Mfahamu mwanadada Nightbird wa American Got Talent (AGT)

Jul 29, 2021
24
45
NIGHTBIRD 1.jpg
nightbird 3.jpg

Moja kati ya Matukio yaliyogusa hisia za watu wengi nchini marekani na duniani kote basi ni performance aliyoifanya mwanadada Nightbirde (Jane Marczewski)

Mwanadada Jane Marczewski anayeenda kwa jina la Nightbirde amesisimua halaiki ya watu wengi katika stage alipoimba nyimbo yake original inayoitwa ‘’Its Okay’’ nyimbo ianayoelezea maisha yake ya mwaka uliopita.

Kama alivyoelezea kabla ya performance yake, amekua akipambana na ugonjwa wa saratani (Cancer)__na bado imekua ikimtafuna katika sehemu mbalimbali za mwili wake- - Lakini amesema anafikiria ni muhimu kwa watu kufahamu kuwa “Sisi ni bora na muhimu sana kuliko hata mambo mabaya ambayo yamekua yakitokea kwa ajili yetu”. Mwanadada huyu aliyezaliwa 31 Disemba mwaka 1990 alizidi kueleza kuwa huwezi kusubiri mpaka maisha yakawa rahisi ndipo uamue kuwa na Furaha (You can’t wait until life isn’t hard anymore before you decide to be happy) yeye anasema yote yanayotokea kwenye Maisha yake ni sawa tu, (’It’s Okay’’)

Mwanadada huyo mwenye asili ya Ohio nchini Marekani alizidi kufafanua kwa majaji Simon Cowel, Howie Mandell, Sofia Vergara and Heidi Klum kuwa amekua akipitia kwenye kipindi kigumu sana cha ndoa yake ya muda mrefu kuvunjika mwishoni mwa mwaka 2019 hali iliyosababishwa na harakati zote za kupambana na saratani ya mapafu, Mgongo na Ini. Alieleza katika akaunti yake ya instagram kuwa hadi sasa amepewa nafasi 2% ya kuishi. (miezi sita ya kuishi) amesema “nashukuru naendelea vizuri kwangu mimi naona kama ni muujiza juu ya muujiza. Nimemaliza baadhi ya matibabu wiki iliyopita na madaktari wanatarajia kuhakikisha nakuwa sawa na matibabu baadhi yaliyobaki”

Mwishoni,Jaji Simon alimpa nightbirde zawadi ya kengele (The golden buzzer) na kumkumbatia kwa furaha kwenye stage na kumpa sifa nyingi mwanadada nightbird na kumwambia imekua ni siku ya kushangaza na performance maridadi na watu wote walisimama kumpigia makofi na majaji wengine wakitoa maoni yao ya uimbaji mzuri kwa nightbird.

Katika mahojiano yaliyofanyika kati yake na NBC4i alielezea kwa nini aliamua kubadilisha jina lake, alisema kuwa alikua na ndoto nyingi sana katika Mziki na kila ikifika majira ya usiku katika safu za nyumba aliyokua akiishi ndege walikua wakiimba nje ya madirisha ya chumba chake usiku, na sasa ndoto yake ya kuimba ilipotimia.

Ndege walikua wakiimba kama vile ilikua ni asubuhi lakini hakukuwa na dalili zozote za mwanga bado, “nilikua ni mtu wa kuimba muda wa usiku na nilikua mwenye tumaini na uhakika kuwa asubuhi itakuja. Mwaka uliopita nilipoteza kabisa fahamu ambapo nilikua siwezi tena kuongea, siwezi kula na siwezi kuamka tena kwenye kitanda changu kwa miezi mitatu, Nilipoteza zaidi ya paundi 80 na katika hali hiyo niliamini sasa naenda kufa. Ni kipindi ambacho niliandika nyimbo ya ’It’s Okay’’ nilikua na wakati mgumu sana mambo yalikua yakienda vibaya , Niliamua kuandika , ’It’s Okay’’kwa sababu nilikubali, nilijiamini na nilijiambia kwa sauti kuwa Its Okay, kwa hiyo imekua ni nyimbo nikiimba na kujiona mimi mwenyewe mwenye nguvu bado, Its okay, ni story yangu, ni maisha yangu na kwa kila mmoja mwenye story yake pia”.

Hata hivyo imekua ni siku ya huzuni mwanadada Nightbirde alipoyaaga kwa hiari Mashindanao ya American got Talent kutokana na Saratani. Alisema “Saratani inanichukua nguvu na attention yangu” Akiongea na majaji wa AGT kwa njia ya Video ameeleza kwa sasa anahitaji muda zaidi wa kupambana na saratani, Majajai wamempa moyo wa matumaini na kumtakia kheri na kumuombea aweze pata nafuu na kurudi tena. Jaji simon alisema “Ahsante sana kwa kushiriki nasi na kwa kuimba nyimbo nzuri” Nightbird amepata mashabiki wengi sana katika akaunti yake ya instagram @nightbird na wengi wamekua wakimfariji na kumtaka azidi kupambana

Nightbirde aliandika “I cannot say thank you enough for the opportunity to have a moment to share my story, I think we’re witnessing such a beautiful picture of the human spirit and the triumph of the human spirit. I think it’s restored my faith in humanity a whole lot to see people come together just over the fact we all hurt, we all suffer and we all have the potential to overcome. This is the most beautiful thing that’s ever happened to me in my life.”

Hadi sasa –Its OK ambayo ina Golden Buzzer imefikisha viewers zaidi ya million 32 tangu ilipowekwa rasmi kwenye mtandao wa Youtube June 08. Jane anatufundisha kuhusu zawadi pekee ya Maisha, anatufundisha Tumaini anatufundisha Upendo. Be strong Jane



Black foreigner

Dodoma

12:57 PM​
 
Mbona iko wazi mkuu. Wote hao akina George Clooney, Adele, Beckham, Kanye & Kim, Oprah, Harry & Meghan, Pharrell, Beyonc na Kigogo, Messi, Ronaldo, Uefa champions league, na ligi zote za ulaya, tesla na musk, Bill gates, Amazon na bezos, uhuru kenyata, ramaphosa, ZEMBWELA
Kwahiyo Mkuu kama ni Freemason ina uhusiano gani na mada hapo juu kumhusu Nightbirde?.. Na Simon akiwa Freemason si ni maisha yake binafsi mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom