Mfahamu Zodiac Killer, muuaji aliyeitikisa Marekani

Mark pawelk

Senior Member
Jan 6, 2017
103
500
Kuanzia mwaka 1968 mpaka mwanzoni ya miaka ya 70 taifa kubwa la Marekani lilikubwa na mtu mmoja hatari sana,si mwingine bali ni muuaji tambulishi(serial killer) ambaye yeye kama yeye alipendelea kuitwa zodiac killer. Mpaka mtu apate sifa ya kuitwa serial killer anatakiwa awe ametekeleza mauaji wa watu si chini ya watatu katika matukio tofauti tofauti, na pawe na muda wa mapumziko(cooling off period) kati ya tukio moja na jingine.

Hii ni tofauti kidogo na FBI ambao wao wanamtambua 'serial killer' kama mtu aliyetekeleza mauaji ya kuanzia watu wawili katika matukio tofauti. Rekodi za vyombo vya usalama zinaonyesha huyu zodiac killer aliua watu watano waliodhibitishwa(zodiac's confirmed victims) na kujeruhi wengine wawili kwa vipindi tofauti,huku rekodi hizo hizo zikiinisha kua anaweza kua ameua watu 20 mpaka 28. Watu wengi wanaamini hii ni janja ya vyombo vya usalama kuficha aibu maana zodiac mwenyewe anadai kua ameua watu 37.

Muuaji tambulishi huyu alijizolea umaarufu mkubwa mpaka ikafika mahali kuna mtu aliyekua na umajinuni(obsession) na mapigo ya huyu zodiac killer akaanza kuiga na kutekeleza mauaji kama ya zodiac killer miaka ya tisini. Huyu bwana mdogo aliyekua anamuiga 'MASTER' zodiac killer(zodiac killer's copycat) alikua anaitwa Heriberto eddie seda,.

Seda alifanikiwa kuua watu watatu na kujeruhi wengine sita vibaya sana katika kipindi cha miaka mitatu, kutokana na ujuzi kuwa mdogo ukilinganisha na zodiac killer,Bwana mdogo Seda alikamatwa mwaka 1996 na kupigwa 'mvua' ya miaka 232 jela bila msamaha. Turejee kwa 'MASTER' zodiac killer ambaye alikua akifanya mauaji yake katika jimbo la Carlifonia japo pia inasadikika alifanya na matukio mengine jimbo la Nevada.....TUKIO LA KWANZA 'LAKE HERMAN ROAD ATTACK'
Tarehe 20 disemba mwaka 1968, Binti Betty Jensen mwenye miaka 16 anaonekana kua mwenye furaha kuliko watu wote duniani, Hii ni kutokana na sababu ya kupewa ruhusa kwa mara ya kwanza na wazazi wake kutoka na mpenzi wake David Faraday mwenye miaka 17 usiku(first date)...

Baada ya kufanya matanuzi ya hapa na pale wapenzi hawa wanaamua kwenda sehemu moja tulivu(lover's lane) ambayo ilikua mahususi kwa ajili ya wapendanao. kufika pale wapenzi hawa wakapaki gari yao, baada ya muda ikaja gari nyingine nyuma yao nayo ikapaki. Akatoka mtu akawaamuru washuke kwenye gari...

Bila ya kelewa nini kinaendelea akaanza kushuka bidada Betty Jensen, ile David nae akiwa anashuka mtu huyu aliyekuja akatoa bastola na kumpiga David risasi ya kichwani iliyopelekea mauti yake papo hapo. Kuona vile bidada betty akawa hana namna zaidi ya kukimbia ili kunusuru maisha yake, Alipofika hatua 28 kutoka pale walipokua wamepaki gari nae aliuliwa kwa kupigwa risasi tano mgongoni.. muuaji akawasha gari lake akaondoka zake..

Picha ya tukio zima ndio hiyo, ila swali la msingi sana(critical question) ni kwamba inawezekanaje jopo hili la wanausalama kupata picha kamili ya tukio zima ilihali hawa wapenzi walikutwa wameshakufa na muuaji hajulikani???walichokuta ni miili ya marehemu na gari lao na wakadai wamekuta alama ya matairi ya gari lingine likiwa linaondoka. Lakini je,hii inatosha kupata tukio zima la haya mauaji? je, kuna mtu alishuhudia hili tukio?TUKIO LA PILI 'BLUE ROCK SPRINGS ATTACK'

Kwa wajuzi wa historia mtakubaliana na mimi kwamba tarehe 4 ya mwezi wa saba ni siku kubwa sana nchini marekani, hii ndio tarehe wamarekani walipata uhuru na ndio mwanzo wa kuzaliwa kwa taifa kubwa duniani,hii ilikua mwaka 1776. Ni tarehe 4 mwezi wa saba 1969 mida ya usiku,watu wakiwa kwenye shamra shamra za hapa na pale, hii ni tofauti kwa wapenzi wawili Michael Mageau na Darlene Ferrin ambao walikua wamekaa kwenye gari kwa utulivu kabisa mahali panapoitwa 'Blue rock springs'(Maili nne kutoka Lake herman sehemu ya tukio la kwanza)...

Baada ya muda wanakuja vijana kwenye gari lingine wanaanza kupiga baruti(fireworks) nyingi huku wakizisindikiza na vicheko..hii ni kawaida sana kwa siku hii ya kipekee,hawakai sana hapo baada ya dakika kadhaa wanaondoka na kuwaacha hawa wapenzi wawili kwenye utulivu tena..
Wakiwa bado kwenye gari, Mara linakuja gari lingine karibu yao lakini linaondoka, baada ya muda kidogo gari lile lile linarudi kwa mara nyingine, anashuka dereva wa hili gari na kuanza kuelekea kwenye gari walilokaa Michael na Darlene. Mtu huyu aliyekuja anawafata huku akiwa kawamulika na tochi yenye mwanga mkali(flashlight) wapenzi hawa.

Michael anamtoa woga mpenzi wake kwa kumuambia kua huyu atakua ni polisi hivyo watoe vitambulisho vyao maana atahitaji kuviona, kwa mshangao mtu huyu aliyekuja alivyofika karibu bila ya kuongea lolote alitoa bastola na kuwafyatulia wapenzi hawa risasi tano kisha akageuka kuondoka zake...

Akiwa anaelekea kwenye gari lake, Michael alitoa kilio cha kuashiria kuugulia maumivu hali iliyopelekea mtu huyu kurudi tena na kuwapiga wapenzi hawa risasi mbili mbili nyingine kisha kuondoka zake.. Michael alikufa hospitalini lakini kwa bahati sana bidada Darlene alipona licha ya kupigwa risasi usoni,shingoni na kifuani. Yeye ndio alioelezea hili tukio licha ya kutoona sura ya muuaji.ZODIAC KILLER ANAHUSISHWAJE NA MATUKIO HAYA MAWILI?
Kesho yake(05/07) 'Mnyama' zodiac killer kwa mbwembe kabisa anawapigia simu polisi kwa kutumia simu za vibandani(phone booth) kuwa yeye ndio kahusika na mauaji yaliyotokea jana yake, polisi wanafanya jitihada wanajua sehemu simu ilipotoka lakini mtu huyu alishaondoka muda sana...


BARUA ZA ZODIAC
Mwezi wa nane mwaka huo huo Zodaic anaandika barua moja moja kwa vyombo vitatu vya habari tofauti, na katika kila barua akaweka kipande cha fumbo(cipher) huku akibainisha kua wakiunganisha hayo mafumbo matatu na kuweza kung'amua(crack) fumbo hilo litawapa mwanga ye ni nani. pia alielezea kuhusika na matukio yote mawili hapo juu.

Zodiac akaenda mbali zaidi na kuwatumia ujumbe wa sauti akieleza hatua moja baada ya nyingine jinsi alivyotelekeza mauaji hayo, hii inapelekea kuaminiwa kwa kua taarifa za kina za haya mauaji hazikua zimetolewa kwa jamii(confidental information)
Kuonyesha ubabe zodiac anawaamuru wachapishe barua zake katika ukurasa wa mbele wa magazeti yao la sivyo ataua watu mfululizo wiki nzima, Mpaka hapa vyombo vya usalama washaelewa kua zodiac si mtu wa 'Mchezo Mchezo' hivyo basi kesho yake wanachapisha barua zake katika ukurusa wa nne wa gazeti.
Juhudi zinafanyika wataalamu wanang'amua fumbo la zodiac baada ya wiki na kugundua alikua anadhamiria kutoa ujumbe kama ilivyoonekana pichani

(solved zodiac cipher) photo credit; biography.com


TUKIO LINGINE LA ZODIAC 'LAKE BERRYESSA ATTACK'

Hili ziwa la kutengeneza(man made) lilipendwa sana na watu kwa ajili ya kwenda kupumzika au kuvua, tarehe 27 septemba 1969,Wanachuo wawili ambao walikua ni marafiki Bryan Hartnell na Cecilia Shepard walikua ziwani hapa kwa ajili ya mandhari(picnic), ndipo alipotokea mtu mmoja akiwa amevaa sweta linalofunika kichwa(hood) na miwani.

Mtu huyu alikuja akiwa kawashikilia bastola marafiki hawa na kudai kua anahitaji gari lao na pesa ili atoreke maana alikua amefanya mauaji. Baada ya kupata anachohitaji mtu huyu aliwafunga mikono marafiki hawa lakini kabla ya kuondoka aliwachoma choma na kisu kirefu kisha akaondoka na gari lao.

Hili gari lilikuja kukutwa limetelekezwa mahali likiwa na ujumbe mlangoni uliosomeka sept 27 'S6:30/by knife' .... Kuonyesha ubabe wake tena, Zodiac aliwapigia simu polisi tena akitumia simu za vibandani na kuwaeleza juu ya tukio alilolifanya na kuwaelekeza mahali,Huku akijigamba kwa sauti 'I did it,I did it'(nimefanya,nimefanya) Lakini kwa bahati nzuri marafiki wale wawili waliokolewa na wasamaria wema na kupelekwa hospitali ambako bryan alipona na cecilia kufariki... Bryan ndo alielezea hiki kisa na kusaidia katika kuchora mchoro unaotoa picha ya huyu muuaji. Mpaka hapo juhudi za kumpata zodiac zimegonga mwamba


ZODIAC ANASHAMBULIA TENA 'PRESIDIO HEIGHT ATTACK'
Baada ya wiki mbili, mtu mmoja anachukua teksi na kuomba kupelekwa mahali panapoitwa "presidio heights', lakini wakiwa njiani mtu huyu anatoa risasi na kumuua dreva teksi huyu, tukio hili linashuhudiwa na watoto watatu ambao walikua mbali kidogo na lile eneo, wanapiga simu polisi na polisi wa karibu anafatilia mahali pale..

Taarifa kutoka kwa hawa watoto ni kwamba japokua hawajamuona vizuri muuaji ila wanahisi ni kama mtu mweusi, polisi aliyekua anafatalia hili tukio anakuja badae kudai kua alipishana na mwanamme mzungu ambaye alionekana kama ana haraka na wasiwasi mwingi karibu na eneo la tukio lakini hakumtilia maanani maana alipewa maelekezo ya kumtafuta mtuhumiwa mweusi. Mchanganyo huo wa rangi mpaka leo umeshindwa kuelezewa

Siku tatu baada ya tukio, 'Mbabe' Zodiac anawatumia polisi barua yenye maelezo kua yeye ndie aliyemuua yule dreva teksi, ili kudhibitisha hili akawatumia na kipisi kidogo cha nguo(swath) ambacho alikikata kutoka kwenye shati alilovaa yule dreva. Watoto wale watatu wanasaidiana na watalaamu kuchora picha ya muonekano wa zodiac(composite sketch)

ZODIAC ANAWATEKA MAMA MJAMZITO NA MTOTO WAKE MCHANGA
Mwezi machi 22 1970, mwanamke mjamzito kathleen jones akiwa na mwanae mchanga wa miezi kumi yupo ndani ya gari akiwa anaenda kumtembelea mama yake, ghafla kwa nyuma linatokea gari lingine likiwapigia honi na kuwawashia taa.. Mwanamke huyu anaamua kupaki gari pembeni. Anakuja mwanaume kutoka kwenye lile gari lingine na kumwambia huyu mwanamke kua tairi lake na mbele linacheza cheza kama limelegea.

