Mfahamu mchawi aliyekoswa na kitanzi mara 3

Mfahamu mchawi aliyekoswa na kitanzi mara 3

Mkuu nyoosha maelezo tu kwamba unataka pm za wadau wa Dawa za kienyeji. Pia lipia hii promo
 
Nini sasa kufanyiana uhuni mkuu?, siumalizie basi.
 
dunia ina mambo....waweza hisi kuwa ni sinulizi ya kutungwa ila mi naamini kwa 90% maana nimeshuhudia mengi hapa duniani.
 
Assalam
muendelezo juu ya Mzee Mchawi yataendelea Alhamisi kwani niko bize kidogo na operation za Nane8 so stay tuned by hiyo siku itakuwa ok tuvumiliane majukumu mengi yangu binafsi, familia na Kitaifa ila naahidi BAADA YA 88 MAMBO YATAENDELEA M/Mungu akipenda

Mkuu leo ndiyo Alhamis vipi muendelezo wa kisa cha Mzee Mchawi.
 
assalam wakuu
'huyu mzee ni mchawi sio buree, haiwezekani nasema huyu ni mchawi kwanini kwake tu? ila ok mrudisheni ndani' anaanza kusimulia Mzee Lingulungundwangu Kumahame akimnukuu mkuu wa gereza kuu mkoa wa Mtwara, LILUNGU lililopo Mtwara mjini.
Ilikuwa miaka ya 1980 enzi za utawala wa Mwl. Nyerere ndipo nilipokutwa na hatia kwa kesi ya mauaji hivyo nilihukumiwa kunyongwa hadi kufa. hukumu ilichelewa kutekelezwa kwani mwl hakupenda sana kuruhusu watu wake wanyongwe hivyo ilifika hadi kipingi cha Mwinyi ambae bila hiana alisaini hati ya kumruhusu mnyongaji mkuu wa Serikali atekeleze wajibu wake kwangu.
Kweli uliua?
kweli niliua nilisababusha kifo cha msela mwenzangu kisa demu kwani alinikuta niko na demu wake sio mkewe wakati wa ngoma za unyago kule kwetu Umakuani-(kabila la wamakua lipo Masasi(Mtwara). Jamaa kanikuta naongea na binti ghafla akanivamia kwa mangumi na mateke kwa kuwa wote tulikuwa vijana sikukubali nikajikaza mtoto wa kiume huku navizia upenyo nikimbie nikampiga ngumi moja tu shingoni jamaa chini. nilitoka eneo la tukio nikiamini nimemtia adabu kumbe duuh Lahaulaah jamaa ndo ikawa mwinyo wa uhai pale hivyo nikashtakiwa kwa kosa la kuua. Tendo lile liliharibu taswira yangu hata shahidi ilikuwa ngumu kumpata kwa sababu jamii iliona kunitetea laana ya kumtetea muuaji.
familia yangu tu ndio iliniona kuwa sina ukatili wa kudhamia kuua bali ilikuwa suala lisilowezekana upigwe na kijana mwenzio halafu uwe kimya eti unaogopa ukijihami utaua haiwezekani. mwanamgu we bado kijana je ukifumaniwa kwa mfano ila tusiombeee itokee na mfumanizi anakushambulia je utakaa tu akumalize au utajihami? ananiuliza mzee Mchawi nikamjibu nitajitetea ili nijinasue, akadakia naam hicho ndicho nilichokafanya bahati mbaya akafa
mwanangu kinachokufanya uende jela siyo matendo uliyofanya bali ushahidi na maelezo yako mbele ya Jaji. kifupi nilihukumiwa kwa sababu sikuwa na shahidi mujarabu.
siku ya Hukumu
kesi yangu
ilikuwa ya kwanza siku hiyo Mh Jaji alinitia hatiani na kunihukumu kunyongwa hadi kufa kwani niliua kwa kukusudia. familia ilipokea kwa masikitiko hukumu yangu kwani walijuwa kijana wao nilikuwanajinasua na kipigo, sikwenda eneo lile kudhuru mtu hibyo waliponitemeblea gerezani waliniahidi watapambana hadi mwisho kwani nilionewa tu sikusitahili kitanzi,anaendelea kusimulia Mzee Mchawi Jina maarufu alopewa na mkuu wa Gereza
Maisha ya gerezani
Maisha ya gerezani hasa miaka ile yalikuwa ya tabu na ubabe sana kwani msosi na malazi ya shida kwelikweli pia kwangu mie ambae nasubiri siku tu nile kitanzi yalikuwa magumu zaidi kwakuwa nishajuwa siko mbali kufa kwa maana kutoka tena kwenda uraiani haiwezekani.
Kitanzi cha kwanza
Sina kumbukumbu ya siku au tarehe ya kunyongwa bali matukio tu ya unyongaji yalivyokuwa yanafanyika. tulipewa taarifa ya kunyongwa miezi mitatu kabla ili mwenye ndugu aage japo wosia na sala za mwisho mwisho. Siku ilipofika tulikuwa paleple gerazani kwetu jumla ya wahalifu kama 5 hivi wote tunasubiri kunyongwa. Alienda wa kwanza, pili mi nikawa wa tatu nilipofika nikapewa dakika 2 za dua nami bila ajizi nikapiga dua zangu nzito nzito halafu nikavalishwa kitambaa chekundu nikasimama sehemu husika na kuvalishwa kamba ya kunyongea. Baada ya kujiridhisa na maadalizi yao ndipo kitufe kikabonyezwa ili sehemu niliyosimama ibonyee/izame chini nami nining'inie(hang) b ahati zuri ile sehemu ya kusimamia ambayo ndio huzama chini nashukuru haikuzama licha ya kubonyezwa zaidi ya mara 3. sijuwi tatizo lilikuwa umeme sijuwi.
Kilichpfuata
nilirudishwa gerezani kuendelea na maisha ya ufungwa ila wale wenzangu wote ambao nilikuwa nao sikuwaona tena nikajuwa washakufa ila na wale walionifuatia je maana kama mtambo uligoma kwangu iweje ulikubali kwa wengine nikahisi ni umeme ulikata. Anasisitiza mzee Mchawi
apangiwa siku nyingine ya kunyongwa
baada ya siku ya mwanzo mambo kufeli nilitaarifiwa tena siku ya kunyongwa, kama kawaida wazazi wangu wakaje wakaniopa moyo kuwa usijali M/Mungu yu pamoja nasi

Itaendele

Nawahi siti ya mbele ilikuwaje sasa ? Lete vitu
 
Gereza la Lilungu ni hatari sana watukutu wote wa Tanzania utawakuta pale
Yap...Karibia watukutu wote wanaweza kuwa pale ila ni kwa kanda ya kusini hilo ndio gereza kuu...Kuna Ukonga-Dar, Isanga-Dom, Uyui-Tabora, Butimba-Mwanza baadhi haya, ni habari nyingine...
 
Back
Top Bottom