GAS STATE
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 1,770
- 959
assalam wakuu
'huyu mzee ni mchawi sio buree, haiwezekani nasema huyu ni mchawi kwanini kwake tu? ila ok mrudisheni ndani' anaanza kusimulia Mzee Lingulungundwangu Kumahame akimnukuu mkuu wa gereza kuu mkoa wa Mtwara, LILUNGU lililopo Mtwara mjini.
Ilikuwa miaka ya 1980 enzi za utawala wa Mwl. Nyerere ndipo nilipokutwa na hatia kwa kesi ya mauaji hivyo nilihukumiwa kunyongwa hadi kufa. hukumu ilichelewa kutekelezwa kwani mwl hakupenda sana kuruhusu watu wake wanyongwe hivyo ilifika hadi kipingi cha Mwinyi ambae bila hiana alisaini hati ya kumruhusu mnyongaji mkuu wa Serikali atekeleze wajibu wake kwangu.
Kweli uliua?
kweli niliua nilisababusha kifo cha msela mwenzangu kisa demu kwani alinikuta niko na demu wake sio mkewe wakati wa ngoma za unyago kule kwetu Umakuani-(kabila la wamakua lipo Masasi(Mtwara). Jamaa kanikuta naongea na binti ghafla akanivamia kwa mangumi na mateke kwa kuwa wote tulikuwa vijana sikukubali nikajikaza mtoto wa kiume huku navizia upenyo nikimbie nikampiga ngumi moja tu shingoni jamaa chini. nilitoka eneo la tukio nikiamini nimemtia adabu kumbe duuh Lahaulaah jamaa ndo ikawa mwinyo wa uhai pale hivyo nikashtakiwa kwa kosa la kuua. Tendo lile liliharibu taswira yangu hata shahidi ilikuwa ngumu kumpata kwa sababu jamii iliona kunitetea laana ya kumtetea muuaji.
familia yangu tu ndio iliniona kuwa sina ukatili wa kudhamia kuua bali ilikuwa suala lisilowezekana upigwe na kijana mwenzio halafu uwe kimya eti unaogopa ukijihami utaua haiwezekani. mwanamgu we bado kijana je ukifumaniwa kwa mfano ila tusiombeee itokee na mfumanizi anakushambulia je utakaa tu akumalize au utajihami? ananiuliza mzee Mchawi nikamjibu nitajitetea ili nijinasue, akadakia naam hicho ndicho nilichokafanya bahati mbaya akafa
mwanangu kinachokufanya uende jela siyo matendo uliyofanya bali ushahidi na maelezo yako mbele ya Jaji. kifupi nilihukumiwa kwa sababu sikuwa na shahidi mujarabu.
siku ya Hukumu
kesi yangu ilikuwa ya kwanza siku hiyo Mh Jaji alinitia hatiani na kunihukumu kunyongwa hadi kufa kwani niliua kwa kukusudia. familia ilipokea kwa masikitiko hukumu yangu kwani walijuwa kijana wao nilikuwanajinasua na kipigo, sikwenda eneo lile kudhuru mtu hibyo waliponitemeblea gerezani waliniahidi watapambana hadi mwisho kwani nilionewa tu sikusitahili kitanzi,anaendelea kusimulia Mzee Mchawi Jina maarufu alopewa na mkuu wa Gereza
Maisha ya gerezani
Maisha ya gerezani hasa miaka ile yalikuwa ya tabu na ubabe sana kwani msosi na malazi ya shida kwelikweli pia kwangu mie ambae nasubiri siku tu nile kitanzi yalikuwa magumu zaidi kwakuwa nishajuwa siko mbali kufa kwa maana kutoka tena kwenda uraiani haiwezekani.
Kitanzi cha kwanza
Sina kumbukumbu ya siku au tarehe ya kunyongwa bali matukio tu ya unyongaji yalivyokuwa yanafanyika. tulipewa taarifa ya kunyongwa miezi mitatu kabla ili mwenye ndugu aage japo wosia na sala za mwisho mwisho. Siku ilipofika tulikuwa paleple gerazani kwetu jumla ya wahalifu kama 5 hivi wote tunasubiri kunyongwa. Alienda wa kwanza, pili mi nikawa wa tatu nilipofika nikapewa dakika 2 za dua nami bila ajizi nikapiga dua zangu nzito nzito halafu nikavalishwa kitambaa chekundu nikasimama sehemu husika na kuvalishwa kamba ya kunyongea. Baada ya kujiridhisa na maadalizi yao ndipo kitufe kikabonyezwa ili sehemu niliyosimama ibonyee/izame chini nami nining'inie(hang) b ahati zuri ile sehemu ya kusimamia ambayo ndio huzama chini nashukuru haikuzama licha ya kubonyezwa zaidi ya mara 3. sijuwi tatizo lilikuwa umeme sijuwi.
Kilichpfuata
nilirudishwa gerezani kuendelea na maisha ya ufungwa ila wale wenzangu wote ambao nilikuwa nao sikuwaona tena nikajuwa washakufa ila na wale walionifuatia je maana kama mtambo uligoma kwangu iweje ulikubali kwa wengine nikahisi ni umeme ulikata. Anasisitiza mzee Mchawi
apangiwa siku nyingine ya kunyongwa
baada ya siku ya mwanzo mambo kufeli nilitaarifiwa tena siku ya kunyongwa, kama kawaida wazazi wangu wakaje wakaniopa moyo kuwa usijali M/Mungu yu pamoja nasi
Itaendele
Mfahamu Mzee Mchawi aliekoswa na Kitanzi mara 3
Safari hii alikuja mama tu, ila kilichonishtua hakuwa na hali yoyote ya mshangao kwanini amenikuta hai ilhali alijuwa juu ya kitanzi, nami bila hiana baada ya salamu nikamuuliza mama safari hii ulipoipanga ulikuwa na dhamiria ipi yaani umekuja kufanya nini? Akanipa mshangao mi nikajuwa bado hajanielewa nikamuuliza tena mama ulitarajia kunikuta hai,au kuona kaburi?. Cha ajabu mama akacheka sana hadi afande akashtuka “vipi tena we Mchawi mnaleta makelele” nikamtuliza samahani mkuu tumekumbushana ya kifamilia, poa kimyakimya basi alimalizia afande.
Safari hii mama alikuwa na furaha sana hadi nikashangaa nikajiuliza kimoyomoyo kwani Huyu bi mkubwa leo vipi au anataka anisahaulishe na kifo kilichopo mbele yangu?. Mazungumzo yetu yalikuwa kama ifuatavyo
Mama:unaitwa jina gani? Kuna jina nimelisikia hapa
Mimi: Mchawi
Mama:yaani wewe ni Mchawi
Mimi: ndo jina naloitwa siku hizi baada ya kitanzi kunikosa
Mama: hee kumbe, mbona unapewa sifa sio zako wachawi sie tunaofanya mambo huko kitaa ila ok tuyaache.
Mimi: swali langu hujajibu juu ya ujio wako
Mama: hee wewe kwani ubaya mi kuja kukuangalia au unataka nisije tena sio?
Mimi: sa mama naanzaje kukukataza ila vipi ulijuwa kuwa nimenusurika kunyongwa baada ya mtambo kugoma.
Mama: nilijuwa sana, siku yako ya kunyongwa mimi na baba yako tulikesha maana hatukujuwa muda sahihi wa kitanzi hivyo tulikuwa macho muda wote huko Mtambaswala kwa babu yako
Mimi: ahsanteni kwa hiyo mkiniombea dua muda wote
Mama: naam, mbali ya dua tulikuwa tunakuona mubashara/live
Mimi: mmhh, nikaguna mama unataka kunibebesha magogo hapa live hiyo kivipi
Mama:kila ulichofanya hadi mtambo unakataa tulikuwa tunakuona we juwa hivyo tu kwa leo zaidi hadi ukitoka. Ila yote narudia tena leo M/Mungu yu pamoja nasi
‘Eti nikitoka huyu mzima huyu, Mama aliniacha na maswali kibao na hapo ndipo nilipojuwa kuwa tatizo halikuwa mtanbo bali ni maufundi ya familia ama kweli nimeamini Mwafrika ndio mwanzishaji na mzungu ni mboreshaji siku tukiacha ujinga na kuboresha wenyewe tutakuwa mbali sana’ alimalizia mzee Mchawi kwa kushusha pumzi
Hapo ndipo uzalendo ulipoinishinda nikamdadisi mzee Mchawi ina maana mchakato wote wa wewe kunyongwa walikuwa wanaushuhudia? Na je kwa njia gani? Nilimuuliza.
‘Ndio walishuhudia ila walitumia nini kuniona alinificha hakuniambia ‘ alinijibu mzee Mchawi
Hapo ndo nilikumbuka jinsi nikiwa mdogo kijijini kwetu hapohapo anapoishi mzee Mchawi siku hizi ila sio kwao kwani baada ya kutoka gerezani hakurudi kwao tena kwa sababu za kiusalama hivyo yupo kijijini kwetu.
Ilikuwa niaka ya 1998 niko darasas la pili kulikuwa na ligi ya mpira wa miguu kijiji jirani na bahati zuri timu moja kubwa iliwakilisha kijiji chetu katika mashindano hayo. Siku timu yetu ikicheza wazee walitumia kifaa maalumu kuangalia mwenendo wa mechi. Kifaa hiko kiliitwa Ngondingo chenye umbo la chupa kama ya shampeni na rangi nyeupe pee, ngondingo lilikuwa linasimamishwa halafu wazee wa timu (kamati ya ufundi) wanakizunguka na kukiangalia kwa maana ndani yake waliona mpira unavyopigwa/move lakini wachezaji hawakuonekana.
Mechi ikiwa ya uwiano/balance ngondingo ilitulia, timu yetu ikishambuliwa ilitikisika kulingana na kasi ya shambulio na ikishambulia ilizunguka pia kwa kasi ya shambulio. Timu ikifungwa ililala kwa maana toka kutikisika hadi kulala na ikifunga pia iliala toka kuzunguka hadi kulala.
Hivyo wazee walijuwa kuwa tumefungwa au tumefunga kwa kuangalia nini kimesababisha chupa kulala ni mtikisiko au mzunguko hivyo walijuwa matokeo mapema tu kwa kuuona kwao mubashara.
Nikarudi kwa Mzee Mchawi
‘Tutaona leo si unajifanya mchawi igome leo tuuone’ Mzee Mchawi alimnukuu askari wa zamu aliyemtoa selo kumpeleka chumba cha mauaji. Anaendelea nilipofika nilikuta sura mpya za waheshimiwa wale wanaopata riziki kupitia roho za watu ila kabla kuitwa nilipiga dua zangu kama kawa na yale maneno ya kijasiri niliyopewa na mama nikawa sina hofu liwale na liwe nikajiuliza kwa nini wameleta wanyongaji wapya? Aaahh inawezekana ndo mwenye zamu, nilijipa moyo.
Safari hii tulikuwa zaidi ya kumi maana gereza letu ndo kituo cha kunyongea kwa kanda ya kusini yote hivyo wingi wa waathirika sio ajabu sana.
Nikaanza mimi safari hii nilipofika tu nikaulizwa jina nikawatajia ghafla wakaanza kutazamana na kunigeukia pole “ndugu tunatekelza hukumu tu anaekuua sio mimi ni Jamhuri” nami nikakubali kauli yake kwa kutingisha kichwa,
‘panda kilingeni’.aliniamuru Yule mnyongaji mkuu nisie mjuwa jina, nami nikapanda afande Marwa mvalishe kitambaa alimuagiza msaidizi wake ambae ni afande wa pale gerezani na alizisikia taarifa zangu awali hivyo alikuwa na hamu aone je ni nguvu za soda tu au na leo tena. Ile ananigusa na tambala lake tu akala mweleka baba wa watu chini. “Vipi afande twende na muda” alikoroma mnyongaji mkuu. Anasimulia Mzee Mchawi kwa kicheko huku akimuigizia afande Marwa.
Alisimama afande Marwa kwa uoga na kunikaribia ili anivalishe tena ile kunigusa tu duhh …lahaulaaa umeme ukazima tii ndani giza tupu, nje kukaanza piga mvua na radi za kutisha ambazo ziliharibu transfoma ya gerezani pale na kusababusha kishindo kikali ambacho klia mfungwa na askari walisikia. Giza liliendelea hadi muda wa robo saa watu hawaonani ndani ya gereza ila nje kuna mvua ya kawaida na bustani zinaonekana kwani ilikuwa mida ya saa tano hivi asubuhi. Ila je giza hili linatoka wapi, nilishangaa, anaeleza mzee Mchawi.
‘Je taa za umeme ziliwashwa kabla ya tukio’ nilimuuliza, “hapana ndani kulikuwa kawaida tu hakukuwa na uhusiano baina ya umeme na mwanga mule ndani kifupi taa zilizimwa” anasisitiza Mzee Mchawi
‘Je giza lilitoka wapi’ nilimsaili mzee ndipo akanijibu sijuwi
kilichofuata
Nikiwa bado nipo palepale ndipo mayowe yakaanza mwacheni huuyooo, mwacheni huuuyooo
Mkuu wa gereza la Lilungu Kamishna Halfani Chitundi akaja chumbani akiwa na tochi na kukuta zoezi limesimama akawajuza kuwa umeme umekata kuna tatizo la transfoma pia akanishika mkono hadi chumbani kwangu. “Unatusumbua sana wewe Mmakua tutakunyonga hata kienyeji bwege… wewe” alinibwaga chini puu… naye akaenda zake ile nameza mate kwa kutoamini nilivyonusurika nuru ikaanza ndani yaani kweupeee. Baada ya hali ile yakasikika mayowee tena oyoooooo, kucheleeeeee. Muda wa chakula nikafuatwa na wafungwa wenzangu huku wakiimba Mchawiii kidume, mchawi kidume, mchawi nomaaa.
Aitwa na Kamishna wa Magereza
Nilipofika nilimkuta mnyongaji, afande Marwa na Mkuu wa gereza,wakinisubiri, nilipoketi nikaulizwa maswali machache ikwemo kwetu ni wapi nikawajibu ni Masasi Mkoani Mtwara. Hali iliyotokea ya giza nimeionaje nikawajibu ni kawaida tu Chief yoyote hafi pekeake lazima ampate wa kumsindikiza yaani pale mngelazimisha lazima ningetoka na mmoja kati yenu nyie watatu, anaendelea kufunguka mzee Mchawi kwa ujasiri mkubwa.
Wakanishangaa wale maafande Napata wapi ujasiri huo wa kuwatishia maisha,nikawaambia mimi ni chifu wa Ukoo yaani Mwenye (mwenye ni cheo kama vile Ntemi au Mangi au Mtwa) hivyo sifi kizembe. Niliwakazia macho wote watatu. Hebu kamalizane na wale wengine halafu huyu tumtafutie dawa yake hawezi kusumbua jeshi huyu hawezi sumbua jeshi hatadirishani tutamnyongea kwani hakimu kasema anyongwe hadi afe lakini ananyongwaje ni jukumu langu mimi alinitisha Mkuu wa gereza huku akipiga kifua chake. ‘Sawa mkuu’ aliitika afande Marwa na kwenda kuwanyonga wale wenzangu.
Anyongwa siku ya pili
Mnyongaji akionesha moyo wa huruma alimwamuru afande Marwa anifunge kitambaa haraka kwani anatakiwa akanyonge wengine huko Dodoma. Baada ya kuwa tayari walinivalisha kitanzi vp tayari sio ndio mkuu walijibizana wenyewe ok fyatua tu. Mnyongaji alibonyeza kitufe na kikakubali hivyo nikaning’inia jambo ambalo liliamsha shangwe kwa askari mule ndani duuh mtu anafurahi mwenzie kunyongwa lahaulaa ama kweli dunia haina huruma. Ndipo walipoenda kumfuata mkuu wa gereza ili kumpasha kuwa Mzee Mchawi kala kitanzi na biashara imeisha.
Wakosea kuvalisha kitanzi
‘Washenzi wakubwa ndo nini mmefanya hapa sasa kwa hiyo kafa au ndio mkuu ok mtoeni basi afande Marwa akanitoa ile kufika chini nikampa mkono kama namsalimia ‘hongera mkuu’. Afande hakuamini macho yake ndipo aliporoka “sijawahi ona mchawi kama wewe duuh” ‘usiogope mi mzimu tu’ nilimjibu. “Nilishawaambia huyu mchawi, ujuwe unatuumiza kichwa kwanini hutaki kufa wewe?” Aliwaka mkuu wa gereza kamishna Chitundi.
‘we kweli Mchawi Kwa hiyo ilikuwaje hadi unusurike’ nilimuuliza Mzee Mchawi
kitanzi walinivalisha kifuani yaani kwapani kama mtoto anavyopimwa kliniki hivyo hakikuwa na madhara kwangu. Anatiririka mzee Mchawi Je wao hawakuliona hilo au walipokuwa wanakuvalisha hawakujuwa sehemu sahihi? Nilimuuliza ndipo akanijibu sijuwi ila Yule ni mnyongaji mkuu wa serikali haiwezekani asijuwe wapi kitanzi hulengwa huenda ni kiini macho tu yaani anaona kama shingo kumbe kifua na kifua kama shingo’. Anasimulia mzee Mchawi kwa hamasa sana
Itaendelea

MUENDELEZO-Part II