Mfahamu Martin Luther King

Adil_101

Senior Member
Jul 26, 2022
110
339
Mnamo Agosti 28 mwaka 1963, karibu watu 250,000 walikusanyika kaika bustani ya kihistoria ya Lincoln Memorial mjini Washington-DC kumsikiliza mtu huyu akizungumza.

Jina lake lilikuwa Dkt Martin Luther King Jr na maneno aliyosema yanakubalika kote duniani hadi wa leo.

Dkt King, mwana wa kiume wa mhubiri kutoka Jimbo la Georgia kusini mwa Marekani, alikuwa na ndoto kuwa maisha ya watoto wake yatakuwa tofauti na jinsi maisha yake yalivyokuwa.
IMG_20230403_085809.jpg
 
Mnamo Agosti 28 mwaka 1963, karibu watu 250,000 walikusanyika kaika bustani ya kihistoria ya Lincoln Memorial mjini Washington-DC kumsikiliza mtu huyu akizungumza.

Jina lake lilikuwa Dkt Martin Luther King Jr na maneno aliyosema yanakubalika kote duniani hadi wa leo.

Dkt King, mwana wa kiume wa mhubiri kutoka Jimbo la Georgia kusini mwa Marekani, alikuwa na ndoto kuwa maisha ya watoto wake yatakuwa tofauti na jinsi maisha yake yalivyokuwa.View attachment 2574752
Ubaguzi wa rangi, au utengano kati ya wazungu na watu weusi,bado ulitekelezwa rasmi kote Amerika Kusini.

Waafrika na wazungu walitenganishwa, walikula katika migahawa tofauti, walikunywa maji kutoka kwenye chemichemi tofauti na kusafiri kwa kukaa katika maeneo tofauti ya mabasi.

Kimsingi, sheria za kibaguzi zilifanya iwe vigumu kwa wapiga kura weusi kuchagua wabunge ambao wangebadilisha kanuni hizo.

Lakini, ikiwa unafikiri ndoto za Dkt King ni za zamani za kale, pengine unahitaji kutafakari mara ya pili.

Kulingana na familia yake, miezi michache iliyopita imekuwa ukumbusho kwamba sehemu kubwa ya ndoto ya Dkt King bado haijatimia.

Katika majimbo yale yale ambapo ubaguzi ulikuwepo hapo awali, mabunge yanayoongozwa na Republican yamewezesha sheria ambazo wanaharakati, wanasema kuwanyima haki watu walio wachache, hususan wapiga kura weusi.

Hizi ni pamoja na masharti magumu ya kitambulisho na hata marufuku ya kutoa chakula au maji kwa watu waliopanga foleni kwa saa kadhaa kupiga kura.
IMG_20230403_085921.jpg
 
Ubaguzi wa rangi, au utengano kati ya wazungu na watu weusi,bado ulitekelezwa rasmi kote Amerika Kusini.

Waafrika na wazungu walitenganishwa, walikula katika migahawa tofauti, walikunywa maji kutoka kwenye chemichemi tofauti na kusafiri kwa kukaa katika maeneo tofauti ya mabasi.

Kimsingi, sheria za kibaguzi zilifanya iwe vigumu kwa wapiga kura weusi kuchagua wabunge ambao wangebadilisha kanuni hizo.

Lakini, ikiwa unafikiri ndoto za Dkt King ni za zamani za kale, pengine unahitaji kutafakari mara ya pili.

Kulingana na familia yake, miezi michache iliyopita imekuwa ukumbusho kwamba sehemu kubwa ya ndoto ya Dkt King bado haijatimia.

Katika majimbo yale yale ambapo ubaguzi ulikuwepo hapo awali, mabunge yanayoongozwa na Republican yamewezesha sheria ambazo wanaharakati, wanasema kuwanyima haki watu walio wachache, hususan wapiga kura weusi.

Hizi ni pamoja na masharti magumu ya kitambulisho na hata marufuku ya kutoa chakula au maji kwa watu waliopanga foleni kwa saa kadhaa kupiga kura.View attachment 2574755
Wimbi la sheria kama hizo zilipitishwa katika majimbo 19, ikiwemo Florida, Texas na Arizona, baada ya kuchaguliwa kwa Rais Joe Biden mnamo 2020.