Mwanaume huyu anajitolea kumpa msaada Kathleen wa kukaza nati za tairi lake, Anachukua vifaa na kuanza kukaza nati kisha anamwambia " you are good to go"(unaweza kwenda).... Kathleen anashukuru kwa usamaria na kurudi kwenye gari, lakini anashangaa pale anapotaka kuondoka lile tairi linakua limelegea zaidi kiasi cha kutaka kuchomoka kabisaa..
Kuona vile yule mwanamme anaamua kuwapa lifti mpaka kituo cha karibu cha mafuta ili waweze kupata msaada zaidi, lakini cha ajabu mwanamme huyu akawa anaendesha gari kwa zaidi ya lisaa huku akiwa amevipita vituo vingi vya mafuta. Kathleen ameshapata wasiwasi na kila akiuliza akawa anapewa majibu yasioridhisha... Wakafika sehemu yule mwanamme akasimamisha gari kisha Kathleen akachoropoka kutoka kwenye gari na kichanga chake na kukimbia, yule mwanamme akawatafuta bila mafanikio maana ilikua usiku akaamua kuondoka zake.

Kathleen alivyotoa taarifa polisi wakamuonesha michoro ya mfanano wa zodiac(composite sketches) na akadhibitisha kua yule mwanamme alikua Zodiac, Japo wanausalama wengi walipata na wasiwasi na maelezo ya Kathleen maana huu mfumo sio wa Zodiac, yeye anafahamika kama mtu hatari sana na walishangaa jinsi huyu Kathleen alivyotoka mikononi mwake kirahisi, hii ilipelekea wao kuhisi huenda Zodiac nae ana ka 'Hofu' ka MUNGU hivyo aliamua tu kuwaacha


ZODIAC ANAZIDI KUWASILIANA NA POLISI NA VYOMBO VYA HABARI

Zodiac alikua ashakua 'supastaa' na alikua anapenda sana kujulikana(attention seeker)... Aliwaandikia barua polisi kuwaeleza alivyohusika na kutekwa kwa Kathleen, Pia aliandika barua nyingine yenye ujumbe uliosomeka 'My name is ....... ikifuatiwa na fumbo lenye alama 13.. Ambalo wataalamu walishindwa kuling'amua. Vyombo vya usalama wakajiuliza kwanini Zodiac anapendelea kutuma ujumbe kwa mafumbo? hali hii ilipelekea kuwapa mwanga kua wanamtafuta mtu ambaye ni mtaalamu wa hisabati...

Katika barua nyingine Zodiac aliwapa pole polisi maana kulikua na tukio la kulipulia kwa kituo cha polisi siku si nyingi lakini alienda mbele zaidi na kusema " it's more glory to kill a cop than a sic, because cops can shoot back" (ni furaha zaidi kuua polisi kuliko mtu wa kawaida maana polisi wanaweza kujihami)

Zodaic anaendelea kuwaandikia 'Marafiki' zake polisi pamoja na vyombo vya habari barua huku mara kwa mara akiambatanisha na kadi za salamu(greeting cards).. katika barua moja anawaamuru polisi wahamasishe watu mtaani kuvaa nguo zenye vifungo vyenye alama ya zodiac, pamoja na vitu mbalimbali venye alama yake( ikumbukwe hapa watu walishaanza kutengeneza vitu venye alama ya Zodiac), anawaambia washipofanya hivyo atalipua gari lenye watoto wa shule na kuwaua wote, kwa dharau na kujiamini kabisa anaandika " it's easy, you just shoot the fucking tires and watch the kids fly out" (ni rahisi sana,unapiga risasi matairi na kuangalia watoto wanavyodondoka)

Pia anaelezea jinsi anavyopanga kuwatesa watumwa wake(slaves) wakifika paradiso. (kama inavyoonesha pale juu kwenye picha,Zodiac anaamini watu wote aliowaua watakuja kuwa mateka wake paradiso)... Anamwaandikia barua pia Paul Avery ambaye alikua mwanahabari aliyekua anaifatilia kesi ya Zodiac kwa karibu ujumbe akimwambia "pick a boo, you are doomed"(umekwisha)

Zodiac pia anaandika barua kuonyesha kusikitishwa na uwezo mdogo(incompetence) ya vyombo vya usalama huku akibainisha kua inawezekanaje wamegundukua matukio yake machache tu wakati yeye amefanya mengi sana.. hapa 'mbabe' Zodiac aliwaandikia "Why are you only finding the easy ones?? there are hell lot more down there" (kwanini mnagundua matukio marahisi tu? kuna mengi sana mbona)...

Kudhibitisha hili anawaeleza kuhusu matukio mbali mbali ambapo kuna watu walikua wanaripotiwa kupotea kua yeye ndiye aliyewaua, pia anaelezea kuhusika na vifo vingine ambavyo polisi walikua hawamuhusishi navyo yeye.


