Hizo ni zama za ujima ndugu yangu, ni zama za kutembea uchi wakati wa ujima mababu zetu na mabibi zetu hawakuwa na nguo za kujisitiri, inawezekana ni mila zao lakini lazima tukubali kuwa kuna mila nyingine hazifai kuendelezwa kwani ni za kishenzi, hao wazungu unaosema wanamuhusudu kwa kweli wanamshangaa alivyo zama za kale, leo hii tunapiga kelele dada zetu kuvaa nguo zinazobana mpaka mahospitalini wanazuiwa kuingia na nguo zisizo na staha, unafikiri kwa nini? Mahitaji muhimu kwa binadamu ni chakula, malazi na mavazi. Hapo mavazi hakuna ni ujinga mtupu, hebu muangalie vizuri alivyokaa, hata hajiamini kabisa kwa sababu yupo tofauti kabisa.