Mtangulizi wake, Donald Trump, anasema uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.

Kwa hiyo wakati Marekani inaadhimisha Siku ya Martin Luther King tarehe 17 Januari, watoto wa kium na wa kike wa kiongozi huyo mashuhuri wanawaomba watu wasimkumbuke tu baba yao - bali wafuate nyayo zake na kuchukua hatua kulinda haki za watu weusi.

Tutakuwa tukiadhimisha sikukuu ya King, na tunawahimiza nyote muendelee na kumbukumbu zenu pia," binti yake Bernice King, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Martin Luther King Jr. wa Kituo cha Mabadiliko ya Kijamii Isiyo na Vurugu, alisema kwenye video.

Hata hivyo, ikiwa haki ya kupiga kura bado inaning'inia kwenye mizani, basi sisi, kwa maana hiyo sote, lazima kwa pamoja tutumie kumbukumbu zetu mbalimbali na majukwaa yetu ya siku hiyo kufanya kile ambacho Dk King angefanya.

Mzozo huo unachukuliwa kuwa "wakati mahususi" kwa demokrasia ya Marekani, kwa matamshi ya kiongozi mashuhuri wa haki za kiraia, Mchungaji Al Sharpton.

Akiongea Jumanne (11) huko Atlanta, latika nyumba ya zamani ya Martin Luther King, Biden alisema suala la haki ya kupiga kura ni "vita kwa roho ya Marekani".
IMG_20230403_090037.jpg
 
Wimbi la sheria kama hizo zilipitishwa katika majimbo 19, ikiwemo Florida, Texas na Arizona, baada ya kuchaguliwa kwa Rais Joe Biden mnamo 2020.

Mtangulizi wake, Donald Trump, anasema uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.

Kwa hiyo wakati Marekani inaadhimisha Siku ya Martin Luther King tarehe 17 Januari, watoto wa kium na wa kike wa kiongozi huyo mashuhuri wanawaomba watu wasimkumbuke tu baba yao - bali wafuate nyayo zake na kuchukua hatua kulinda haki za watu weusi.

Tutakuwa tukiadhimisha sikukuu ya King, na tunawahimiza nyote muendelee na kumbukumbu zenu pia," binti yake Bernice King, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Martin Luther King Jr. wa Kituo cha Mabadiliko ya Kijamii Isiyo na Vurugu, alisema kwenye video.

Hata hivyo, ikiwa haki ya kupiga kura bado inaning'inia kwenye mizani, basi sisi, kwa maana hiyo sote, lazima kwa pamoja tutumie kumbukumbu zetu mbalimbali na majukwaa yetu ya siku hiyo kufanya kile ambacho Dk King angefanya.

Mzozo huo unachukuliwa kuwa "wakati mahususi" kwa demokrasia ya Marekani, kwa matamshi ya kiongozi mashuhuri wa haki za kiraia, Mchungaji Al Sharpton.

Akiongea Jumanne (11) huko Atlanta, latika nyumba ya zamani ya Martin Luther King, Biden alisema suala la haki ya kupiga kura ni "vita kwa roho ya Marekani".View attachment 2574756
"Unataka kuwa upande wa Martin Luther King ama George Wallace?" Biden aliuliza, akiashiria vitendo vya kibaguzi vya gavana wa zamani wa Alabama.

Wakati muhimu katika mapambano ya kukomesha ubaguzi ulikuja mnamo 1955, baada ya Rosa Parks kukamatwa huko Alabama kwa kukataa kutoa kiti chake kwa abiria mzungu.

Jamii ya watu weusi wa eneo hilo ilichagua kususia huduma ya basi na kumtaka Dkt King kuongoza maandamano.

Hotuba zake zilichochea watu kupigana na ubaguzi lakini majibu yalikuwa mabaya: familia ya King ilipokea simu za vitisho na nyumba yao ilipigwa kwa bomu.

Dk King aliendelea kupigana kwa kutumia silaha anazoamini: nguvu ya hotuba na uhamasishaji. Aliamini katika upinzani usio na vurugu na alikataa kujibu madhila kwa chuki.

Maaandamano ya Washington kupigania Ajira na Uhuru mnamo 1963 ikawa wakati muhimu katika harakati za haki za kiraia.

Alikuwa akizungumza mbele ya sanamu kubwa ya Abraham Lincoln, rais wa Marekani ambaye alitangaza watumwa wote wa nchin hiyo kuachiwa huru mnamo 1863.

Mnamo 1964, Dkt King na vuguvugu la haki za kiraia walipata ushindi wao wa kihistoria. Sheria ya Haki za Kiraia ilikomesha rasmi ubaguzi katika maeneo ya umma na kupiga marufuku ubaguzi wa ajira.

Lakini vita hivyo vilikuwa mbali zaidi, kwani maadui wa usawa wa rangi waliendelea kutumia hila kufuata sera za ubaguzi wa rangi.

Sheria kote Kusini ziliendelea kuwanyima haki wapiga kura weusi kwa kuifanya iwe vigumu kwao kujiandikisha kushiriki katika uchaguzi.

Mnamo 1965, Dk King aliongoza maandamano ya kihistoria kutoka mji wa Selma, Alabama, hadi mji mkuu wa jimbo, Montgomery, kupinga sheria hizo.

Wakati waandamanaji hao wakielekea kwenye barabara kuu ya kilomita 87, walikumbana na ghasia mbaya kutoka kwa viongozi wa eneo hilo na vikundi vya walinzi.

Hata hivyo Dk King alishikilia msimam wake wa maandamano yasiyo ya vurugu.

Alikamatwa na kufungwa jela mara 29. Mnamo tarehe 4 Aprili 1968, alikuwa amesimama roshani ya chumba chake cha hoteli huko Memphis,Arizona,wakati alipopigwa risasi na mzungu aliyekuwa na bunduki.

Mauaji yake hayakufanya chochote ambacho kingeweza kupunguza jukumu la Dkt King katika historia ya Marekani, au ushawishi wake katika harakati za kisasa zinazopigania usawa katika jamii.

Vuguvugu kadhaa za kuteteahaki zimefuata nyayo za Dkt King

Maandamano ya amani yameangazia dhuluma sio tu kuhusu haki za kupiga kura,lakini pia "masuala mengine ya kimsingi,kijamii na kiuchumi ambayo yanatishia sio tu demokrasia yetu lakini ubinadamu wetu pia anasema Bernice.

Wakati huo huo, vuguvugu la Black Lives Matter (BLM) limesaidia kuunda mazungumzo kuhusu ubaguzi wa rangi wa kitaasisi, na hasaukatili wa polisi.

Bernice anasema kampeni yake ni "inaenda zaidi ya Marekani ili kujumuisha jamii ya kimataifa, kimkakati katika juhudi za kutokomeza kile baba yangu alichoita maovu mara tatu ya ubaguzi wa rangi, uchu wa mali na kijeshi. Kuunda jumuiya pendwa.

Kila mwaka, hotuba nzuri ya Martin Luther King na nguvu ya "ndoto" yake huadhimishwa kote Marekani siku ya Jumatatu karibu na siku yake ya kuzaliwa, 15 Januari 1929.

Lakini hata kupitishwa kwa sikukuu yenyewe kunaonyesha jinsi suala hilo linaweza kusababisha mgawanyiko - na linaendelea kugawanya jamii.

Ingawa tarehe hiyo ilipendekezwa siku chache tu baada ya kifo cha Dkt King, ilichukua miaka kadhaa kwa Bunge la Marekani kuondokana na upinzani wake dhidi ya kukumbuka picha ya harakati za haki za kiraia.

Siku ya Martin Luther King iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1986 - lakini ilichukuwa miaka mingine zaidi kabla ianze kuadhimishwa maeneo yote ya Amerika Kusini.

THE END
IMG_20230403_090411.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom