Online Pastor
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 1,948
- 1,524
Mwanaume aliyeponzwa na kinywa chake aliitwa Yeftha.
Alikuwa ni mwana wa kahaba na kama haitoshi nduguze walimfukuza ili asirithi nao. Ila Israeli ilipovamiwa na Waamoni waisraeli walimtafuta Yeftha mafichoni ili awaongoze kwenye hii vita ya ukombozi.
Yeftha akawakubalia kwa amri kuwa akiwapa ushindi basi awe mkuu wa Israeli yote. Nao kwa kuwa walikuwa na shida,walikubali. Ila kabla ya kwenda ya kwenda vitani,Yeftha alimwomba na kumwahidi Mungu kuwa iwapo atashinda vita basi,chochote kitakacho kuwa cha kwanza toka nyumbani kitakuwa sadaka ya kuteketezwa ya Bwana.
Na kweli,ushindi aliupata na nyumbani alirudi salama. Wakati akirudi toka vitani akiukaribia mlango wa nyumbani mwake,binti yake na mwanaye wa pekee alitoka mbio kuja kumlaki. Furaha ya ushindi wa vita ikawa kilio,na maumivu ya makovu ya vita yakawa maradufu.
Yeftha alitegemea kitu cha kwanza nyumbani mwake kitakuwa mwanambuzia au kondoo. Alilia sana kwa huzuni kwani kwa sheria ya torati mara ukishahaidi kitu ni lazima ukitende. Japo bintiwe alimfariji babaye kuwa hata kama aliahidi kumtoa kuwa sadaka yeye yuko tayari,ila Jemedari Yeftha aliumia sana.
TUNAJIFUNZA NINI
Usiahidi kitu hasa ukiwa na furaha au hamasa ya kufanya kitu.
Na hasa usimwahidi Mungu kitu usichojua utakitoaje kama nadhiri
REFFERENCES
Waamuzi 11:1-40