Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 741
Simba wakiwa wengi kama kumi na tano na kuendelea wanauwezo wa kumshusha tembo lakini mziki unakuja kwenye kumla maana tembo ana ngozi ngumu ajabu unaambiwa ile ngozi hata mshale unadundaSafi,umechambua vizuri,,,nimependa hapo manii yake ni lita TANO za ujazo, na mkonga wake una misuri elfu moja, ivi simba wana uwezo wakumuua tembo mkuu,,kama wanavyomuua nyati
Ni kama tu ilivyo kwa binadamu lakini kidogo wao hawasikii vizuri ila ni wataalamu wa kunusa pia macho yao hayaoni vizuri wakati wa kula na badala yake hutumia ule mkonga wao kunusia majani kama yanafaa kula kwanza au la. Kwenye swala la kujilinda dhidi ya maadui wao hutumia zaidi miili yao mikubwa kuwatisha maadui na ndio maana tembo na faru ndio wanyama wanaoongoza kwa kuwa na maadui wachache porini ulilinganisha na wanyama wengine kama swala kwa hivyo miili yao ni silaha tosha dhidi ya maadui. Maadui wakubwa wa tembo na faru ni binadamu ambao huwawinda kwa sababu ya pembe zao pamoja na meno na kwa kiasi kidogo simba ambao wao huua zaidi watoto wao.Ana milango mingapi ya ufahamu? Anajilindaje?
Anzisha thread yako na wewe mwenye mwandiko mzuri....Mwandiko mbaya hauvutii kusoma
Simba hana ubavu wa kumuua tembo.Safi,umechambua vizuri,,,nimependa hapo manii yake ni lita TANO za ujazo, na mkonga wake una misuri elfu moja, ivi simba wana uwezo wakumuua tembo mkuu,,kama wanavyomuua nyati
Ni kama tu ilivyo kwa binadamu lakini kidogo.
Andika wako unao vutia tusomeMwandiko mbaya hauvutii kusoma
Hapana mkuu tembo wana rangi moja ila wakati mwingine huweza kubadilika rangi kutokana na tabia yao yard kujiwekea maji na matope (wallowing ) ili kupunguza joto katika miili yao wakati wa jua kali kwa sababu wao hawana nywele kama wanyama wengine wao ni hairless mammals na pia hii tabia ya wallowing hufanywa na wanyama wengine pia ambao hawana nywele katika miili yao kama mbogo (Buffalo ), faru (Rhino ) na hata ngiri (Warthog )
nadhani hii hutokana na athari za jua.Mbona tembo wa Manyara wana utofauti wa rangi na tembo wa Ngorongoro crater?
nadhani hii hutokana na athari za jua.
pindi mnyama anapo pingwa na jua muda mwingi rangi yake hupauka mfano ni nyumbu wa kusini na nyumbu wa kaskazini.
huenda wa manyara akawa na rangi ilo iva kutokana na nature ya hifadhi ilivyo maana ni sehemu kubwa ni forest ambapo humsaidia mnyama kujikinga na jua.
nafikili ndo sababu japo sina uhakika.
Wanaweza wakatofautiana rangi na ukubwa lakini wote ni specie moja. Kama mkuu alivyosema hapo juu, ni tofauti za mazingira ndio zinazosababisha hizo tofauti. Sina uhakika sana na hili, nadhani kuna wale tunawaita Forest Elephants na Savannah/Plains Elephants na ukiangalia hata kwenye haya majina tofauti ni mazingira ambayo wanyama hawa wana ustadi nayo na jinsi mazingira hayo yanavyochangia katika tofauti za either kimaumbile au rangi katika wanyama hao.Sio rangi tu mpaka ukubwa wa mwili. Wa Ngorongoro ni wakubwa zaidi ya Manyara.
nshu ya ukubwa hii hutokana na gene za mnyama husika.Sio rangi tu mpaka ukubwa wa mwili. Wa Ngorongoro ni wakubwa zaidi ya Manyara.
nshu ya ukubwa hii hutokana na gene za mnyama husika.
ni kweli tembo wa ngorongoro na ruaha hawa huwa na maumbo makubwa kulinganisha na tembo wa maeneo mengine na huwa nasikia tembo wa mikumi huwa na umbo dogo zaidi kuliko wengine.
hata zamani kulikuwa na simba wakubwa ila walimalizwa kwa kuwindwa na jamii za kimasai kutokana na nshu ya kuwa Moran ni mpaka umuue simba dume.
Poa mkuu nikipata nafasi nitaiwekamtaalam tukimaliza ya Tembo utupe na ya nyangumi maana kwa uzito(190t) aliokuwa nao anaweza akaja feri ghafla na kugeuka akayarusha maji yakafika mpaka magomeni na akaondoka kwa kasi ya bombadia....
Task zile ni meno ya mbele upande wa juu yaliyobadilika na kuwa katika mfumo wa pembe kwa kiswahili fasaha yale ni meno ya tembo na siyo pembe. Ukimwita tembo au ndovu ni sawa yote ni majina yakeMkuu hebu tufafanulie zile task zake kwa kiswahili fasaha huitwaje?
ni meno ya tembo, pembe za tembo au ndovu na je nisahihi tembo kumuita ndovu?