali lazima septemba mosi mwaka huu wanakijiji wote tujitokeze mitaani na kupinga udhalimu huu..."
....akaendelea na maandamano hayo yatashirikisha watoto kwa vijana ,weusi kwa weupe,wafupi kwa warefu,wanene kwa wembamba,,,nk...
Anayetoa maneno hayo ni Bwana mmoja maarufu sana kijijini Fikara kwa kubishana na wafalme mara zote wanapoenenda tofauti.
Wanakijiji wengi waliamini ndiye mwanakijiji pekee jasiri,asiyeogopa kuweka korokoroni.,amewahi kusekwa korokorokoni mara kenda kwenye harakati zake.
Azimio la kukutana septemba mosi likapandwa na kumea na baadaye kukomaa kwenye mioyo ya wanakijiji wa Fikara.
Mfalme alipoona hali hii,akaagiza wapambe wake wapita mitaani na mapanga na majambia,visu na mundu,mishale na silaha nyingine za jadi kuwaonesha namna ambavyo silaha hizo zinavyua na kuumiza..kujeruhi na kutoa vilema..
Kijiji kikapata moto na kuiva tayari kwa ajili ya septemba mosi.viongozi wa dini za kijadi wakajitokeza kutoa neno....
Na hatimaye..........
Itaendelea....