MoroGent
Senior Member
- Jan 10, 2018
- 146
- 460
Salam sana wakuu,
MFAHAMU DAVID ERNEST SILINDE NA UJIFUNZE KITU KUTOKA KWAKE
UONGOZI NA NYADHIFA ALIZOSHIKA
Ubunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Uongozi katika Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Uongozi wa Kamati za Bunge na Vyombo vingine
Mheshimiwa Silinde kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha jimbo la Tunduma kuanzia mwaka 2010 mpaka 2025 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ikumbukwe kwamba jimbo la Tudum ani jimbo lenye ushindani mkubwa na limeshawahi kuongozwa na vyama vya upinzani kwa muda mrefu. Kwa Mh. Silinde kuongoza hili jimbo kupitia CCM ni dhahili kuwa ana ushawishi mkubwa sana na anakubalika kwa wanachi wengi na chama chake katika kutekeleza ilani na ahadi zake za kuleta maendeleo jimboni hapo,
VITU VILIVYONIVUTIA KWA HUYU KIONGOZI
1. Maamuzi magumu na Uthubutu
2. Maono na Umahiri
3. Lifestyle yake
4.Uwezo wake wa Kujenga hoja
5. Ushawishi na Mafanikio
6. Utofauti (Uniqueness)
Wakuu, Natumai mu wazima wa afya tele. Awali ya yote mimi ni kijana wa ki-Tanzania na mzalendo kwa nchi yangu. Mimi ni msomaji wa vitabu hasa vinavohusu wasifu wa viongozi mashuhuri na michango yao kwenye Jamii. Pia ni mfuatiliaji wa viongozi hasa vijana wa Tanzania wanaofanya vizuri hasa kwa ajili ya kujifunza. Katika kipindi cha maiaka ya hivi karibuni nimekuwa nikimfuatilia na kujifunza kwa David Ernest Silinde na leo nimewiwa kumuongelea hapa jukwaani. Nitazungumza ninavyomfahamu na mambo niliojifunza kwake.
MFAHAMU DAVID ERNEST SILINDE NA UJIFUNZE KITU KUTOKA KWAKE
Hili ni jina maarufu nchini Tanzania, na ni miongoni mwa viongozi vijana wazalendo wenye mchango mkubwa katika maeneo mbalimbali, hasa katika siasa, kilimo na huduma za jamii. Kihistoria alizaliwa Julai 28, 1984 nyanda za juu kusini Mkoa wa Songwe, chimbuko lake ni kabila la Wanyamwanga wanaopatikana tarafa na kata ya Kamsamba, ambapo yeye anatokea Kijiji cha Mkonko katika kitongoji cha Mwami. Asili ya neno “Mwami” linamaanisha Kiongozi Mkuu wa jamii katika makabila mengi ya Tanzania wakiwemo wafipa, hii inaweza kumaanisha au kuakisi kaliba na sifa ya kuzaliwa kiongozi (Born-Leader) wa Silinde kutokana na mfanano wa jina na sehemu ambapo ni asili yake.
Elimu ya Msingi na Secondary: Mheshimiwa Silinde, Amesomea shule za kawaida kabsa za kitanzania ikiwamo Shule za Msingi Kilwa Masoko(wilaya ya Kilwa-Mkoa wa Lindi) na shule ya msingi Rungwa (Wilaya ya Ileje-Mkoa wa Mbeya, kwa sasa Songwe), Silinde ni Msemenari wa St. Marys kwa olevel na advance amesoma shule ngumu na maarufu nchini ya MINAKI secondary.
Elimu ya juu: Mh. Silinde amasoma vyuo vikuu viwili vikubwa nchini Tanzania. Kwanza kabisa mwaka 2006-2010 alihitimu shahada ya Biashara na Utawala(Bcom) katika Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam (UDSM) chuo kikuu pekee kikongwe na kibobezi nchini Tanzania. Pili, mwaka 2021-2024 alihitimu shahada ya Uchumi (BA Economics) katika chuo kikuu huria Tanzania (The Open University of Tanzani (OUT). Elimu hii ya Mheshimiwa Silinde aliyoipata chuo kikuu imekuwa chachu katika uongozi wake, na hii ni dhahili kwamba imechangia katika mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii nchini Tanzania.
Elimu ya juu: Mh. Silinde amasoma vyuo vikuu viwili vikubwa nchini Tanzania. Kwanza kabisa mwaka 2006-2010 alihitimu shahada ya Biashara na Utawala(Bcom) katika Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam (UDSM) chuo kikuu pekee kikongwe na kibobezi nchini Tanzania. Pili, mwaka 2021-2024 alihitimu shahada ya Uchumi (BA Economics) katika chuo kikuu huria Tanzania (The Open University of Tanzani (OUT). Elimu hii ya Mheshimiwa Silinde aliyoipata chuo kikuu imekuwa chachu katika uongozi wake, na hii ni dhahili kwamba imechangia katika mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii nchini Tanzania.
UONGOZI NA NYADHIFA ALIZOSHIKA
Ubunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ni vijana wachache sana wenye Tanzania wenye historia kama ya Mh. Silinde kisiasa, yeye alimaliza chuo kikuu 2010 akifanya harakati zake za siasa na chama cha CHADEMA na mwaka huo huo akafanikiwa kuwa mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2010-2015 akiwakilisha Jimbo la Mbozi Magharibi, Mwaka 2015-2020 akiwakilisha jimbo la Momba ambapo kwa awamu hii aliaminiwa zaidi na potential yake kuonekana zaidi hivyo mwaka huo huo (2015-2020) alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika lenye makao yake makuu Afrika Kusini jijini Johannesbug katika kitongoji cha Midrand.
Uongozi katika Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kuwa mbunge na kuaminiwa katika majukumu ya serikali ni vitu viwili tofauti, hapa wengi ni mashuhuda na mifano ni mingi kwamba wabunge wengi wameingia bungeni kwa awamu nyingi sana au kipindi kirefu na hawajawahi kupata Bahati ya kuteuliwa na mweshimiwa Raisi kuongoza wizara za serikali. Hii imekuwa tofauti kwa Mh. Silinde amabapo ameaminiwa na kuteuliwa uongozi katika wizara tatu tofauti; Ambapo December 9,2020 mpaka February 28,2023 alihuduma kama Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kuanzia March 1, 2023 mpaka August 30,2023 aliteuliwa na kuhudumu kama Naibu Waziri wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuanzia September 1, 2023 aliteuliwa na mpaka mwaka huu 2025 ameendelea kuhudumu kama Naibu waziri wizara ya Kilimo amabapo amendeleza agaenda muhumi za vijana kama Building a Better Tommorow (BBT) na Agenda 10/30 kuhakikisha kilimo kinakuwa kwa aslimia 10 ifikapo mwaka 2030 kwa kuchangia zaidi katika ukuaji wa Uchumi wa Taifa letu la Tanzania.
Uongozi wa Kamati za Bunge na Vyombo vingine
Kama nilivyotangulia kusema awali, kuwa mbunge ni kitu kimoja na kuwa kiongozi ni kitu kingine, Mheshimiwa Silinde akilitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa akiaminiwa katika nafasi mbalimbali Bungeni, upande wa kamati za Bunge amepata kuteuliwa kama Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini (2010-2015) na Kamati ya Bunge ya Budgeti (2015-2018). Ukichunguza kwa umakini utaona hizi ni kamati muhimu sana nan nyeti zinazotegemewa na taifa kiuchumi na kijamii hivyo kuhitaji watu makini kama yeye wanaoweza kushauri na kutoa maamuzi sahihi yenye maslahi mapana na mustakabali wa Taifa letu.
Uogozi wa Mh Silinde kwa sasa
Mheshimiwa Silinde kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha jimbo la Tunduma kuanzia mwaka 2010 mpaka 2025 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ikumbukwe kwamba jimbo la Tudum ani jimbo lenye ushindani mkubwa na limeshawahi kuongozwa na vyama vya upinzani kwa muda mrefu. Kwa Mh. Silinde kuongoza hili jimbo kupitia CCM ni dhahili kuwa ana ushawishi mkubwa sana na anakubalika kwa wanachi wengi na chama chake katika kutekeleza ilani na ahadi zake za kuleta maendeleo jimboni hapo,
Mh. Silinde, Akiwa katika nafasi hizi amekuwa akichangia masuala mbalimbali katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, akiwakilisha wananchi wa majimbo aliyoyaongoza kwa kipindi chote. Pia ni miongoni mwa wanasiasa vijana ambao wamejitokeza kwa nguvu katika kipindi cha hivi karibuni katika kuhimiza ajenda za maendeleo, haki na mtazamo chanya wa kifikra hasa katika uwekezaji wa kilimo kwa vijana wengi nchini Tanzania.
VITU VILIVYONIVUTIA KWA HUYU KIONGOZI
1. Maamuzi magumu na Uthubutu
Kwanza, Vijana wachache sana Tanzania, labda mmoja kati ya mia, amabao wanauwezo wa kuwa na uthubutu au ujasiri wa kuchukua maamuzi ya kugombea ubunge after chuo, wengi wetu tukimaliza tunawaza skills tulizozipata tuzitumie katika kuajiliwa, lakini huyu jamaa aliamua kuthubutu bila kujali umri na kipato akaenda kugombea na kufanikiwa kitu ambacho kimenivutia sana na ni somo kwa viajana wengi wenye fursa kama hii. Pili, kuhama CHADEMA na kujiunga na CCM ni maamuzi magum ambayo wanasiasa wengi wameshindwa na ata wakiweza hukosa msimamo na kurudi, kufanikiwa kwake kunaleta somo kwamba wananchi huchagua kiongozi na sio chama cha siasa, if you have qualities of leadership you will automatically being chosen regardless of your party, hii hunifunza msimamo, flexibility na kuwa bora always kwenye maisha.
2. Maono na Umahiri
David Silinde amekuwa kiongozi mwenye maono na mfano bora wa kijana mwenye ndoto kataka taifa lake, mfano mzuri ni kutoka chuo direct na kuanza kuaminiwa na vyama vya siasa, wananchi na taifa kutoka ubunge mpaka uwaziri si jambo la mzaha, amefanya kazi nzuri katika uongozi wa siasa na pia ameweza kufanya kazi kwa karibu na jamii. Katika kipindi cha uongozi wake, ameweza kutetea haki za wananchi na kutoa mchango muhimu katika kujenga taifa. Mfano ni Miradi ya mabilioni jimboni kwake na miradi na events nyinzi anazoongoza na kuwakilisha taifa katika wizara ya kilimo. Hii imenivutia sana kuishi ndoto na kufanya vizuri unapoaminiwa.
3. Lifestyle yake
Huyu bwana ana maisha flani yanavutia sana, kwanza sio limbukeni na wala mropokaji wa majukwaa ya kisiasa na mitandao ya kiamii, hivyo inafanya watu wengi wasimjue kwa mengi. Ni mtu strategic sana, ana busara, anazingatia utendaji zaidi kuliko maneno, ataonekana kwenye matukio muhimu na hana skendo za ovyo na hawezi kujikweza au kujimwambafai. Hii ndo style ya maisha napenda na natamani niyaishi, si ajabu ndo maana fursa nyingi zimemkuta, kwa hapa yeye ni roll model wangu
4.Uwezo wake wa Kujenga hoja
Nimemfatilia bungeni mara nyingi akiwa CHADEMA na akiwa CCM, hajawai kubadilikia uongeaji wake, ni mtulivu na anayeweza kutoa mawazo mtambuka na yenye sense. Kwa kipindi ambacho amekuwa naibu waziri amekuwa akijibu maswaki kwa kifupi, kwa kutumia data (statistics) na kwa usahihi zaidi, hiki kinaonesha ni jinsi gani alivomsomaji wa documents, mtafiti na mchambuzi wa mambo. Huwa najifunza sana kuwa well informed katika majukumu yangu na kuwa na majibu yasiyokuwa na maswali, reading and researching is a part and parcel of professional life.
5. Ushawishi na Mafanikio
Kitendo cha kuwa kiongozi wa kitaifa katika umri wake, kushika wadhifa wa ubunge kwa vipindi vitatu, hii ni dhahili na inaonesha mafanikio makubwa kwanza katika maisha yake binafsi, kiuongozi na taifa kwa ujumla. Hii inaonesha ushawishi wake ni mkubwa kwa watu wanaomzunguka na anaowaongoza. Hii ilinifanya nivutiwe kusoma kitabu cha "How to win friends and influence people" cha Dale Carnegie ili niwe kama Silinde
6. Utofauti (Uniqueness)
David Silinde ni kiongozi wa peke yake na moyo wa peke ake. Yeye ndo definition ya every person is unique. Niliwahi kukutana na mtu (mwalimu) alowahi kusaidiwa na Dave wakati akiwa TAMISEMI, aliponipa stori nikaishia kuamini kuwa huyu mwheshimiwa hasemagi uongo anapoongea, akikuahidi jambo linakuwa kweli na na unapomwamini anaaminika na unategemea. Nilijifunza ukipewa nafasi siku zote itendee haki na ukiaminiwa prove kwamba unaweza kuaminika.
HITIMISHO
David Silinde anayo nafasi muhimu katika siasa za Tanzania, na ameendelea kuwa kiongozi anayeonyesha kujitolea kwa taifa na jamii kwa ujumla. Mchango wake unajikita pia katika kuwatumikia wananchi na kwamba masuala ya kijamii yanapata kipaumbele.
Namuombea sana kwa MUNGU aweze kuendelea kuaminiwa na wananchi wa Jimbo lake, watanzania na mamlaka za uteuzi (RAIS) ikiwezekana awamu ijayo awe Waziri Kamili au hata Waziri Mkuu ili aendelee kutoa mchango wake katika taifa lake. Mimi binafsi nitaendelea kujifunza kwake na kupata motisha zaidi wa kupambania ndoto zangu katika utafutaji wa mafanikio.
Namuombea sana kwa MUNGU aweze kuendelea kuaminiwa na wananchi wa Jimbo lake, watanzania na mamlaka za uteuzi (RAIS) ikiwezekana awamu ijayo awe Waziri Kamili au hata Waziri Mkuu ili aendelee kutoa mchango wake katika taifa lake. Mimi binafsi nitaendelea kujifunza kwake na kupata motisha zaidi wa kupambania ndoto zangu katika utafutaji wa mafanikio.
HONGERA sana Mh. David Ernest Silinde, Mungu akubariki, aendelee kukutunza na nakutabiria mafanikio makubwa sana mbeleni
makubwa sana mbeleni
makubwa sana mbeleni