BARUA YA MWISHO YA ZODIAC
Baada ya kua kimya kwa muda mrefu Zodiac anaandika barua yake ya mwisho huku sehemu kubwa akiisifia filamu ya kutisha ya 'THE EXORCIST' iliyotoka mwaka 1973. Hapa anawaandikia kwamba "its the best sateral comidy i have ever seen". anamalizia barua yake kwa kujigamba na namba ya watu aliowaua akisema " ME=37 POLICE=0

WATUHUMIWA KESI YA ZODIAC

Watuhumiwa walikua wengi ila aliyewavutia sana vyombo vya usalama alikua Leign Allen, hawakua na ushahidi mzuri sana (solid evidence) wa kuweza kubaini kama ndiye Zodiac killer zaidi ya hisia na ushahidi wa mazingira(circumstantial evidence).. Walikuja kumuachia Allen baada ya kupima vinasibu(dna) yake wakilinganisha na sampuli ya vinasibu walivyopata kwenye mate ya kufungia bahasha katika mfululizo wa barua za Zodiac na kukuta havifanani

HITIMISHO
Mpaka leo 'Bingwa' huyu Zodiac hajulikani ni nani, Mwaka 2004 waliamua kufunga hii kesi, 2007 wakaifungua tena lakini hakuna chochote kilichoendelea ikabidi waifunge tena. Kuna vitabu vingi sana vimeandikwa kwa kutumia matukio haya na filamu mbalimbali,mfano ni filamu ya ZODIAC yenyewe. Wanasema huenda Zodiac bado yupo hai.(zodiac composite sketch) photo credit: biography.com-zodiac mystery remains unsolved-

Reference

> FBI CASES FILES ON THE ZODIAC KILLER ( ntajaribu kuweka link )
> REDDIT WEBSITE


~Mark Pawelk~
 

kanonb

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
369
500
Huyo Jamaa kwa matukio hayo naweza mfananisha na yule jamaa wa Tarime aliyewalaza Tarime saa 12 za jioni pamoja na kupelekewa kikosi maalum haikufua dafu. Jina lake limenitoka ila alijiwekea historia ya pekee kwa wakurya wa Tarime.

Mauaji ya Kutisha Tarime
Mtu huyu alikuwa akijitambulisha kwa jina la Charles Range Kichune, Josephat Chacha, Charles Joseph Msong’o (38) mkazi wa Kijiji cha Kenyamanyori Kata ya Turwa wilayani Tarime.
 

mogitete

Senior Member
Oct 12, 2016
137
250
Huyo Jamaa kwa matukio hayo naweza mfananisha na yule jamaa wa Tarime aliyewalaza Tarime saa 12 za jioni pamoja na kupelekewa kikosi maalum haikufua dafu. Jina lake limenitoka ila alijiwekea historia ya pekee kwa wakurya wa Tarime.

Mauaji ya Kutisha Tarime
Umenikumbusha mbali sana,jamaa alisumbua sana alikuwa anaitwa Charles Kichune(Kinonke)kwa utani SAA 12 jioni ndani ya Nyumba na madirisha umefunga.
 

denoo49

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
6,111
2,000
Umenikumbusha mbali sana,jamaa alisumbua sana alikuwa anaitwa Charles Kichune(Kinonke)kwa utani SAA 12 jioni ndani ya Nyumba na madirisha umefunga.
Ewaaa hilo la Kinonke ndio nilikuwa nalisubiri mkuu, wakurya wote Ujasiri waliuazima nchi jirani.
 

chenjichenji

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
1,420
2,000
Mkuu stori safi sana na ahsante kwa kushea nasi hii kitu.
Hapa nimekumbuka muvi moja ya Denzel Washington na Anjeline Jolie,jina lake limenitoka kidogo.Inashabihiana na baadhi ya matukio ulioyaelezea.
 

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,150
2,000
kuna crime moja nimeisahau jina huyo jamaa alikuwa anaua watoto tu.ilisababisha huo wa marekani uingie hofu ya kutisha ya kupotea watoto.jamaa katika interogation anasema aliamua kuua watoto sababu wakikua watakutana na changamoto kubwa za kimaisha kama zake hivyo akaona bora awasend afterlife
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom