Mfahamu kunguru ndege anayeongea

Mfahamu kunguru ndege anayeongea

Duuuuhh .. hii kali ila ninafahamu kwamba kuna dini wanasema kunguru ndio alitambulisha kuzika na siku za kuomboleza..
Ushuhuda:
Kunguru walikiwa na mchezo wa kuingia banda la nguruwe na kudokoa vile piglets na kula utumbo wa uzazi kama nguruwe kazaa na vijana hawajasafisha.

Kuna siku tukawabananisha tukaua mmoja kisha tukamninginiza kwenye mlango...

Kunguru wote hawakufika tena, tukasema dawa tumepata

Aisee siku ya 40 walitokea kunguru kwa maelfu; walizunguka pale kama saa nzima huku wakipiga kelele, nilishangaa sana kwa nini

Baada ya huo muda wakaondoka; hadi leo sijaona kunguru tena mabandani.
 
Wanaitwaa KUNGURU ndege wenye uwezo wa kuongea zaidi ya kasuku

Unaweza ukashangaa lakini ndio uhalisia kwamba kunguru wanapiga lugha vizuri Pia ni ndege wenye akili sanaa

Kwa kingereza wanaitwa RAVENS wanapatikana bara la Africa, na bara la ulaya
kitaalam wanaitwa "Corvus corax" wanaurefu wa inch 15-27, mabawa yao yana urefu wa cm 120-150 na uzito ni kg 3
.mifupa yao ina hewa sio uroto mwekundu ndio mana hapigwi shoti

Ni ndege wenye akili sanaa hii ni kutokana na mfumo wa maisha yao na wanafananishwa na sokwe na dolfin kwa uwezo wa akili
kunguru huwezi kumkamata kizembee maana wanauwezo mkubwa wa kureason mambo

Ni moja ya ndege wanaoweza kuongea kama vile binadamu zaidi ya kasuku hii ni kwasababu wanamemory kubwa ya kukalili vile vile hukalili mtu hasa aliyewafanyia ubaya kama kuuwa mwenzao na ikitokea hivyo mara nyingi huwa wanasumbua na kula vitu vyake makusudi kama kisasi

Kunguru wanaishii kijaamii sana na hufanya michezo mingi sana kama vile kulea watoto matoy, na vile vile huwa na vita na ndege wengine hasa wanapoona ni adui yao humrukia na kumparua kwa umoja
vile vile huonyesha kujaliana hata mwenzao akifa huweka kabisa msibaa kuomboleza kwa siku kadhaa

Chakula chao kikuu ni vyakula vya majumbani na baadhi hula mizoga na kunaa baadhi hula nyama yaani wanaweza hata kuwinda wakizidiwa

Pia wanatabia inaitwa Anting yaani hufanya kitendo cha kwenda sehemu za siafu na hulala hapo ila wataalam hawajagundua kwanini iko hvi

Kawaida kunguru wanamate for life hawa ndege huwa hawacheat kabisaa.. na hata akifa mmoja mwingine hubaki mjane lakini kwenye familia huwa ni dume na jike tu,
na watoto wakishakua hulazimishwa kuingia kwenye makundi

Jike hutaga mayai 3-7 na huenguliwa baada ya siku 28 ambapo mtoto hukaa na wazazi kwa muda
life span ni miaka 15, kunguru wa Africa hafugikii maana anaamini sana kwenye uhuru

Follow us instagram Thewildlife_tz
View attachment 1087184
video download chini ya maelezo
je,Kunguru Wana lika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom